Wabongo kweli wamechoka!!

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,027
Kwenye barabara kuu ya Ocean Road, asubuhi kumekutwa bonge la bango...''KIKWETE NCHI IMEKUSHINDA JIUZURU''....Haa, jamaa sijui aliweka usiku wa manane!!
 
Kwani ni uongo? Nchi imemshinda kweli Vasco Da Gama ukweli ndio huo akitaka asitake lazima aambiwe na tena hakushinda Uchaguzi bali amewekwa na akina Tendwa kuendeleza Ufisadi na kuwasaidia Wageni waibe rasilimali zetu. Mwizi tu huo Kikwete na Magogoni ameigeuza sehemu ya kupigia dili zake kwa kifupi ameifanya Ikulu kama salamanda kila mtu anaingia kupiga dili nae
 
Watu tumechoka na uchafu unaofanywa na serikali,nampongeza aliyeandika ujumbe barabarani,alibuni namna ujumbe wake utakavyo fika bila kjiumiza.
 
kwa mujibu wa intelijensia yangu..HILO BANGO LIMEANDIKWA NA WATU WA USALAMA WA TAIFA MAANA NDIO WAO WAMEZAGAA MAENEO HAYO KULINDA IKULU"...kama mnabisha shauri yenu..na nikweli kabisaaa "DOGO INCHI IMEMSHINDA AMEAMUA KULA BATA KILA SIKU ANASAFIRI HOVYO"
 
Machungu ya kukosa umeme,watoto wake wanashindwa kujisomea,mara ooh kapeleka mtoto hospitali kaambiwa dawa hakuna huku zingine zikioza MSD,mke alibwagwa na chini na bajaji huku akiwa na uchungu wa uzazi,mara mama yake kule kijijini mahindi yote yamekauka na kijiji chao hawapewi msaada kwa vile walimchagua diwani wa chadema,binamu yake jirani kwao kanyofolewa mkono na fisi akiwahi kuteka maji alfajiri,mtoto wa mjomba wake akababuka ngozi kwa kunywa maji ya sumu nyamongo,mpenzi wake wa zamani kageuka malaya kwenye dangulo moja baada ya kuporwa ardhi na mwekezaji,jirani yake kaziba uchochoro wa kumfikisha nyumbani kwake baada ya kujenga kiosk cha biashara,mdogo wake alikuwa anasoma kati ya chuo kikuu kimoja juzijuzi hapa kafukuzwa na kurudi nyumbani kwake mzigo juu ya mzigo kwa nini asilale macho na kuende kubandika bango wengi tutabandika mabango Kikwete ni Mapepe hasikii na wala hamjali mtu,na sasa hivi ana hasira za kuchukiwa ameamua kumaliza mpaka senti tano ya mwisho hazina kwa kuzurura dunia nzima,
 
Source ni Magic Fm kipindi cha kina Nzowa...!! Na Jamaa kapatia kweli manake ile barabara ya viongozi!!
 
Mm naona bora kaandika tu sababu hasikilizi watu wana matatizo mazito sana na hayatatuliwi hata kidogo mtu ajieleze wapi.
 
Machungu ya kukosa umeme,watoto wake wanashindwa kujisomea,mara ooh kapeleka mtoto hospitali kaambiwa dawa hakuna huku zingine zikioza MSD,mke alibwagwa na chini na bajaji huku akiwa na uchungu wa uzazi,mara mama yake kule kijijini mahindi yote yamekauka na kijiji chao hawapewi msaada kwa vile walimchagua diwani wa chadema,binamu yake jirani kwao kanyofolewa mkono na fisi akiwahi kuteka maji alfajiri,mtoto wa mjomba wake akababuka ngozi kwa kunywa maji ya sumu nyamongo,mpenzi wake wa zamani kageuka malaya kwenye dangulo moja baada ya kuporwa ardhi na mwekezaji,jirani yake kaziba uchochoro wa kumfikisha nyumbani kwake baada ya kujenga kiosk cha biashara,mdogo wake alikuwa anasoma kati ya chuo kikuu kimoja juzijuzi hapa kafukuzwa na kurudi nyumbani kwake mzigo juu ya mzigo kwa nini asilale macho na kuende kubandika bango wengi tutabandika mabango Kikwete ni Mapepe hasikii na wala hamjali mtu,na sasa hivi ana hasira za kuchukiwa ameamua kumaliza mpaka senti tano ya mwisho hazina kwa kuzurura dunia nzima,

Hata akimaliza senti zote hazina akija Kiongozi mzalendo atamweka selo kama ameyafanya hayo kweli. Amuangalie mwenzie Ben Ali wa Tunisia au Hosni Mubarak. Huko si kuchoka bali ni ujasiri na freedom of expression. Kwa tunaofahamu sheria kuna right of peaceful demonstration is a fundamental right of human being. Hilo bango ni moja ya mifano yake, mengine ni maandamano, migomo.
 
Laaaaaaaaaaaaaah hili nalo neno acha kwanza nikapate lunch kwa mama nitilie.
 
kwa mujibu wa intelijensia yangu..HILO BANGO LIMEANDIKWA NA WATU WA USALAMA WA TAIFA MAANA NDIO WAO WAMEZAGAA MAENEO HAYO KULINDA IKULU"...kama mnabisha shauri yenu..na nikweli kabisaaa "DOGO INCHI IMEMSHINDA AMEAMUA KULA BATA KILA SIKU ANASAFIRI HOVYO"

Kuna usalama siku hizi?
Ndio maana raia wanaweza fanya vitu kama hivyo hata mbele ya nyumba ya rais.
 
Hivi yuko nchi gani sasa hivi?, mara ya mwisho nilimsikia eti amefanikisha kuleta mkutano uliokuwa ukifanyika Malaysia kwa miaka zaidi ya 15 hapo 2013, hivi ni kweli tunahitaji mikutano???, nadhani matatizo ya nchini kwake hayampi shida..
 
Back
Top Bottom