Wabunge CHADEMA, Posho mliyoikataa, mnaifanyia nini?

Ni vizuri kusema ukweli au kukaa kimya kama hujui ukweli. Toka tarehe 8 Juni 2011 sichukui posho za vikao. Posho haiingizwi kwenye akaunti kwa lazima kama tunavyoambiwa hapa jukwaani. Mbunge husaini fomu maalumu za kuonyesha amehudhuria kikao na kutokana na fomu hizo hulipwa posho. Mimi nimekataa kusaini fomu hizo ili Ofisi ya Bunge isiwe njia ya kuniingia fedha hizo kwenye akaunti yangu. Hivyo sipokei Posho za Vikao kwa kuwa sisaini fomu za maalumu za posho.

Sio kwenye Bunge tu, sipokei posho kwenye viako vyote ninavyoalikwa kama Mbunge au ambavyo mimi ni mjumbe kutokana na wadhifa wangu. Nimekataa posho ya kikao katika kikao cha Bodi ya Barabara Kigoma, Kamati ya Ushauri ya Mkoa Kigoma na Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Kigoma. Vilevile nimekataa posho za kikao kwenye semina ya CAG kuhusu kamati za Bunge. Ukipenda kuona ushahidi wa risiti (stakabadhi) za posho nilizokataa nenda katika blogu yangu Zitto na Demokrasia

Uamuzi wa kukataa malipo makubwa kwa wabunge ni uamuzi wa kisera wa chama chetu. Mimi ninatakeleza maagizo ya chama kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA. Hili sio suala la Zitto ni suala la chama. Zitto ni msemaji tu wa suala hili kwa sababu ni Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi na kwa kweli lazima niwe mbele kutekeleza maamuzi ya chama kivitendo.

Nimejuaje kama posho zilipanda? Nilijuaje mkataba wa Buzwagi umesainiwa? Slaa alijuaje kuna wizi wa EPA Benki Kuu? Nilijuaje kuna mabilioni yamechotwa kupitia kampuni ya meremeta? Nadhani hapa utajua kuwa Mbunge yeyote makini ana vyanzo vingi vya habari

Nduguyo Zitto

Ka ulivyosema ni sera ya chama, inabidi uje utuambie kama Naibu K/Mkuu mmechukua hatua gani kwa wabunge wanaozipokea!?
 
jumakidogo umeelewa?

Maelezo ya mh Zitto yanaeleweka lakini bado kuna maswali yanatambaa na kuisakama akili yangu. Kama suala la posho ni sera ya chama, mbona misimamo ya baadhi yao inatia mashaka? Kwa mfano Mh Shibuda, yeye alitetea posho tena kwa mbwembwe nyingi huku akishangiliwa na wabunge wa CCM. Hapa bado napata shida, kama ni sera na msimamo wa chama kwa ni isitoke kauli moja yenye maamuzi ya mwisho?
 
Back
Top Bottom