Wabunge angalieni hili la VAT kwenye nyumba za kuishi

HISIA KALI

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
694
108
Kifungu hiki cha bajeti kingefaa kuweka nafuu ya kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili wananchi waweze kujenga nyumba bora za kuishi kwa bei nafuu. Hii ya kusamehe tu kodi ka NHC haitoshi kwani ni wananchi wachache sana wenye uwezo wa kununua nyumba NHC, pia NHC sina uhakika kama ina uwezo wa kujenga nyumba nyingi kukidhi mahitaji ya wananchi wa mijini na vijijini. Wananchi wengi wanajijengea nyumba zao taratibu kulingani na kipato chao.

A. Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148

vi) Kuondoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye kuuza na kupangisha majengo ya kuishi ya nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
 
wanajitafutia unafuu wakuzidi kutumia rasilimali zetu, wanajua kabisa watapangishana wenyewe na watauziana wenyewe.
bora kweli kama wana dhamira ya dhati wapunguzekodi kwenye vifaa vya ujenzi.
 
Hawa! wataua sekta binafsi ambayo inaajiri Watanzania wengi zaidi. Kweli tutakoma.
 
wahindi ndio wanapunguziwa kodi kimtindo maana wengi wao mikoa yote asilimia kubwa sana kwenye hizo nyumba wanaishi wahindi na wale amabao wamepangishwa na watu binafsi kwa pesa kubwa (cha juu).......Najuta kuwa na serikali kama hii
 
HTML:
Kifungu hiki cha bajeti kingefaa kuweka nafuu ya kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili wananchi waweze kujenga nyumba bora za kuishi kwa bei nafuu. Hii ya kusamehe tu kodi ka NHC haitoshi kwani ni wananchi wachache sana wenye uwezo wa kununua nyumba NHC, pia NHC sina uhakika kama ina uwezo wa kujenga nyumba nyingi kukidhi mahitaji ya wananchi wa mijini na vijijini. Wananchi wengi wanajijengea nyumba zao taratibu kulingani na kipato chao.

A. Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148

vi) Kuondoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye kuuza na kupangisha majengo ya kuishi ya nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Hicho kifungu kina maana kwamba, kabla kulikuwa na msamaha wa VAT, lakini sasa wanapendekeza msamaha huo ufutwe.
 
Back
Top Bottom