Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Ndugu wananchi !Kwa miaka mingi sana serikali ya Tanzania inatumia kodi ya vinywaji kuongeza mapato ya serikali. Katika kipindi cha Nyerere na cha Mwinyi, walipaji wakubwa wa kodi walikuwa ni viwanda vya vinywaji, hususa bia. Ukweli wa mambo utamaduni huu wa kutegemea kodi ya vinywaji hususa maji hauna faida kwa serikali na kwa jamii kwa sababu zifuatazo:-
Maji ni kitu muhimu kwa maisha ya binadamu. Unywaji wa maji masafi unapunguza magonjwa mbalimbali. Na kuwepo kwa kodi katika bidhaa hiyo kunasababisha maji ya chupa kuwa kitu cha anasa na hivyo kutumiwa na wale wenye uwezo. Hii ni fikra mbovu. Kinachotakiwa ni kuwa kabla mtanzania hajanunua vocha ya simu, awe na uwezo wa chupa ya maji.
Ni kweli punguzo la kodi litawasaidia wafanya biashara wa maji ya chupa. Lakini ni nani amesema kuwa watu wa kawaida hawatafaidika. Punguzo la kodi litafanya watu wengi kunywa maji safi. Na ongezeko la idadi litafanya ongezeko la uzalishaji ambalo litaongeza nafasi za kazi. Hivyo sioni sababu za kimsingi za kutopunguza au kuongoa kabisa kodi kwenye maji.
Wabunge mnapokuwa bungeni au kwenye magari yenu ya kifahari mna chupa za maji. Na ikitokea mtu kaiba chupa zako, hamkubali kuomba maji kwenye nyumba za wanyonge. Sasa kwanini kitu chenye manufaa kwa afya yenu mnakifanya kiwe adimu kwa walala hoi?
Mwishoni kodi ya maji haina faida kwa taifa. Hii ni kwa sababu, wanyonge wanaposhindwa kunywa maji safi au kujenga tabia ya kunywa maji safi, wanakunywa maji ambao yanawapa magonjwa. Na magonjwa yatokanayo na maji machafu yanatibiwa na mapato ya kodi. Hivyo serikali haipati faida yoyote hile.
Ni muhimu kwa watanzania kuelewa kuwa sio kila kodi ni muhimu kwa wananchi.Ndugu wabunge, wananchi, na wale wenye kufikiri kuwa kila kodi ni muhimu kwa taifa naomba wafikiri kuwa kodi ya chupa ya maji ni sawa na kodi kwenye kondomu. Unapoweka kodi kwenye kondomu, unafanya iwe na bei mbaya na kufanya masikini waache kutumia.Hivyo basi ningependelea kuwa chupa za maji zisiwe na kodi, au ikiwezekana serikali itoe ruzuku ili kila mtanzania awe na uwezo wa kunywa maji safi.
Wenu
Z10