Wabongo mlioko majuu hivi huko mnafanya kazi gani?

another thread inayoonyesha kuwa ignorance bado kubwa sana

wabongo walio nje ni sawa na wabongo walio bongo kimaisha. Kuna wenye kazi nzuri na kubwa sana , za kawaIda, na waLio na kazi. Tofauti ni ile quality of life kwa walio nje... Na kwa walio nyumbani ni ile raha ya kuwa nyumbani.

Sasa sisi tulio asia na larin america mbona umetutenga?
 
kitu kimoja ni kuwa wabongo tusaidiane kwenda nje wengi iwezekanavyo
hata kama huko nje kazi ni za vibarua,lakini kama kuna mtu unamjua anataka kwenda nje
ni vizuri kumsaidia......

tazama wafilipino .
wengi wao wanafanya kazi za chini mno nje ya kwao
lakini pesa wanayotuma kwao kwa pamoja ni zaidi ya bajeti yetu(kama sijakosea data)..

tazama wa Nigeria....wapo zaidi ya milioni 20 nje ya Nigeria na
pesa wanayotuma kwao na biashara tu ya makampuni ya ndege kwenda na kurudi Nigeria
ni billions of dollars....

nilishangaa mno kusikia watanzania waliopo marekani ni elfu themanini tu
na waliopo UK ni elfu thelathini tu....
inawezekana data sio sahihi but bado wa TZ wako wachache mno nje.....

tujitahidi kutoka nje wengi iwezekanavyo na huko nje kuanzishwe Organisations
za kusaidiana kwenye mambo kama ada za vyuo na kadhalika....

kuna vitu tunaweza ku organise kama friendly match ya football kati ya taifa stars na USA hivi
na pesa ikaenda kwenye 'kusaidia ada za wabongo wanaosoma USA' na kadhalika...
inawezekana kabisa...
 
Mimi nafanya kazi Supermarket hapa Clarendon Road London and i am paying my bills, sijui habari ya mgao wa umeme, ukame, ubovu wa huduma za hospitali na mengineyo..

zidisha bidii katika kuwahudimia wazungu hapo sokoni mi nipo soko la tandale hongera!!
 
kitu kimoja ni kuwa wabongo tusaidiane kwenda nje wengi iwezekanavyo
hata kama huko nje kazi ni za vibarua,lakini kama kuna mtu unamjua anataka kwenda nje
ni vizuri kumsaidia......

tazama wafilipino .
wengi wao wanafanya kazi za chini mno nje ya kwao
lakini pesa wanayotuma kwao kwa pamoja ni zaidi ya bajeti yetu(kama sijakosea data)..

tazama wa Nigeria....wapo zaidi ya milioni 20 nje ya Nigeria na
pesa wanayotuma kwao na biashara tu ya makampuni ya ndege kwenda na kurudi Nigeria
ni billions of dollars....

nilishangaa mno kusikia watanzania waliopo marekani ni elfu themanini tu
na waliopo UK ni elfu thelathini tu....
inawezekana data sio sahihi but bado wa TZ wako wachache mno nje.....

tujitahidi kutoka nje wengi iwezekanavyo na huko nje kuanzishwe Organisations
za kusaidiana kwenye mambo kama ada za vyuo na kadhalika....

kuna vitu tunaweza ku organise kama friendly match ya football kati ya taifa stars na USA hivi
na pesa ikaenda kwenye 'kusaidia ada za wabongo wanaosoma USA' na kadhalika...
inawezekana kabisa...

NIMEKUTA nchi za far east wana program inayosimamiwa na serikali kuaidia vijana kupata kazi nje ya nchi kwa ajili yamkupunguza makali ya maisha na remittance iongezeke
 
Nina marafiki wengi wapo ulaya na marekani kazi yao ni kunitumia picha walizo piga kwenye majengo mbalimbali, lakini hawaniambii wanafanya kazi gani.Ninavyo wajua kwa kupenda sifa wangekuwa na kazi nzuri wangeniambia haraka .Kama kuna mtu mkweli aseme yeye anafanya nini? huko.
Hayo ni mawazo mgando kama vile wazungu ulaya bado wanafikiri wa afrika bado tunalala
kwenye miti na tunakunya tukiwa juu ya miti
 
Hayo ni mawazo mgando kama vile wazungu ulaya bado wanafikiri wa afrika bado tunalala
kwenye miti na tunakunya tukiwa juu ya miti
kweli aisee, picha zao ni mapori na misitu, wamasai, na vitoto vyenye nzi hadi ndani ya pua
 
The Boss uko very right hasa kwenye issue ya EXPOSURE ambalo ni tatizo la watanzania wengi tena wasomi. LAKINI shida ipo hapa kama hawa ndugu zetu waliopo nje hawatuambii wazi ni nini wanafanya nitatakaje/tamanije niende huko. Aniambie anafanya kazi gani na inamlipa vp ili anihamasishe. Honestly rafiki yangu na ndugu yangu kabisa hawasemi ni nini wanafanya. Am confused ni nini hicho siri hata nduguyo asiseme (wako sita).
 
NIMEKUTA nchi za far east wana program inayosimamiwa na serikali kuaidia vijana kupata kazi nje ya nchi kwa ajili yamkupunguza makali ya maisha na remittance iongezeke

MTM ....
Tena serikali ikiingiza mkono wake hata masuala ya visa na vibali vya kufanya kazi
yanakuwa rahisi mno.....
fikiria Kikwete amshirikishe Andrew Young na wengine kwenye kuhakikisha kila
Mtz aliye marekani ana access na kupata 'education 'akitaka....itakuwa rahisi zaidi
tunaweza kuwa na Tanzanian -American Society maalum kwa kutoa msaada wa Kielimu kwa wabongo waliopo USA
na kama nilivyosema pesa inaweza kupatikana kwa matamasha na kadhalika...
nchi nyingi wanafanya....
 
kitu kimoja ni kuwa wabongo tusaidiane kwenda nje wengi iwezekanavyo
hata kama huko nje kazi ni za vibarua,lakini kama kuna mtu unamjua anataka kwenda nje
ni vizuri kumsaidia......

tazama wafilipino .
wengi wao wanafanya kazi za chini mno nje ya kwao
lakini pesa wanayotuma kwao kwa pamoja ni zaidi ya bajeti yetu(kama sijakosea data)..

tazama wa Nigeria....wapo zaidi ya milioni 20 nje ya Nigeria na
pesa wanayotuma kwao na biashara tu ya makampuni ya ndege kwenda na kurudi Nigeria
ni billions of dollars....

nilishangaa mno kusikia watanzania waliopo marekani ni elfu themanini tu
na waliopo UK ni elfu thelathini tu....
inawezekana data sio sahihi but bado wa TZ wako wachache mno nje.....

tujitahidi kutoka nje wengi iwezekanavyo na huko nje kuanzishwe Organisations
za kusaidiana kwenye mambo kama ada za vyuo na kadhalika....

kuna vitu tunaweza ku organise kama friendly match ya football kati ya taifa stars na USA hivi
na pesa ikaenda kwenye 'kusaidia ada za wabongo wanaosoma USA' na kadhalika...
inawezekana kabisa...
Boss wabongo kwa kifupi hatuna utamaduni huu sisi tuna roho ya kwanini ingekuwa kusaidiana wengi wangekuwa huko kwanza sisi ni wa kwanza kuchomana wenyewe kwa wenyewe halafu unategemea ni wabongo wangapi watasaidia wenzao kwenda nje kuna wafilipino na wathailand kibao wamejaa Casino za Kilimanjaro Hyatt, Le Grand na Sea Cliff mbongo akiwa nje hata ukiwa unafanya jitihada za kwenda huko utasikia anakwambia huku hakufai usije..
 
Hivi wakazi walioko Mwanza wanafanya kazi gani? mfano na mimi huwa wananitumia picha wakiwa mashambani.....
Una maana wale wanapopiga picha wamesima kwenye majumba ina maana kazi zao ni nini, ni walinzi wa majumba hayo au una maanisha nini
 
Wewe mwanzisha hoja nahisi kama uelewa wako una shida, kwani wewe kazi za watu zinakuhusu nini? Una kazi unataka kuwapa? Nina wasiwasi na hata kazi unayofanya wewe. Haya ndugu yangu; kuna wengine wanafanya kazi supermarkets, wengine bar, wengine hotelini, wengine wanauza magazeti, wengine ma-ofisini, wengine wanafundisha kwenye vyuo, wengine wanasoma na kufanya part-time, wengine wamekaa na wanalipwa na serikali za nchi husika, wengine wanlea watoto wa watu, wengine house-boy, wengine house-girl, n.k, n.k.
Sasa nahisi utakuwa umeridhika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom