Wabunge 46 na mawaziri 13 wahamasisha wananchi kutaka JK ajiuzulu

Hawa wabunge ndio wawe kwanza kujiuzulu,wewe angalia wabunge asilimia 90% wanakaa Dar watajua vipi matatizo ya wananchi mpaka ifike wakati wa uchaguzi ndio wanaanza kusema.
Imebaki miezi tu kufika uchaguzi ndio wanaamka kutoka usingizini na ndio wanarudi ktk majimbo yao.
Hawa ndio wakupingwa chini hakuna kuwapa kula kabisa.
Nchi imeanza kuliwa siku nyingi sio Kikwete
 
Waswahili husema ukiona moshi wafukuta, ujuwe moto waja...
Haya ndo matokeo ya dhambi ya ubaguzi aliyoyasema hayati mwalimu Nyerere,wao walijitenga na wenzao ndani ya chama,wakaunda mtandao.sasa ktk mtandao huo walikuwa na malengo tofauti kila mmoja. wapo waliofikiri ndo njia ya kutokea kimaisha,wapo waliokuwa na dhamila njema ya kulitumikia taifa, Sasa wale ambao wametolewa kafara na kukwaruzwa na ajali za kisiasa kwa njia moja au nyingine lazima waendeshe harakati kama hizo.
 
well mkuu hayo yote uyasemayo ni ya kweli hila nimdhaifu na yeye in terms of kukemea watumishi walio chini yake ndio maana kama kuna ukweli kwenye hii ripoti ni bora achukue tu hiyo pension plan yake ajipumzikie.

alianza kazi vizuri na sifa nyingi hila sasa Tanzania imekua gunia zito kwake bora amuachie mchukuzi mwingine. usiseme hili ukafanya vile kunyuma ukadhani wewe ni invisible wapi vita yake na rushwa ya nchini bado ipo palepale tu, wapi maendeleo ya mtanzania amna lolote.

jasiri angewaambia watu wote wenye shutuma inabidi muachie wadhifa kwani watanzania inavyoonekana hawana tena confidence na nyie na nyadhifa zenu. kwake yeye ni sawa tu watanzania ni waongeaji tu watasahau amna kusahau sasa kwa watu wanaotuletea umaskini kama ingekua ni nguvu yetu mkapa angekua wa kwanza hata kabla ya mahakamani arudishe asset za tanzania yeye na mkewe wote.

na aondoke tunahitaji kiongozi mwenye nia na maendeleo ya kweli sio mtu anaelitia hasara taifa wakati mataifa mengi africa sasa yana anza kuwa serious nakuanza vita ya kweli kujisaidia wenyewe na mariasili walizo nazo bora nahodha apumzike kwa faida yake yeye na kwa maendeleo yetu sisi. hila atutaki kiongozi mwingine tena aje na absolute power nguvu za raisi ni lazima zipunguzwe kwa yeyote atakaekuwa in the future vinginevyo huu upuuzi wa ufisadi utajirudi tuu.
 
Dawa ya kuondokana na huu mfumo mbovu ni kuwaondoa kwa nguvu madarakani, tukisema ustaarabu hawa mafisadi hawajui ustaarabu na hilo hawatalikubali litokee.Kwa kuwa wanajua wazi siku Mtanzania anashika wajibu wa kuwawajibisha viongozi waliopo madarakani huo ndio utakao kuwa mwisho wao na mali walizochuma kwa njia ya uovu.

Ili watanzania waweze kupata uhuru wao wa kiuchumi ni lazima nguvu itumike kuondoa huu uozo madarakani.Hawa watu wako wengi na wote wataendelea kulindana tuu hata aje nani,dawa ni kuwang'oa madarakani.
 
kulindana wana lindana that is obvious kama ulivyoona mkuu wa takuruku kashapewa clear ya uzembe ndio ujue mzunguko ni mkubwa in fact desturi yao tangu Mwinyi awe madarakani.

lakin lazima huu approach vitu hivyi kwa namna ya ukweli ujue kwamba kote madarakani sehemu kuu jeshi na ufisadi wao,polisi na cover story zao, gavana wa fedha ndio ng'ombe wao wakuwa kamulia mali hasili. sheria wanatunga wao, asset zetu wanajipa wao kutumia nguvu zao. sijui utakuja na njia gani hapo zaidi ya bunduki ni kitu ambacho kitawatesa watanzania wengine wasio jali ata hiyo siasa yenyewe. na nani atakae kuuzia kwanza na hiyo hela utaitoa wapi. kwani kuna watu wanao monitor tanzania fromoutside for their interest.

kitu cha kuzingatia kama unavyoona bungeni kuna baadhi ya wabunge ambao wana oppose sera zao lakini hawana madaraka ya hivyo na wengi ufikiria hatima zao iwapo mambo yenyewe uishia wao kupata ajali za magari alafu amna anae kamatwa wameshaona mifano ya wenzao sasa mtu mwenye akili timamu lazima ajiulize mara mbili na wanangu atawalisha nani litakalo nikuta. hii ndio line niifikirio yayo mimi kuwapa sauti bila ya uwoga hawa wabunge kwani nguvu yao ndio itatusaidia na namna moja wapo ni kuwa na vyombo vingine independent venye nguvu yakupambana na serikali, sasa basi si wabunge sehemu nyingi tu wapo hawa watu maloya na majaji, mapolisi, wanajeshi etc we punguza nguvu zao tu utawaona watanzania wenye madaraka watakavyo pambana nao na namna moja ni open transparency kwenye kila cha taifa apart from national security matters.

au labada upinzani uwe serious waunde chama kimoja ndio hapo wawape watanzania choice ya kweli ya kupambana na CCM vinginevyo ni hadithi hadithi tu.
 
Kachero, katiba ya Tanzania inaruhusu Bunge kumuondoa Rais madarakani wakati wowote endapo itadhihirika ameshindwa kutekeleza majukumu yake. Kwa hiyo hakuna haja ya kutumia nguvu na mabavu wakati huu ambapo ni dhahiri hatua kama hiyo inafaa kuchukuliwa.

Ibara Na. 46A(1) ya Katiba yetu, Toleo la 2005 inasema:
"Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii".

Masharti ya hiyo ibara yanaendelea kueleza kwamba hoja hiyo haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais:-
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria
ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo vinavyokiuka maadili yanayohusu uandikishwaji
wa vyama vya siasa......
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya
Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi 12
tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge'.

Rais wetu kwa kutochukua hatua kuwapeleka mahakamani mafisadi waliotajwa na Kamati mbalimbali za Bunge na kuidhinishwa na vikao vya Bunge, ni kukiuka Katiba. Hata pale alipoamuru wale wahalifu waliokwapua fedha za EPA wazirejeshe na wasiadhibiwe zaidi, ni ukiukaji wa Katiba.

Kwa hiyo hawa Wabunge 46 na Mawaziri 13 wanaohamasisha wananchi kuwaunga mkono ili hoja ya kumuondoa madarakani Rais wanafanya kitendo cha ushujaa na wa kizalendo. Kumekuwa na vacuum katika uongozi wa nchi hii. Wahalifu kama Bwana "Vijisenti", wanaohusishwa kimataifa na ufisadi wa Rada na ukwapuaji wa dhahabu ya nchi hii katika Kashfa ya Meremeta, wangali Bungeni na wanakula na Rais.Serikali yake hata imeshindwa kuadhibu wezi wa Migodi ya Mkaa wa Mawe wa Kiwira, eti hata kujaribu kuwa compensate majizi kama BM na Yona.

Bunge likiruhusu Serikali iliyolala kama hii kuendelea mpaka Oktoba 2010, tutakuta raslimali zetu zote zimerithishwa kwa wawekezaji wa nje wakishirikiana na mafisadi wa ndani. Sasa ni wakati wa kuwaondoa before it is too late.
 
Ni vema Rais akajiokoa kwa kuisafisha Serikali na CCM kuwaondoa mafisadi wanaoinyonya Nchi kama kupe.
 
Hebu tushushi hiyo list ya hao mafirauni maana naamini kutakuwepo na mkono wa kina Rostam na E L
 
Si rahisi kwa wabunge wa sisiem (ambao wengi wameingia madarakani kwa rushwa) kumng'oa mwenyekiti wa chama chao (ambaye ni raisi wa jamhuri) kwa sababu za kutowajibika. Hili haliwezekani kwa aina ya wabunge tulionao.
Lakini kama mtakumbuka vema, Mchungaji William Mwamalanga Mgala alikuwa mmoja wa wachungaji (na Mchungaji Mtikila akiwemo) walioitisha mkutano na waandishi wa habari wakipinga kitendo cha Mheshimiwa Rostam Aziz kujisafisha kanisani wakati akizindua albamu ya kwaya pale Kinondoni.
Kwa hiyo kelele za huyu bwana hazijaanzia hapa, zimetoka mbali kidogo katika harakati hizi.
 
Mmeambiwa ni mafisadi.

Kwa hiyo jaribuni kuorozesha list ya wabunge 46 na mawaziri 13 mafisadi then jibu mnalo.
 
Rais anaondoka!

Haiko ndani ya uwezo wake tena kuzuia hali hii.

Kawashindwa mafisadi hata yeye anajua jambo hilo.

He has no choice and no body can intercept that!!

He has to go!!

As a Person Jakaya Mrisho Kikwete is very ok and very fine...

BUT

He has to strp down as a president!!!

God Bless Him
 
Kachero, katiba ya Tanzania inaruhusu Bunge kumuondoa Rais madarakani wakati wowote endapo itadhihirika ameshindwa kutekeleza majukumu yake. Kwa hiyo hakuna haja ya kutumia nguvu na mabavu wakati huu ambapo ni dhahiri hatua kama hiyo inafaa kuchukuliwa.

Ibara Na. 46A(1) ya Katiba yetu, Toleo la 2005 inasema:
"Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii".

Masharti ya hiyo ibara yanaendelea kueleza kwamba hoja hiyo haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais:-
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria
ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo vinavyokiuka maadili yanayohusu uandikishwaji
wa vyama vya siasa......
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya
Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi 12
tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge'.

Rais wetu kwa kutochukua hatua kuwapeleka mahakamani mafisadi waliotajwa na Kamati mbalimbali za Bunge na kuidhinishwa na vikao vya Bunge, ni kukiuka Katiba. Hata pale alipoamuru wale wahalifu waliokwapua fedha za EPA wazirejeshe na wasiadhibiwe zaidi, ni ukiukaji wa Katiba.

Kwa hiyo hawa Wabunge 46 na Mawaziri 13 wanaohamasisha wananchi kuwaunga mkono ili hoja ya kumuondoa madarakani Rais wanafanya kitendo cha ushujaa na wa kizalendo. Kumekuwa na vacuum katika uongozi wa nchi hii. Wahalifu kama Bwana "Vijisenti", wanaohusishwa kimataifa na ufisadi wa Rada na ukwapuaji wa dhahabu ya nchi hii katika Kashfa ya Meremeta, wangali Bungeni na wanakula na Rais.Serikali yake hata imeshindwa kuadhibu wezi wa Migodi ya Mkaa wa Mawe wa Kiwira, eti hata kujaribu kuwa compensate majizi kama BM na Yona.

Bunge likiruhusu Serikali iliyolala kama hii kuendelea mpaka Oktoba 2010, tutakuta raslimali zetu zote zimerithishwa kwa wawekezaji wa nje wakishirikiana na mafisadi wa ndani. Sasa ni wakati wa kuwaondoa before it is too late.

well mkuu, asante kwa kunielimisha hapo mimi binafsi hilo geni kwangu hila kama bunge lina nguvu hizo je kwa nini hawafanyi maamuzi hayo wazi wazi na hao wabunge wakasema freely wanavyoona mbele ya wabunge wenzeo sehemu inayo husika "bungeni". Mpaka wapitie sehemu za nyuma clearly kwa maelezo yako ni rahisi basi kumtoa huyu bwana na sheria alioivunja umeitoa.

why wameshikamana na kutaka kupewa ukweli ambao mpaka dakika hii unawakwepa na amna lolote la maana linaloendelea kufikia mwisho wa kesi za ufisadi. kwa upande wangu hilo ni tatizo kama wabunge hawaamki basi na sisi tunalazwa bila ya majibu. Hila kama tungekua na strong sectors ambazo ni independent of parliament interference labda tungepata na upande wao pia wa-hizi habari. kwa hivyo tusi rely na sehemu moja tu, ambayo clearly aifanyi kazi yake vizuri. kwani wezi tunao washutumu wengi ndio wamo jumba hilo hilo. lazima tujifunze kuwabana au nitumie msemo wa kujipa sauti sisi watanzania. na sauti yetu tusitegeme jibu la chombo kimoja, hivyo bunge na raisi wake lazima liturudishie baadhi ya sauti zetu. nguvu ziongezwe kwenye vyombo vingine kama polisi, judiciary ishirikiane na polisi closely katika maswala haya na raisi wa tanzania asiwe na hati au mtu yeyote asiwe na sauti ya kuingilia upelelezi wao. yaani sehemu nyingi inabidi zihusike katika maslahi yetu si bunge tu. Kwani hili tatizo linatokana na sehemu na mtu mmoja kuwa na nguvu za ajabu nchini kwetu. leo tunasema kwanini ana walinda why yeye JK ndio awe sauti ya mwisho hilo ni tatizo tunalojitakia.
 
Kachero, katiba ya Tanzania inaruhusu Bunge kumuondoa Rais madarakani wakati wowote endapo itadhihirika ameshindwa kutekeleza majukumu yake. Kwa hiyo hakuna haja ya kutumia nguvu na mabavu wakati huu ambapo ni dhahiri hatua kama hiyo inafaa kuchukuliwa.

Ibara Na. 46A(1) ya Katiba yetu, Toleo la 2005 inasema:
"Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii".

Masharti ya hiyo ibara yanaendelea kueleza kwamba hoja hiyo haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais:-
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria
ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo vinavyokiuka maadili yanayohusu uandikishwaji
wa vyama vya siasa......
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya
Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi 12
tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge'.

Rais wetu kwa kutochukua hatua kuwapeleka mahakamani mafisadi waliotajwa na Kamati mbalimbali za Bunge na kuidhinishwa na vikao vya Bunge, ni kukiuka Katiba. Hata pale alipoamuru wale wahalifu waliokwapua fedha za EPA wazirejeshe na wasiadhibiwe zaidi, ni ukiukaji wa Katiba.

Kwa hiyo hawa Wabunge 46 na Mawaziri 13 wanaohamasisha wananchi kuwaunga mkono ili hoja ya kumuondoa madarakani Rais wanafanya kitendo cha ushujaa na wa kizalendo. Kumekuwa na vacuum katika uongozi wa nchi hii. Wahalifu kama Bwana "Vijisenti", wanaohusishwa kimataifa na ufisadi wa Rada na ukwapuaji wa dhahabu ya nchi hii katika Kashfa ya Meremeta, wangali Bungeni na wanakula na Rais.Serikali yake hata imeshindwa kuadhibu wezi wa Migodi ya Mkaa wa Mawe wa Kiwira, eti hata kujaribu kuwa compensate majizi kama BM na Yona.

Bunge likiruhusu Serikali iliyolala kama hii kuendelea mpaka Oktoba 2010, tutakuta raslimali zetu zote zimerithishwa kwa wawekezaji wa nje wakishirikiana na mafisadi wa ndani. Sasa ni wakati wa kuwaondoa before it is too late.
Samahani mkuu wangu hapa JK kavunja sheria gani vile!, maanake sijaoni ndani wala sijawahi kuona hoja yoyote Bungeni yenye vielelezo (masharti) kama hivyo hapo juu kuvunjwa..

Kinyume cha hapo maswala yote ya Kiwira, BoT, Ufisadi wa rada na ukwapuaji wa dhahabu hivi kweli vyombo vya sheria kama Takukuru wakiamua kufanya kazi JK anaweza kuwazuia?..si kisha toa ruksa jamani au!
Na hata kama JK anaweza kuwazuia kwa nini hoja kama hii haijawakilishwa bungeni, wananchi tupate kufahamu kwamba JK kazuia sheria isitumike, maanake nachoona huko bungeni hoja zote za ufisadi huzimwa na wabunge wenyewe.
Navyofahamu mimi swala la Mkapa huyu baba analindwa na sheria kama tulivyoambiwa na vyombo vya usalama kabla hata ya Kikwete hajasema kitu.
Kikwete alisema -Tumwache mzee wa watu ajipumzishe!..Kwa maelezo haya bila shaka hili lilikuwa OMBI kwetu sisi wananchi na sii kwamba amezuia kumsimamisha Mkapa..
Kusema kweli tukitaka Mkapa asimame mahakamani sidhani kama JK ana nguvu ya kutuzuia..Na nadhani ndio maana Dr. Slaa husema zipo sheria zinazotuwezesha kumsimamisha Mkapa na mara zote hazungumzii msamaha wa JK... kwa sababu haikuwa msamaha ila ombi.

Jk aliomba tumwache Mkapa apumzike hakusema hakuna kesi against Mkapa.. na sii kazi yake kumfikisha Mkapa mahakamani kwani nijuavyo mimi kisha toa ruksa zoezi la kukamata Mafisadi lifanyike..
Problem kubwa tulokuwa nayo ni vyombo vya usalama ambavyo vimekamatwa na watu ambao ni royal na walikuwa chini ya mzee Apson...Na kama mjuavyo huyo Othman ni cha mtoto kwa Apson, ikisimamisha watu mahakamani kwa Ufisadi, jina la Apson litatokea.. na hapo ndipo kazi mpya itakapoa anza.
 
Kikwete ni Rais safi Tanzania haijawahi kupata na huenda haitampata tena kama huyu atakapomaliza muda wake. Maisha bora kwa kila mtanzania hayatawezekana hivi hivi, hili Kikwete analijua na ili yawezekane mpaka msingi uliopo ubomolewe na ujengwe mwingine mpya. Hili si jambo rahisi ni kama kubomoa Dar es Salaam ya leo na kijenga siku moja.

To restore the trust and harmony it will take sometime, quite sometime; probably more than 30years.[/B] Kwa kuwa ni kweli tunajua ni rahisi kubomoa kama walivyofanya mafisadi BUT kujenga it will and may take quite sometime.

I support you 100%. Misingi ya Ufisadi iliyowekwa na Mwinyi na kisha kuimarishwa na Mkapa inahitaji muda sana kuibomoa kama siyo kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi. Kwani kwa kujua kuwa anayefuata katika urais ni mtu mwadilifu, Mkapa na watu wake walihakikisha kuwa wanajenga mazingira ya nchi kutotawalika kwa kujimilikisha njia kuu za Uchumi. Mathalani:

TANESCO- Kwa kupitia NET Group Solution
waliivuruga walivyotaka na ndio maana Kikwete akaanza na tatizo
la Umeme. Kwa wenye kukumbuka unganisheni dots na mtauona
ukweli. Kana kwamba
hiyo haitoshi, akajimilikisha KIWIRA ili aendelee kumtesa JK.

VIWANDA VYA CEMENT: Baada ya kuviuza kwa wageni huku washkaji wake
wakimiliki hisa kwenye viwanda walihakikisha kuwa
uzalishaji unakuwa under control. Yaliyotokea 2007 kila mtu anayajua.

UUZAJI WA MABENKI: Mkapa kwa kujua kuwa mabenki ni taasisi muhimu
katika uchumi wa nchi, alihakikisha kuwa anayagawa kwa wageni ili
kudhoofisha nguvu za ajaye kwani hatakuwa na pa kushika kwani
mabenki yote yanamilikiwa na wageni. Mwenye kukumbuka kauli ya
Mramba kuwa ni lazima NMB iuzwe, atakubaliana nami hasa
ikizingatiwa uhusiano uliokuwepo kati ya Mramba na Mkapa wa a.k.a
UUME wenza.

UBINAFSISHAJI WA TRC, BANDARI NA ATC[/B]: Huu pia
ulikuwa ni mkakati uliosukwa kwa uhodari na umakini wa hali ya juu
lengo likiwa ni lile lile la kuhakikisha kuwa nchi inakuwa wazi kwa njia
zote za usafiri na usafirishaji kuwa mikononi mwa wageni ili waweze kuingia na kutoka
watakavyo.
kuwa nchi haitawaliki kwani njia muhimu na m

EPA, MEREMETA, MIGODI YA DHAHABU N.K. Hizi zilikuwa ni nyenzo muhimu na za mwisho za kuhakikisha kuwa licha ya kumiliki njia kuu za uchumi lakini wanakuwa na ukwasi mkubwa ambao ambao hauzingatii kanuni za kiuchumi kwa kujilimbikizia mamilioni ya fedha ILI WAWEZE KUWANUNUA WANAOWATAKA kwa wakati wanaotaka bila kuathiri Vitegauchumi vyao.

Haya yote hayakufanyika kwa bahati mbaya bali yalipangwa kwa lengo la kudhoofisha utawala wa JK kwani tangu 1995, walijua kuwa ndiye angefuata na kwa kujua tabia na uzalendo wake, walijenga misingi imara ya haya tunayoyaona leo. WENYE KUMBUKUMBU NA WAKUMBUKE.
 
well mkuu hayo yote uyasemayo ni ya kweli hila nimdhaifu na yeye in terms of kukemea watumishi walio chini yake QUOTE]

KUMBUKA FAGIO LA CHUMA LA MZEE MWINYI NA HARAKATI ZA MREMA vililenga kuondoa wafanyakazi wabovu serikalini lakini vilishindwa na wengine leo hii ndio Makatibu Wakuu wa mawizara.

MABORESHO YA UTUMISHI WA UMMA YA MKAPA pia yalishindwa na hayakuwa na jipya zaidi ya kuweka vigezo vya masters Degree kama Dili tu kushepu mitendaji inayomsumbua JK leo hii.
 
Samahani mkuu wangu hapa JK kavunja sheria gani vile!, maanake sijaoni ndani wala sijawahi kuona hoja yoyote Bungeni yenye vielelezo (masharti) kama hivyo hapo juu kuvunjwa..

Kinyume cha hapo maswala yote ya Kiwira, BoT, Ufisadi wa rada na ukwapuaji wa dhahabu hivi kweli vyombo vya sheria kama Takukuru wakiamua kufanya kazi JK anaweza kuwazuia?..si kisha toa ruksa jamani au!
Na hata kama JK anaweza kuwazuia kwa nini hoja kama hii haijawakilishwa bungeni, wananchi tupate kufahamu kwamba JK kazuia sheria isitumike, maanake nachoona huko bungeni hoja zote za ufisadi huzimwa na wabunge wenyewe.
Navyofahamu mimi swala la Mkapa huyu baba analindwa na sheria kama tulivyoambiwa na vyombo vya usalama kabla hata ya Kikwete hajasema kitu.
Kikwete alisema -Tumwache mzee wa watu ajipumzishe!..Kwa maelezo haya bila shaka hili lilikuwa OMBI kwetu sisi wananchi na sii kwamba amezuia kumsimamisha Mkapa..
Kusema kweli tukitaka Mkapa asimame mahakamani sidhani kama JK ana nguvu ya kutuzuia..Na nadhani ndio maana Dr. Slaa husema zipo sheria zinazotuwezesha kumsimamisha Mkapa na mara zote hazungumzii msamaha wa JK... kwa sababu haikuwa msamaha ila ombi.

Jk aliomba tumwache Mkapa apumzike hakusema hakuna kesi against Mkapa.. na sii kazi yake kumfikisha Mkapa mahakamani kwani nijuavyo mimi kisha toa ruksa zoezi la kukamata Mafisadi lifanyike..
Problem kubwa tulokuwa nayo ni vyombo vya usalama ambavyo vimekamatwa na watu ambao ni royal na walikuwa chini ya mzee Apson...Na kama mjuavyo huyo Othman ni cha mtoto kwa Apson, ikisimamisha watu mahakamani kwa Ufisadi, jina la Apson litatokea.. na hapo ndipo kazi mpya itakapoa anza.

Samahani mkuu wangu hapa JK kavunja sheria gani vile!, maanake sijaoni ndani wala sijawahi kuona hoja yoyote Bungeni yenye vielelezo (masharti) kama hivyo hapo juu kuvunjwa..

Kinyume cha hapo maswala yote ya Kiwira, BoT, Ufisadi wa rada na ukwapuaji wa dhahabu hivi kweli vyombo vya sheria kama Takukuru wakiamua kufanya kazi JK anaweza kuwazuia?..si kisha toa ruksa jamani au!
Na hata kama JK anaweza kuwazuia kwa nini hoja kama hii haijawakilishwa bungeni, wananchi tupate kufahamu kwamba JK kazuia sheria isitumike, maanake nachoona huko bungeni hoja zote za ufisadi huzimwa na wabunge wenyewe.
Navyofahamu mimi swala la Mkapa huyu baba analindwa na sheria kama tulivyoambiwa na vyombo vya usalama kabla hata ya Kikwete hajasema kitu.
Kikwete alisema -Tumwache mzee wa watu ajipumzishe!..Kwa maelezo haya bila shaka hili lilikuwa OMBI kwetu sisi wananchi na sii kwamba amezuia kumsimamisha Mkapa..
Kusema kweli tukitaka Mkapa asimame mahakamani sidhani kama JK ana nguvu ya kutuzuia..Na nadhani ndio maana Dr. Slaa husema zipo sheria zinazotuwezesha kumsimamisha Mkapa na mara zote hazungumzii msamaha wa JK... kwa sababu haikuwa msamaha ila ombi.

Jk aliomba tumwache Mkapa apumzike hakusema hakuna kesi against Mkapa.. na sii kazi yake kumfikisha Mkapa mahakamani kwani nijuavyo mimi kisha toa ruksa zoezi la kukamata Mafisadi lifanyike..
Problem kubwa tulokuwa nayo ni vyombo vya usalama ambavyo vimekamatwa na watu ambao ni royal na walikuwa chini ya mzee Apson...Na kama mjuavyo huyo Othman ni cha mtoto kwa Apson, ikisimamisha watu mahakamani kwa Ufisadi, jina la Apson litatokea.. na hapo ndipo kazi mpya itakapoa anza.

well Mh, mimi nina swali moja unasema tunasheria za kumpeleka mtu mahakama na ambozo hazii itaji raisi wala bunge. ni vyombo vingine vina weza fanya hiyo kazi bila idhini ya yeyote bali power walizonazo. basi kama ni hivyo hawa wabunge wote ni useless na kwanini wanawapigia makelele na wabunge wenzao badala yakupeleka lawama sehemu zenyewe.

kitu chapili umetaja wizi wote hapo juu ebu sema takuruku wamependekeza nini katika hata moja. zaidi ya hilo bunge kuja nakutuambia jamma(MKUU) alikua anadanganywa that is mkuu wa takuruku ni mzembe. uoni hiyo ni hadithi. kwanza nataka uniambie takuruku ni chombo cha polisi au vipi? halafu uje naa hidho sheria ambazo zinaweza kutufanya kumbana na ufisadi bila ya raisi, wala bunge lake kwani clearly tunalalamika kisima kimeisha maji, wakati mto aupo mbali. na vyombo vipi vingine kwani takuruku na bunge sasa tumeshawaona awana shughuli. Na uje vile vile na sheria zinazosema raisi mstaafu hata kama alikua mwizi awachwe. ninachotaka kujua hasa who is responsible for what ili tulalame nao basi.
 
well mkuu hayo yote uyasemayo ni ya kweli hila nimdhaifu na yeye in terms of kukemea watumishi walio chini yake QUOTE]

KUMBUKA FAGIO LA CHUMA LA MZEE MWINYI NA HARAKATI ZA MREMA vililenga kuondoa wafanyakazi wabovu serikalini lakini vilishindwa na wengine leo hii ndio Makatibu Wakuu wa mawizara.

MABORESHO YA UTUMISHI WA UMMA YA MKAPA pia yalishindwa na hayakuwa na jipya zaidi ya kuweka vigezo vya masters Degree kama Dili tu kushepu mitendaji inayomsumbua JK leo hii.

Alipoingia 2005 watu wote walikuwa nyuma yake wakijua tume zote alizoziunda na safari zake alizopita kwenye wizara zote,na warsha zote alizofanya kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi,walijua alikuwa anasafisha njia ya kuifanya nchi itawarike

sasa hivi hata akilialia na mnagani Jakaya hana pa kukwepea ni dhaifu hawezi kuendesha nchi,kwa sababu yeye mwenyewe aliingia kwa kutumia mtandao,alikuwemo serikali iliyopita kwa hiyo maamuzi mengi ya baraza la mawaziri wakati wa mkapa aliyafahamu na alishiriki pia kupindisha baadhi ya sheria ili wao wanufaike kama viongozi

Hebu tujiulize kitu gani kinamfanya sasa hivi mambo ameyaacha holela hakuna utawala wa sheria ,hakuna anayemuogopa wala kumuheshimu kiongozi wa nchi anakataza hiki yue anafanya hiki ,mambo yanazidi kubomoka kuliko hata yalivyokuwa kwa Mkapa.

Miaka minne serikalini hajatafuta mbinu za kutukwamua kila siku vilio tuu kutoka kwa wananchi kutokana na jinsi mali zake zinavyoporwa na wahuni,wazungu,wahindi na waarabu,ametukatisha tamaa sana tulimwamini mno sasa anatuonyesha kwamba ni muhimu kuwe na mabadiliko makubwa kuanzia serikali za mitaa vinginevyo wanataka kutupeleka kusikofaa, kuzagaa kwa vijana bila kazi,njaa,hasira za watu maskini, ukosefu wa mapato sawia ni vitu vinavyoleta chuki,yeye ameshindwa hata kudhibiti mfumuko wa bei,watu wanateseka sana,maradhi,maisha tuu ni magumu mno kwao
Mimi naona apumzike tuu amwachie mwingine ampokee kijiti
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom