Waathirika wa mabomu ya gongo la mboto, sasa kuchakavya na mvua na magonjwa

lifeofmshaba

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
867
219
MVUA zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam zimeathiri makazi ya muda ya waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto na kuwafanya waishi kwa mashaka na hofu ya kupata magonjwa ya milipuko na vichomi.

Aidha, waathirika hao wanaodai kuishiwa vyakula na maji, wameilalamikia Serikali kwa kutowajulisha kinachoendelea kuhusu nyumba ilizoahidi kuwajengea ikiwa ni pamoja na kutotekeleza ahadi yake ya kuwapelekea magodoro ya ziada.


waathirika hao wamesema tumeanza kuishi kwa mashaka na hofu ya kupata magonjwa ya milipuko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Viongozi wetu wa serikali hatuwaoni sio wa ngazi ya kata wala mkoa,


, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam (RAS), Rose Mbando amesema kuwa gazeti hili ndilo lilikuwa likimtaarifu kuhusu kuwepo kwa hali mbaya ya mazingira kwa waathirika hao ambalo hata hivyo ameahidi kuhakikisha linashughulikiwa mara moja.


Alisema, anakiri kuwepo kwa udhaifu katika suala la mawasiliano kati ya viongozi na waathirika hao kwa sababu walipaswa kujua kinachoendelea kuhusu ujenzi wa nyumba walizoahidiwa ambao hata hivyo uko katika hatua ya kufyatua matofali.


“
Nashukuru kwa kutujulisha kuwa waathirika wetu hawana mahitaji ya vyakula, maji na magodoro, ni mawasiliano mabovu ndio yamesababisha tusiwapelekee kwa sababu hatujui kama wanahitaji, tuna vyakula vingi na magodoro ya kutosha stoo kwa ajili yao kwa hiyo tutakwenda kesho (Jumanne kuwaona ili tujue idadi ya wahitaji na utaratibu wa kuufuata kuwagawia…

Lakini tuna tatizo la uhaba wa maji, hatuna hata chupa moja ya maji hadi sasa na najua watakuwa wanayahitaji pia. Vile vile tunaisubiri serikali iseme nini kifuate kwa sababu tumepata ripoti ya tathmini kutoka kwa watendaji kata leo (jana)”.


SOURCE
HabariLeo | Mvua yawachakaza waathirika wa mabomu G/Mboto
 
Back
Top Bottom