Wabara wanapoitwa wageni ligi kuu Zenji

LENIN'S

Member
Mar 13, 2011
13
1
NIPOKEENI, MGENI LICHA SINA KAMBA!

(Juzi) majira ya saa 1:30 nimekaa kando ya redio yangu, nasikiliza Kipindi cha spoti cha Radio One Stereo, taarifa ya kispoti inatoka pemba kwamba, timu ya Miembeni inapania kuishtaki Mundu ZFA kwa kile inachokiamini kuwa imechezesha wageni wengi kuliko utaratibu.

Kwa kweli nilishawishika kujua uwezo wa kifedha iliyonayo Mundu hata kuweza kuwaleta wageni ilhali udhamini kwa vilabu vya zenji ni tatizo.

Kumbe hawakuwa wageni kitoka mipaka ya Jamhuri ya Muungano (ya,wa) Tanzania. Kwamba wabara walikuwa wengi kuliko Wazanzibari.

Nikajiluliza, hawa si watanzania? kwa nini waitwe wageni? kwa nini wasiitwe wabara tu ionekane kosa ni kiuvuka bahari?

Je tutaendelea hivi hadi lini, kwa kubaguana kiasi hiki?

MUUNGANO HUU WAWEZEKANA MAUNGO YAKE AMA SI SAHIHI AU YAMECHAKAA.
 
Washazoea hao chao cha kwao peke yao cha kwetu chao pia
 
ofcoz ni wageni!.. unless kama wanakitambulisho cha ukazi!.. kile ambacho wanatumia kupigia kura!..
 
Back
Top Bottom