Wabeba vitu vizito (mabaunsa) DSM

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
637
Mimi ni mmpenzi sana wa mazoezi ya aerobikale na ya kunyanyua vitu vizito(vyuma) sasa kuna hili swala linanitatiza sana kwa mabaunsa/wanyanyua vitu vizito wengi hapa DSM na sehemu nyingine za TZ wana train eneo moja tu la kifua madhara yake ni kwamba mtu anakuwa na umbile kama la gitaa i.e anajaa juu/kifua sana tena na kibiongo juu kwa vile anapress bench tu bila kupiga na mgongo. Matokeo yake miguu inakuwa membamba kama fito na haina nguvu. na ndio maana wengi wao hawavagai kaptula. Kuna madhara mengine ya kibailojia nimesikia yapo ila sina uhakika nayo labda watalaalamu watusaidie hapa.

Je ni kutokujua au imegeuka kuwa tamaduni?
 
Jibu hili litolewe pia juu ya wacheza karate wanaokata msamba...ina madhara gani. kumekuwa na misemo mingi juu ya madhara ya mazoezi mbalimbali, bila shaka madaktari na watu wenye ufahamu huo humu watatoa maeleza ya kutosha.
 
Kifupi Dar haina trainers kwa hiyo watu hujifanyia chochote tu! wengine GYM huwa ni sehemu ya kwenda kupigia storiez na kutafuta milupo
 
Kweli mkuu wengi wao walikuwa wafagiaji/wafanya usafi wa gym then wakikaa miaka 2 wanapanda cheo wanakuwa hata chief instructor. Na kweli hilo swala la milupo nalo linashika kasi hasa pale COLLESSEUM HOTEL O'bay kumeharibika.

Hata misosi huwa hawatilii maanani jamaa anapiga chuma anashindia ugali bamia kwa mama Ntilie.

ha ha ha ha ha, wengine wanapiga hata mlo 1 ukata mzee hili ni janga la kitaifa umasikini unepiga kila kona.
 
Kiafya sijui madhara yake..Ila hizo shepu za namba saba mmh!..mtu juu hilo kachana,chini kanyauka!Hivi wanakuwa na nguvu kweli za kupigana hao baunsaz?
 
hahaha, nguvu za kupigana wanakuwa nazo, wakikukamata mwilini wakakuskwizi unaweza pasuka, pia wakikupiga ngumi moja wakafanikiwa kukupatia inakuwa nzito sana. tatizo ni kwamba, nguvu za kupigana wanazo, ila ufundi wa kupigana hawana,....ndo maana wanaweza kupigwa na mchina mwembamba kama unyasi...kupigana si jambo zuri, ila incase umevamiwa just for self defense, ukawa ulishakuwa trained for self defense, hawana lolote.
 
ha ha ha ha, Unautani na huyu eeh?

k0191894.jpg

x16642849.jpg
 
hawana lolote hao. mwili mkubwaa akili kidogo, na wakifika miaka kama hamsini hivi ndo wanaanza ugonjwa wa kutetemeka kama mohamed ali, misuli yao inakuwa imelazimishwa kupanuka artificially. kwa kung fu zangu, sihesabugi kama kuna kitu hapo pamoja na kwamba huwa sipigani, ila akinikuta usiku labda anataka kunipora kitu, ataendak usimulia nda rafiki zake wote...
 
Mimi ni mmpenzi sana wa mazoezi ya aerobikale na ya kunyanyua vitu vizito(vyuma) sasa kuna hili swala linanitatiza sana kwa mabaunsa/wanyanyua vitu vizito wengi hapa DSM na sehemu nyingine za TZ wana train eneo moja tu la kifua madhara yake ni kwamba mtu anakuwa na umbile kama la gitaa i.e anajaa juu/kifua sana tena na kibiongo juu kwa vile anapress bench tu bila kupiga na mgongo. Matokeo yake miguu inakuwa membamba kama fito na haina nguvu. na ndio maana wengi wao hawavagai kaptula. Kuna madhara mengine ya kibailojia nimesikia yapo ila sina uhakika nayo labda watalaalamu watusaidie hapa.

Je ni kutokujua au imegeuka kuwa tamaduni?

Kwanza, neno baunsa ambalo linatokana na neno "bouncer" umelitumia visivyo. Ingia kwenye kamusi usome maana yake.

Pili, hayo unayosema wewe, hasa kwa Tanzania yatakuwa maumbile zaidi kuliko transformation iliyosababishwa na kunyanyua vitu vizito kwenye sehemu ya juu ya mwili (upper body). Kwenye genetic body types kuna endomorph, mesomorph, na ectomorph (kama sijakosea). Naweza kwenda kwa undani zaidi kuhusu hili kama utapenda lakini ninachotaka kusema ni mwamba kuna watu walio top heavy na nadhani hawa ndio hasa wewe unawaongelea.

Na hakuna madhara yoyote ya kiafya yatokanayo na kunyanyua vitu vizito. Hiyo ni dhana potofu tu. Nitarudi baadae kwa undani zaidi.

NB: Mimi ni certified personal trainer na ninayajua haya mambo nje ndani. Kuna a lot myths out there.
 
Kwanza, neno baunsa amablo linatokana na neno "bouncer" umelitumia visivyo. Ingia kwenye kamusi usome maana yake.

Pili, hayo unayosema wewe, hasa kwa Tanzania yatakuwa maumbile zaidi kuliko transformation iliyosababishwa na kunyanyua vitu vizito kwenye sehemu ya juu ya mwili (upper body). Kwenye genetic body types kuna endomorph, mesomorph, na ectomorph (kama sijakosea). Naweza kwenda kwa undani zaidi kuhusu hili kama utapenda lakini ninachotaka kusema ni mwamba kuna watu walio top heavy na nadhani hawa ndio hasa wewe unawaongelea.

Na hakuna madhara yoyote ya kiafya yatokanayo na kunyanyua vitu vizito. Hiyo ni dhana potofu tu. Nitarudi baadae kwa undani zaidi.

NB: Mimi ni certified personal trainer na ninayajua haya mambo nje ndani. Kuna a lot myths out there.

bouncer [ˈbaʊnsə]
n 1. Slang a man employed at a club, pub, disco, etc., to throw out drunks or troublemakers and stop those considered undesirable from entering
2. (Economics, Accounting & Finance / Banking & Finance) Slang a dishonoured cheque
3. (Team Sports / Cricket) Cricket another word for bumper1
4. a person or thing that bounces
 
Na hakuna madhara yoyote ya kiafya yatokanayo na kunyanyua vitu vizito. Hiyo ni dhana potofu tu. Nitarudi baadae kwa undani zaidi.

Mkuu Ngabu kuna Dakatari aliniambia kwamba kwa Wanyanyua Vitu vizito wana hatari ya Kutokwa na Nyama ya Anus ( Mku**) kwa maana wanaponyanyua vyuma vizito hewa inatokea makalioni na kusababisha Nyama ( Nadhani sijui Utumbo mkubwa) kutokea kunako tigo. Hii Dhana wewe unaionaje maana nilianza mazoezi ya Kunyanyua Vitu vizito Daktari akanipa hilo angalizo nikaamua kuacha
 
Heheheheheee...ningependa kujua elimu ya huyo daktari na alipoipatia
 
bouncer [ˈbaʊnsə]
n 1. Slang a man employed at a club, pub, disco, etc., to throw out drunks or troublemakers and stop those considered undesirable from entering
2. (Economics, Accounting & Finance / Banking & Finance) Slang a dishonoured cheque
3. (Team Sports / Cricket) Cricket another word for bumper1
4. a person or thing that bounces

Ewaaaa....unaona sasa babu. Watu wengi sana hulitumia hilo neno kimakosa. Mtu anyanyuaye vyuma vizito kwa mazoezi siyo baunsa "bouncer". Tukianza na hilo kwanza nadhani tunaweza kupata uelewa mzuri zaidi wa weight training.
 
Kwa hiyo Baunsa siyo Lazima ajazie au
 
Mkuu Ngabu kuna Dakatari aliniambia kwamba kwa Wanyanyua Vitu vizito wana hatari ya Kutokwa na Nyama ya Anus ( Mku**) kwa maana wanaponyanyua vyuma vizito hewa inatokea makalioni na kusababisha Nyama ( Nadhani sijui Utumbo mkubwa) kutokea kunako tigo. Hii Dhana wewe unaionaje maana nilianza mazoezi ya Kunyanyua Vitu vizito Daktari akanipa hilo angalizo nikaamua kuacha

:angry:Mh! ni daktari wa kienyeji e.g dr. Manyuki au dactari wa kisasa/hospitalini?
 
Back
Top Bottom