Wabunge 10 bora na dhaifu katika kuchangia bajeti kuu ya serikali 2012/2013

Uchambuzi huu umefanywa na tuliokuwa tunasikiliza bunge tangu kuanza kusoma kwa bajeti, waweza kuongeza majina katika kundi lolote ili waheshimiwa hawa wajirekebishe au waendelee kutoa michango bora.

A: Waliotoa michango bora kwa serikali
1. Mh Beatrice Shelukindo - CCM Kilindi
2. Mh. Mbowe - CHADEMA Hai
3. Mh Deo Filikujombe - CCM Ludewa
4. Mh Prof Peter Msola - CCM Kilolo
5. Mh Akonay -CHADEMA - Mbulu
6. Mh Mpina CCM
7. Mh Prof Kahigi -CHADEMA - Bukombe
8. Mh Eng. Makani - CCM Tunduru
9. Mh James Mbatia - NCCR (Kuteuliwa)
10. Mh Nomrod Mkono -CCM (Musoma)

B: Waliotoa michango dhaifu na ovyo
1. Mwigulu Nchemba - CCM
2. Lusende - CCM
3. Tundu Lissu - CHADEMA
4. John John Mnyika - CHADEMA
5. William Ngereja - CCM
6. Felix Mkosamali - NCCR
7. Capt John Komba - CCM
8. Ole Sendeka - CCM

Umetumia criteria gani kumweka lissu grp B?
 
Tupe vigezo ulivyotumia kupata hayo makundi au maksi (scores) za kila mchangiaji kwa makundi yote.
 
Aisee hapo group A embu weka kichwa mh.Msigwa na Dada Esther Bulaya, pia umemnyima haki ya msingi Kaputeeeni Kombaaa gruop B inabidi awe namba moja hapo.
 
cdm walifanya vizuri sana, wabunge wa ccm unafiki mtupu, unakuta mbunge anaponda kwa 100% halafu anaunga hoja 100%.. shelukindo huwa simsikilizi
 
TAARIFA:
Leo nimeisikia sauti ya mohamed dewji alipotakiwa kupiga kura na kujibu "ndiiio" kisha akawa bize kumsaka yule aliyekuwa wa fedha, jina nimemsahau.
 
Mnyika anastahili A 1 kwa kutueleza udhaifu uko wapi bahati mbaya kazuiwa kumaliza kuielezea hoja yake
 
DT125:A S thumbs_down:, hiyo list sawa kulingana na mawazo yako. Ila, kwa Mnyika nawe umeshiriki huku nje kumnyongea mbali km ilivyokuwa, Mjengoni. Mnyika usingemweka kwenye list yyote kwasbabu, hakukkamilisha hoja zake za msingi; pia hakupewa nafasi ya kuthibisha alilokuwa akilifikiria.
 
TAARIFA:
Leo nimeisikia sauti ya mohamed dewji alipotakiwa kupiga kura na kujibu "ndiiio" kisha akawa bize kumsaka yule aliyekuwa wa fedha, jina nimemsahau.

Ulikuwa hujawahi kumsikia sauti yake bila shaka, angalau jana kuna wabunge walikuwa hawajulikani wamejulikana japo sauti zao.
 
Back
Top Bottom