Jumakidogo
R I P
- Jul 16, 2009
- 1,851
- 417
Kwa bahati nimeamua kuwa siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa bali ni shabiki wa siasa na baadhi ya wanasiasa. Mfano halisi wanasiasa ninao wakubali bila kujali itikadi zao ni Mbowe, Slaa, Mnyika, Lissu, Magufuli, Lowassa nk. Napata fursa ya kuwa makini na kauli za wanasiasa wa nchi hii bila kujali chama atokacho. Wabunge wa CDM Wamekuwa na msimamo wa kutopokea posho zao katika vikao vya bunge. Msimamo ambao wananchi tulio wengi tunauunga mkono mia kwa mia. Lakini utaratibu wa malipo ya posho hizo ni halali kwa mujibu wa kanuni za bunge. Na bahati mbaya hawapewi mkononi hivyo huingizwa moja kwa moja kwenye akaunti zao. Kwa maana ya kwamba watake watapata, wasitake watapata. Ule msimamo wa dhati upo kweli? Manake sijasikia tena wakija na mpango hasi kuhusu posho hizo kuwa, kwa sababu tulizikataa lakini mnatulazimisha. Tunaziingiza katika mradi fulani wa wananchi. Vinginevyo tunarudi kulekule kuwa. Kauli zitokazo midomoni mwa wanasiasa ni tamu masikioni mwa wananchi, lakini kuna dhamira tofauti katika mioyo yao.