Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Hali hii ya uvaaji wa kimagharibi imeleta hofu kubwa kwa wapenzi wa filamu hizo hususani akina mama kutokana na kuhofia kuharibiwa kwa watoto wao ambao watakuwa wanaiga mambo hayo endapo watakuwa wakiangalia filamu hizo.
Mimi ni shabiki mkubwa wa filamu za kitanzania lakini umefika wakati naogopa kununua kazi hizo kwa kuhofia kuharibu maadili ya familia yangu kutokana na uvaaji wa wasanii wetu hivi sasa wanonekana kuiga sana mambo ya Ulaya kitu ambacho kwetu hakina maana yoyote alisema Sikudhani Said, mkazi wa Changombe jijini Dar es Salaam.
Katika kutafuta ukweli wa jambo hilo Risas Wikiendi Vibes liitembelea duka kubwa la kusambaza filamu Kibongo Tollywood na kukutana muuzaji wa bidhaa hizo aliyejitabulisha kwa jina la Michael Mzee, ambaye alikiri kukumbwa na tatizo la kupungua kwa idadi ya wanunuzi wa muvi za Tanzania kutokana na kile wazazi wanadai ni kulinda maadili ya watoto wao.