Wabunge kujengewa nyumba kama mawaziri

Babu Lao

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
2,044
179
WABUNGE sasa watakuwa na makazi yao maalumu mjini Dodoma maarufu kama Bunge Estate, sawa na ilivyo kwa mawaziri jijini Dar es Salaam na Dodoma, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuweka bayana mpango huo kwa wawakilishi hao.

Mradi huo mkubwa na wa kisasa ambao umewakuna wabunge wanaohudhuria semina elekezi ya siku kumi, unatekelezwa kwa pamoja kati ya Ofisi ya Bunge na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), huku ukitarajiwa kuathiri biashara ya nyumba za kukodi na hoteli.

Kwa mujibu wa duru za habari za kuaminika kutoka katika semina hiyo kisha kuthibitishwa na Makinda, zilifafanua kwamba hatua iliyofikiwa hadi sasa ni mchoro wa ramani ya eneo la mradi, huku shabaha ikiwa hadi katikati mwakani kuwe na nyumba zilizojengwa.

"Ndiyo, huo mradi tulikuwa tukiujadili hapo ndani (ukumbi wa semina). Ni mradi ambao tutashirikiana na wenzetu wa NHC (Shirika la Nyumba)," alithibitisha Spika Makinda.

Kwa mujibu wa Makinda, kitu cha kwanza kilichokuwa kikifanyiwa kazi ni kupata eneo na sasa kinachofanyika ni michoro.
"Kuhusu gharama bado hatujapata kwa sababu ndio kwanza mradi uko hatua za awali," alisema.
Aliendelea kuwa, NCH kazi yao ni kujenga nyumba hizo huku Ofisi ya Bunge ikijipanga kurejesha fedha hatua kwa hatua kipindi cha miaka isiyopungua sita.

Spika Makinda alifafanua kwamba, wabunge watatozwa kiasi cha fedha kitakachoamuliwa kama sehemu ya kusaidia kurejesha deni hilo hapo baadaye.

Makinda akithibitisha hayo, duru za ndani ya semina zilizidi kuweka hadharani mpango huo kwamba, zitakuwa nyumba 350 ambazo kati ya hizo 200, zitakuwa kwenye muundo wa ghorofa na nyingine 150 za chini na hautakuwa mbali na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Kwa mujibu wa chanzo hicho huru, ili kuhakikisha nyumba hizo zinabaki kuwa mali ya Bunge, kila mbunge atakaa kwa muda wa miaka mitano na kuongeza: "ikimalizika unaondoka na familia yako."

Source:Mwananchi

Hapa kazi ipo!!!
 
kwa mtaji huu rushwa majimboni hazitaisha ili watu waende bungeni kuneemeka zaidi, Bunge nono katika nchi maskini kabisa duniani:-
a) Isiyo na umeme wa uhakika wakati huu wa karne ya 21.
b) Miundombinu - Ndege, Reli na Barabara dhaifu.
c) ......
d) .......
Nchi hii inafikiria zaidi kuwapa mawaziri na wabunge posho na mishahara minono ili wasiwabane watawala na wapitishe miswaada na mikataba bila kuhoji kama ina maslahi kwa taifa lao sababu wao wanashiba.
 
Kwa hiyo tutakuwa na wabunge wanaoishi kwenye nyumba za kifahari mjini Dodoma wakiongoza wananchi wanaoishi kwenye nyumba za tembe vijijini! Kweli wenye nacho huongezewa! Mwaka huu kazi ipo!
 
Je watakapomaliza bunge au watakapoacha kuchaguliwa tena hizo nyumba watarudisha au?
NA VIPI KILA ANAPOKUA AU WANAPOKUA WANAKUJA WABUNGE WAPYA WATAKUA WANAPEWA NYUMBA???
 
Nchi ya ajabu sana hii, hawa hawakumbuki hata shida kubwa ya foleni chanzo chake ni mipango miji ya hovyo wao wanataka kujengeana majumba tu duh shame on u makinda mi namtambua SITTA kama spika wewe walikuweka mafisadi!!
 
Sijui kama walifanya utafiti wa mabunge mengine katika nchi nyingine wanafanyaje kabla y akufikia mradi huu.Nilibahtika kutembelea makazi ya Wabunge wa Sweden huko Stockholm na nilivutika na kitu kimoja.Wana makazi ya kawaida kama hostel na vitanda vyao ni vidogo havizidi hata futi 2x6! nilishangaa sana maana lengo halikuwa kuwapa luxury bali kuwawezeshe kipindi cha bunge wawe kule na kupata mahali pa kulaza ubavu. Kipindi cha bunge kikiisha basi wanarudi makwao - Majimboni.Sasa hawa wetu wakipewa makazi kama haya kuna kurudi jimboni tena ikiwa wanahamia na familia zao?

SOMA HII:
Rent-free homes
For those Swedish MPs who live more than 50km (31m) from the centre of Stockholm, which is most of them, they are entitled to a rent-free second home owned by Parliament.
There are some 250 such apartments in the city and the political parties decide which of their members get one.
They are neither posh nor palatial but MP Jorgen Johannson, who lives in a block just off one of the main shopping streets, says that 50 square metres is plenty for him when he just uses the flat to sleep.
In his own words, he comes to Stockholm to work not to live.
Family members can stay but they have to pay. So nearly all MPs in Sweden have their main homes in their constituencies and a second home, if applicable, in the capital.
There is the option to buy your own pad in Stockholm and claim up to 7000 kronor a month, equivalent to about £600.
But MPs cannot claim for any improvements to their own apartments whereas the state pays for repairs and improvements to their own accommodation.
Instead of taking work home with them, the political parties often allocate new MPs ready-made homes at work.
With their single beds, kitchenettes and en-suite shower rooms, they are reminiscent of student digs.
But in terms of value for money no doubt very cost effective.
There is a daily subsistence rate for MPs representing constituencies outside Stockholm of 110 kronor a day - just under £10 - to cover travel expenses. With an overnight stay, the daily rate is 360 kronor (£31).
No relatives
All the expenses are administered by a Board of the Parliament made up of 10 MPs.
They suggest the rules and Parliament approves them occasionally by a vote. Home office costs are covered but individual MPs don't receive a set staffing allowance.
Instead, the parties they represent get a pot of money which they allocate to their members to cover staffing and other office related expenses.
This means many MPs share researchers and secretarial staff.
Almost no MP in Sweden employs family members. There is no written rule against it but it is just something they do not do.
And just to make sure that Parliament is for working not playing, there are no bars in the building.

So no scenes of drunk Swedish MPs swaying through the corridors of power.
Instead, there is a swimming pool and sauna to relax in after a hard day's work.
 
Mtu akimaliza muhula wake na hana uhakika wa kurudi lazima atafanya uharibifu tuu!
 
WABUNGE sasa watakuwa na makazi yao maalumu mjini Dodoma maarufu kama Bunge Estate, sawa na ilivyo kwa mawaziri jijini Dar es Salaam na Dodoma, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuweka bayana mpango huo kwa wawakilishi hao.

Mradi huo mkubwa na wa kisasa ambao umewakuna wabunge wanaohudhuria semina elekezi ya siku kumi, unatekelezwa kwa pamoja kati ya Ofisi ya Bunge na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), huku ukitarajiwa kuathiri biashara ya nyumba za kukodi na hoteli.

Kwa mujibu wa duru za habari za kuaminika kutoka katika semina hiyo kisha kuthibitishwa na Makinda, zilifafanua kwamba hatua iliyofikiwa hadi sasa ni mchoro wa ramani ya eneo la mradi, huku shabaha ikiwa hadi katikati mwakani kuwe na nyumba zilizojengwa.

"Ndiyo, huo mradi tulikuwa tukiujadili hapo ndani (ukumbi wa semina). Ni mradi ambao tutashirikiana na wenzetu wa NHC (Shirika la Nyumba)," alithibitisha Spika Makinda.

Kwa mujibu wa Makinda, kitu cha kwanza kilichokuwa kikifanyiwa kazi ni kupata eneo na sasa kinachofanyika ni michoro.
"Kuhusu gharama bado hatujapata kwa sababu ndio kwanza mradi uko hatua za awali," alisema.
Aliendelea kuwa, NCH kazi yao ni kujenga nyumba hizo huku Ofisi ya Bunge ikijipanga kurejesha fedha hatua kwa hatua kipindi cha miaka isiyopungua sita.

Spika Makinda alifafanua kwamba, wabunge watatozwa kiasi cha fedha kitakachoamuliwa kama sehemu ya kusaidia kurejesha deni hilo hapo baadaye.

Makinda akithibitisha hayo, duru za ndani ya semina zilizidi kuweka hadharani mpango huo kwamba, zitakuwa nyumba 350 ambazo kati ya hizo 200, zitakuwa kwenye muundo wa ghorofa na nyingine 150 za chini na hautakuwa mbali na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Kwa mujibu wa chanzo hicho huru, ili kuhakikisha nyumba hizo zinabaki kuwa mali ya Bunge, kila mbunge atakaa kwa muda wa miaka mitano na kuongeza: "ikimalizika unaondoka na familia yako."

Source:Mwananchi

Hapa kazi ipo!!!

Hivi hawa wabunge wetu wanaelewa kwanini huwa tunawachagua??

Kujengewa nyumba dodoma wakaishi na familia zao maana yake hawataishi tena majimboni kwao??? watajuaje matatizo yetu?

Eti tatajengewa ghorofa, je wabunge waliopita hawakuwa na utendaji mzuri kwa sababu ya kutokuwa na nyumba DODOMA?

Je kama watakuwa na makazi dodoma posho zitafutwa?????

Hawa wabunge nao kama hawawezi kuona kuwa nchi haina hela za madawa, madawati, kutoa maji safi na vingine vingi lakini wakasisitiza kujengewa nyumba huku wakilipwa POSHO KUBWA basi nao ni MAFISADI.

Ebu tuone kama atasimama hata mbunge wa upinzani kukataa mpango huu usio na tija kwa taifa!

Kumbukeni wanyonge wakiamuka kudai mali za nchi yao wote mtatafuta pa kwenda. Watanzania wanachukua Tuition kwa yanayotokea MISRI!

For the record: Hatupingi wabunge kuwa na nyumba hata kama watakuwa wanalipa pango, tunapinga ujenzi huo kwa sasa manake nchi ina matatizo makubwa kuliko haya ya makazi ya wabunge.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Msisahau kutuwekea na gym, manake lazime zipigike humo mjengoni kisa tumefumaniana ucku kwenye korido magorofani kwetu 'Bunge Estate'...teh ....teh!
 
WABUNGE sasa watakuwa na makazi yao maalumu mjini Dodoma maarufu kama Bunge Estate, sawa na ilivyo kwa mawaziri jijini Dar es Salaam na Dodoma, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuweka bayana mpango huo kwa wawakilishi hao.

Mradi huo mkubwa na wa kisasa ambao umewakuna wabunge wanaohudhuria semina elekezi ya siku kumi, unatekelezwa kwa pamoja kati ya Ofisi ya Bunge na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), huku ukitarajiwa kuathiri biashara ya nyumba za kukodi na hoteli.

Kwa mujibu wa duru za habari za kuaminika kutoka katika semina hiyo kisha kuthibitishwa na Makinda, zilifafanua kwamba hatua iliyofikiwa hadi sasa ni mchoro wa ramani ya eneo la mradi, huku shabaha ikiwa hadi katikati mwakani kuwe na nyumba zilizojengwa.

"Ndiyo, huo mradi tulikuwa tukiujadili hapo ndani (ukumbi wa semina). Ni mradi ambao tutashirikiana na wenzetu wa NHC (Shirika la Nyumba)," alithibitisha Spika Makinda.

Kwa mujibu wa Makinda, kitu cha kwanza kilichokuwa kikifanyiwa kazi ni kupata eneo na sasa kinachofanyika ni michoro.
"Kuhusu gharama bado hatujapata kwa sababu ndio kwanza mradi uko hatua za awali," alisema.
Aliendelea kuwa, NCH kazi yao ni kujenga nyumba hizo huku Ofisi ya Bunge ikijipanga kurejesha fedha hatua kwa hatua kipindi cha miaka isiyopungua sita.

Spika Makinda alifafanua kwamba, wabunge watatozwa kiasi cha fedha kitakachoamuliwa kama sehemu ya kusaidia kurejesha deni hilo hapo baadaye.

Makinda akithibitisha hayo, duru za ndani ya semina zilizidi kuweka hadharani mpango huo kwamba, zitakuwa nyumba 350 ambazo kati ya hizo 200, zitakuwa kwenye muundo wa ghorofa na nyingine 150 za chini na hautakuwa mbali na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Kwa mujibu wa chanzo hicho huru, ili kuhakikisha nyumba hizo zinabaki kuwa mali ya Bunge, kila mbunge atakaa kwa muda wa miaka mitano na kuongeza: "ikimalizika unaondoka na familia yako."

Source:Mwananchi

Hapa kazi ipo!!!

Huu ni uchakachuaji mali za wapiga kura. baadae watasema kila mbunge akimaliza muda wake wanamuuzia nyumba yake kwa bei ya kutupa.
 
Mtu akimaliza muhula wake na hana uhakika wa kurudi lazima atafanya uharibifu tuu!

Umenikumbusha ya Masha!!!!!!! Ila hilo linchi lina laana!!!!!!!!! yaani katika ufisadi uliotukuka bado kuna watu wanafikiria kikomunisti kikomunisti!
 
Wazo zuri ila shaka inakuja kwenye uadilifu wa watu wetu. Kama kweli watu wangekuwa na nia thabiti ya kuboresha makazi ya Wabunge hapo Dodoma ingependeza lakini sasa hivi utakuta ndo unakuwa mradi wa kujinufaisha watu wachache. Wazo la kujenga nyumba ya familia mimi siliafiki, labda ingependeza kama zitajengwa kwa kila mbunge kuwa na chumba ambacho ni self contained (kikawa na jiko, bafu, choo, sebule na chumba cha kulala) kwisha! Siyo lazima ahamie huko na familia yake nzima bwana. Haya yatakuwa matumizi mabaya ya fedha za umma!

Na wazo la kurudisha gharama hilo halipingiki, ni lazima walipie japo kwa gharama nafuu na mahesabu yapigwe kwa muda wote atakaokuwa madarakani atozwe kila mwezi hata kama hakuna kikao cha bunge endelee kulipia pango. Maana najua wakati usiokuwa wa vikao hakuna mbunge atakayekaa Dodoma bwana hapa tunataka kudanganyana,kwa hiyo kujenga majumba makubwa ya familia itakuwa ni kuharibu raslimali za walipa kodi.

Huu uwe kama mradi wa ofisi ya Bunge. Fedha inakatwa na kuwekwa kwenye mfuko maalum ila sina uhakika kama mafisadi hawataufilisi mfuko huu. Hapo ndo tutasikia ofisa fulani wa Bunge amekwapua mamilioni yetu ya mradi.
 
Hebu tungoje tuone kama wakina Myika nao wataingia kwenye mtego wa rushwa za nyumba kwa wabunge. Haingii akilini kuwajengea nyumba wabunge ili waishi na familia zao Dododma wakati wanapokuwa Dodoma wanakuwa kazini muda wote juu ya hayo makazi yao sio Dodoma bali kwenye majimbo yao, lingekuwa jambo la busara kama Bunge lingejenga hostel kama pale Veta ambapo wabunge wengi wanakaa wakiwa bungeni; mradi kama huo ungekuwa cost-effective. Makinda ana madeni benki nadhani ameusukuma mradi huu ili apate pa kutokea kulipa hayo madeni!! Huyu kawekwa na mafisadi naye pia ana harufu yao lazima mumstukie kabla hajakubuhu.
 
Nashauri mpango huo, mpango wa kuwajengea nyumba wabunge, UACHWE MARA MOJA.

Wabunge wenye uchungu na nchi yenu PINGENI MPANGO HUO, PINGENI KWA NGUVU RUSHWA HIYO.
 
Kwa mujibu wa chanzo hicho huru, ili kuhakikisha nyumba hizo zinabaki kuwa mali ya Bunge, kila mbunge atakaa kwa muda wa miaka mitano na kuongeza: "ikimalizika unaondoka na familia yako."

Kwani huko Dodoma ndiyo wanapokaa!!!! Hata Komandoo Hamza Kalala aliimba Dodoma wanaenda na kurudi, Wabunge wanakaa Darisalaam! wakati walitakiwa wakae majimboni kwao, wastage of our money again, kipindi wakiwa hawana Bunge Session nyumba wanakaa nani popo au wanapangisha? Jamani wangewajengea nyumba walimu au wafanyakazi baada ya kuwachakachulia nyumba za kwanza, wabunge kupoteza hela zetu tu
 
Huu ndio ufisadi wenyewe hivi Tanzania tutazinduka lini kuyaondoa madudu haya? Tunajenga nyumba kwa mabilioni kwa mtu atakayekuja kukaa for two years to five years? Kwanini asipewe allowance ambayo ni standard kama wenzetu nchi zilizoendelea wanavyofanya? Au wachukue mikopo ya kununua nyumba wenyewe kama wanataka.
 
Zile nyumba walizokuwa wanajenga kuhamishia makao makuu zinafanya shughuli gani? Wabunge ni the most highly paid people in Tanzania kwa nini walipa kodi waendelee kugharamia mahitaji yao mengine? Hii ni rushwa ili wanyamaze.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom