Wabunge kataeni lugha hizi za kilaghai!!!

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini mabunge yetu. Moja kati ya mambo ambayo yananishangaza sana ni kauli za spika mama Anna Makinda kipindi anapoongoza bunge au mawaziri kipindi wanapojibu maswali bungeni kama ifuatavyo;

1.0 Mh. Mbunge tunaomba muda zaidi kwa ajili ya kushughulikia suala hili!!!!! Ukifika muda hakuna cha maana kinachootolewa taarifa!!!!

2.0 Mh. Mbunge naomba uthibitishe kauli yako au madai yako. Wabunge wanapothibitisha kauli zao huficha ukweli kama walikuwa wamekosea au laaah! Mfano ni suala la G. Lema mpaka leo hakuja ajuaye rasmi kama uthibitisho wa Lema umetosha kumtia hatiani waziri mkuu au Lema alichemka na hivyo alipaswa kuadhibiwa kwa kumtuhumu PM uongo!!!!!
Wanapodai ushaidi wanadai kwa mbwembwe lakini wakiletewa wanakuwa wanyonge!!!!!

3.0 Tunalifuatilia suala hilo kwa makini na muda ukifika tutawajulisha, au suala hilo bado lipo kwenye uchunguzi.

Natoa wito kwa wabunge kukataa kauli hizo kwani ni za kilaghai na hazina tija kwa kwenu na wananchi zaidi ya kutuliza mambo yanapokuwa arijojo!!!!!! Kauli hizo zimekuwa zikificha ukweli, na kwa kiasi fulani kuwa adui wa demokrasia kwa kuwa zinatumia kama kitisho kwa wabunge hasa kauli No. 2.

Mfano wa kumalizia ni suala la Filikunjombe, unaweza kuona jinsi anavyotakiwa kwa mbwembwe alete ushahidi lakini siku akileta unakaliwa na hakuna mrejeshonyuma (feedback) jambo ambalo linaweza kutafsiriwa kama kitisho dhidi ya kusema ukweli!!!

Wabunge kataeni kwa kuwa wakali pindi mnatajiwa kauli kama hizo kwa kutoa mifano hai iliyopo ili zikome kutumika bungeni bila kumananisha.

Naomba kuwakilisha.
 
Back
Top Bottom