Waarabu Wenye Asili ya Kiafrika?

Tippu Tip alikuwa na damu ya kiafrika lakini alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa watumwa.

Kwa kweli historia potofu imekuwa silaha madhubuti ya kuenea kwa ukristo tuseme hapa Tanzania tulipo.Tip Tip alikuwa mfanyabiashara wa kawaida tu.na alianza na umachinga akiwa na miaka 12.Alikuwa akiwalipa wafanyakazi wake waliokuwa wakimbebea mizigo yake kwa staili ya siku hizo kulingana na kilomita walizombebea.
Wamishionari walipokuja na kumkuta tajiri aliyeendelea na uislamu wake wakamfanyia njama na kumzushia mambo mengi na michoro kama hiyo ya watumwa waliofungwa minyororo.Kabla kufa kwake aliandika historia yake kwa mkono wake na kulalamikia sana akina Jameson waliomzushia maovu pamoja na misaada yote aliyowapa.Ukitaka mjadala zaidi kuhusu hili tutaendelea.....
Huyu Buchanan simjui kwa sura na sura aliyotumia pale si yake.Naweza kusema hivyo kwa kuangalia maelezo na mada zake.Yeye lazima ni kijana mdogo ambaye hata miaka kama yangu hajafika.Kwa hivi chuki zisizokuwa na mashiko anazopewa huenda kanisani kwake hajakuwa na muda wa kuzizingatia na kuzifanyia udadisi angalia kidogo. ,
unataka kutuambia unyanyasaji walioufanya hao waarabu ni porojo?
huna jipya hilo huwezi kulisafisha, na halihitaji uchunguzi sana maana liko wazi, nenda oman ukaoneshwe majengo yaliyojengwa na waafrika kwa adhabu kali
 
Unfortunately, sentensi yako ya kwanza inakushitaki. Umeshajiweka categorically katika kundi la waarabu dhidi ya waafrika waliokuwa wakikunyanyasa. Kama toka mtoto ulikuwa unajihesabu ni muarabu kwa nini basi watoto wenzio wasikuite hivyo? Si dhambi kusifia damu uliokuwa nayo lakini si kwa kuidharau nyingine. Unapojiita mwarabu wakati wote wanajua mmoja wa mzazi wako ni mwafrika ni lazima watakusemea ovyo maana watoto ni wakatili.

Hakuna mwarabu ambaye aliishi pwani ya Tanzania au kwenye visiwa vyake wakati utumwa ni halali ambaye hakuhusika na utumwa kwa njia moja au nyingine. Kuwepo kwa watumwa ndiko kulikoboresha maisha yake. Kuoa mwafrika hakkuna maana kuwa hakuhusika na utumwa! Tippu Tip alikuwa na damu ya kiafrika lakini alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa watumwa.

Na Ngoshwe, ni kuwa disingenious kusema kuwa waarabu waliwauzia wazungu watumwa lakini hawakuwa na watumwa kwao. Saudi Arabia ilipiga marufuku utumwa mwaka 1962, Yemen na Oman 1970 na Mauritania 1981!

Amandla........

Kwa kweli historia potofu imekuwa silaha madhubuti ya kuenea kwa ukristo tuseme hapa Tanzania tulipo.Tip Tip alikuwa mfanyabiashara wa kawaida tu.na alianza na umachinga akiwa na miaka 12.Alikuwa akiwalipa wafanyakazi wake waliokuwa wakimbebea mizigo yake kwa staili ya siku hizo kulingana na kilomita walizombebea.
Wamishionari walipokuja na kumkuta tajiri aliyeendelea na uislamu wake wakamfanyia njama na kumzushia mambo mengi na michoro kama hiyo ya watumwa waliofungwa minyororo.Kabla kufa kwake aliandika historia yake kwa mkono wake na kulalamikia sana akina Jameson waliomzushia maovu pamoja na misaada yote aliyowapa.Ukitaka mjadala zaidi kuhusu hili tutaendelea.....
Huyu Buchanan simjui kwa sura na sura aliyotumia pale si yake.Naweza kusema hivyo kwa kuangalia maelezo na mada zake.Yeye lazima ni kijana mdogo ambaye hata miaka kama yangu hajafika.Kwa hivi chuki zisizokuwa na mashiko anazopewa huenda kanisani kwake hajakuwa na muda wa kuzizingatia na kuzifanyia udadisi angalau kidogo. ,
 
.........Tippu Tip alikuwa na damu ya kiafrika lakini alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa watumwa............

Kwa kweli historia potofu imekuwa silaha madhubuti ya kuenea kwa ukristo tuseme hapa Tanzania tulipo.Tip Tip alikuwa mfanyabiashara wa kawaida tu.na alianza na umachinga akiwa na miaka 12.Alikuwa akiwalipa wafanyakazi wake waliokuwa wakimbebea mizigo yake kwa staili ya siku hizo kulingana na kilomita walizombebea.
Wamishionari walipokuja na kumkuta tajiri aliyeendelea na uislamu wake wakamfanyia njama na kumzushia mambo mengi na michoro kama hiyo ya watumwa waliofungwa minyororo.Kabla kufa kwake aliandika historia yake kwa mkono wake na kulalamikia sana akina Jameson waliomzushia maovu pamoja na misaada yote aliyowapa.Ukitaka mjadala zaidi kuhusu hili tutaendelea.....
Huyu Buchanan simjui kwa sura na sura aliyotumia pale si yake.Naweza kusema hivyo kwa kuangalia maelezo na mada zake.Yeye lazima ni kijana mdogo ambaye hata miaka kama yangu hajafika.Kwa hivi chuki zisizokuwa na mashiko anazopewa huenda kanisani kwake hajakuwa na muda wa kuzizingatia na kuzifanyia udadisi angalau kidogo. ,

Sina chuki ndugu Masoud, nilileta mada kwa nia njema! Maelezo yako hapo juu ndiyo yaliyojaa chuki, tumia busara zaidi kuliko kuandika ulivyoandika hapo juu! Ukishindwa mada hii sio lazima uchangie!
 
Nia njema katika hilo haipo zaidi ya kuwatukana waarabu ambapo nia ya ndani ni kuutukana uislamu.Wewe nakushauri jibu hoja ikiwa unazo kuhusiana na Tip Tip ambaye alikuwa mwarabu mwenye asili ya kiafrika na ambaye ni kiini cha mjadala uliouleta jamvini.
Na wewe ikiwa huna zaidi ya kuudhalilisha uislamu,kwani ni lazima uandike?.Si ukae kimya tu mpaka upate kitu cha maana ulicho na ujuzi nacho?.
 
kipofu kumwongoza kipofu mwenziye lazima watapotea tu, ubaguzi maana uko wapi hapo, udini uko wapi hapo, nyie hebu badirikeni mwende na wakati, siyo tu kwa sababu waliwaletea upagani wenu katika mfumo wa kitabu,
basi muwakumbatie tu hata na ushenzi wao, hapo hamtetei tabia zao bali mmevaa kofia za uislamu
hebu vueni kwanza, then tuwatazame hawa waarabu na faida za kwa jamii nzima

huwezi kuwatetea hawa ni washenzi tu, sitoshindwa kusema hivyo kwa kuonekana mbaguzi ama mdini

Hizi ni comments zenye hisia ile ile anayopinga masoud, Upagani ni nini? na ni kitabu gani unacho kizungumzia? Sina hakika unaijua historia ya utumwa duniani kwa kiwango gani? Je waraabu walikuwa wanawapeleka wapi watumwa? kufanya nini? Kwa taarifa yako hao waarabu walikuwa ni agent wa hao wazungu ambao ni washenzi zaidi kuliko unavyo fahamu wewe.
 
Waarabu ni watu waliofanya biashara ya utumwa kwa muda mrefu sana na victim wakubwa wa biashara hiyo haramu ni Waafrika! Wazungu pia walifanya biashara hiyo kwa muda mrefu. Kwa upande wa Wazungu wao walizaa na Waafrika ambao walichukuliwa utumwani na ndio maana kuna Wamarekani wenye asili ya Kiafrika. Hata hivyo sijawahi kusikia Waarabu wenye asili ya Kiafrika! Tuseme kwamba waarabu hawakuzaa na Waafrika au kilitokea nini hasa?

Hivi asili ya wamarekani wenye asili ya kiafrika kumetokana na wazungu kuzaa na waafrika? Je kina Martin Luther King walikuwa wametokana na kizazi cha kuchanganya damu na wazungu? au ni kizazi cha watumwa walio achiwa huru na kwa bahati mbaya au nzuru hawakurudishwa africa wote, waliorudishwa walipekwa Liberia. Kama si mvivu wa kusoma jaribu ku-search katika internet utapata ufahamu mzuri.
 
Nia njema katika hilo haipo zaidi ya kuwatukana waarabu ambapo nia ya ndani ni kuutukana uislamu.Wewe nakushauri jibu hoja ikiwa unazo kuhusiana na Tip Tip ambaye alikuwa mwarabu mwenye asili ya kiafrika na ambaye ni kiini cha mjadala uliouleta jamvini.
Na wewe ikiwa huna zaidi ya kuudhalilisha uislamu,kwani ni lazima uandike?.Si ukae kimya tu mpaka upate kitu cha maana ulicho na ujuzi nacho?.
Uarabu ndio Uislamu?
 
Nia njema katika hilo haipo zaidi ya kuwatukana waarabu ambapo nia ya ndani ni kuutukana uislamu.Wewe nakushauri jibu hoja ikiwa unazo kuhusiana na Tip Tip ambaye alikuwa mwarabu mwenye asili ya kiafrika na ambaye ni kiini cha mjadala uliouleta jamvini.
Na wewe ikiwa huna zaidi ya kuudhalilisha uislamu,kwani ni lazima uandike?.Si ukae kimya tu mpaka upate kitu cha maana ulicho na ujuzi nacho?.
Uarabu ndio Uislamu?
 
Hizi ni comments zenye hisia ile ile anayopinga masoud, Upagani ni nini? na ni kitabu gani unacho kizungumzia? Sina hakika unaijua historia ya utumwa duniani kwa kiwango gani? Je waraabu walikuwa wanawapeleka wapi watumwa? kufanya nini? Kwa taarifa yako hao waarabu walikuwa ni agent wa hao wazungu ambao ni washenzi zaidi kuliko unavyo fahamu wewe.

haya ni maelezo ya kitabu cha historia ya kuiandika wewe, will you show some evidences to help
others to understand you? au una bwabwaja tu?
 
TIPPU TIP AJIELEZA

╞ Nalipopata miaka thenashara ,nalishika safari za karibu.Hafanya biashara ya sandarusi pamoja na ndugu yangu Muhammed bin Masud el Wardi na mjomba wangu Bushiri bin Habib wa Abdallah bin Habib el Wardijan.Nachukua bidhaa kidogo,maana kijana.Nao wao ndugu yangu na wajomba wangu wakichukuwa bidhaa nyingi kidogo.Hafanza biashara ya sandarusi mwaka mmoja╡ (12)

TIPPU TIP AWALIPA MSHAHARA WAFANYAKAZI

1.╞Hapagaza watu saba mia nefer,nikatoka Unguja na mali,tukaenda Mbwa Maji.Tukafunga mizigo.Ilipokuwa tayari,wakaja jemia wapagazi.Tukakaa siku saba,tukaondoka,tukafika Mkamba.Na wakati huu vyakula muhindi,watu wanakula.Tulipofika Mkamba tukanunua mpunga mwingi,kasidi kuwapa chakula chingi.Njia ya Lufiyi hamna vyakula ila ufike Lufiyi.Na wapagazi walikuwa wengi.Tukawapa kula mtu chakula cha siku sita min gher chakula cha pale.╡

2.╞Na wakati huu yalikuwa njaa mrima.Nasi hupita njia ya Urori na wapagazi wa Kinyamwezi hawakubali kupita Urori,mbali na kwao.Na wazaramo hawapagazi.Lakini walipoona njaa taabu,wakaazimu kupagaza,mtu reale kumi makta,kwenda na kurudi.Wakataka takdimu robo,wengine thuluthi.Wakataka mtama na chakula.╡(18)

WALIPWA NA KURUDI MAKWAO

3.╞Hawaacha jemaa Mambwe,haenda Ruemba……Waruemba wakatoa watu wakachukuwa pembe Ruemba hata Mambwe.Na watu wa Mambwe wakachukuwa pembe hata Nyamwanga,na watu wa Nyamangwa wakachukuwa hata Nyika,na watu wa Nyika wakachukuwa hata Usafwa na watu wa Usafwa wakachukuwa hata auwali ya Urori.Tulipofika Urori bassi,tukachukuwa wenyewe kidogo kidogo…..
Tulipofika Urori,wapagazi si maujudi,kuja pwani Warori.Nikaazim kwenda Tabora kuleta wapagazi Wanyamwezi.Hawaacha jemaa na pembe….╡ (28-30)

Hicho ni Kiswahili cha kale. Kuna baadhi ya majina ya miji hayasikiki sasa,na baadhi ya maneno baadhi yetu yawezekana tusiyaelewe.Baadhi ya miji ni miji ya Kongo.
Kwa kifupi Tippu Tip alikuwa akifanya biashara halali ya vitu vya matumizi ya kila aina kama vile sandarusi na pembe.Alikuwa akiwalipa wafanyakazi wake ama chakula au pesa.
Stanley aliwahi kufanya urafiki mkubwa na Tippu Tip kwa nia ya kumdhuru baadae ili aipige vita dini yake,na wala hakuwa na nia ya kupinga biashara ya Utumwa.Stanley anaikumbuka siku Tippu Tip alipokuwa mkali pale wafanyakazi wake walipotaka kumwibia na kumuharibia biashara zake huku akiwa tayari keshawalipa "advance".Siku hiyo anasema akili ilimruka hatimaye akaamua kupambana nao kwa kutengeneza minyororo na kuwafunga ili wammalizie kazi yake kumfikishia mizigo yake pwani.Tukio hili ndilo walilolitumia wamishionari kumpakazia Tippu Tip mpaka leo mashuleni.
Katika maandishi yake Tippu Tip anasifiwa kwa kueleza ukweli wote.Angekuwa alikuwa akiuza watu angesema.
 
Hakikisha huleti upuuzi wowote ule kwa sababu unaangaliwa hapa.
 
Kwa kweli historia potofu imekuwa silaha madhubuti ya kuenea kwa ukristo tuseme hapa Tanzania tulipo.Tip Tip alikuwa mfanyabiashara wa kawaida tu.na alianza na umachinga akiwa na miaka 12.Alikuwa akiwalipa wafanyakazi wake waliokuwa wakimbebea mizigo yake kwa staili ya siku hizo kulingana na kilomita walizombebea.
Wamishionari walipokuja na kumkuta tajiri aliyeendelea na uislamu wake wakamfanyia njama na kumzushia mambo mengi na michoro kama hiyo ya watumwa waliofungwa minyororo.Kabla kufa kwake aliandika historia yake kwa mkono wake na kulalamikia sana akina Jameson waliomzushia maovu pamoja na misaada yote aliyowapa.Ukitaka mjadala zaidi kuhusu hili tutaendelea.....
Huyu Buchanan simjui kwa sura na sura aliyotumia pale si yake.Naweza kusema hivyo kwa kuangalia maelezo na mada zake.Yeye lazima ni kijana mdogo ambaye hata miaka kama yangu hajafika.Kwa hivi chuki zisizokuwa na mashiko anazopewa huenda kanisani kwake hajakuwa na muda wa kuzizingatia na kuzifanyia udadisi angalau kidogo. ,

Hivi unaamini kuwa habari za Tippu Tip alliandika huyo Jameson peke yake? Hicho kitabu alichoandika mwenyewe kinaitwaje?Unaposema alikuwa mfanyabiashara wa kawaida ulikuwa na maana gani? Huyo unayemuita mmachinga alipataje utajiri wake katika nchi ambamo biashara yake kuu ilikuwa utumwa? Unataka kutuambia alikuwa akifanya biashara gani? Hiyo mizigo ilikuwa mizigo ya nini? Na hao waliombebea aliwatowa wapi na baada ya safari walienda wapi? Ukiangalia umbali alikokuwa akitoa hiyo biashara yake basi hao wafanyakazi wote nao wangakuwa matajiri? Au mnataka kurudia tena uongo wenu kuwa hata biashara ya utumwa haikuweko Zanzibar?

Usitake kuandika historia upya. Hamuwatendei haki wale ambao waliumia kutokana na uovu wa utumwa. Si suala la uislamu au ukristu. Yeyote aliyehusika na biashara hii inabidi alaaniwe, awe mzungu, muarabu au mwafrika. Lakini laana hiyo haihusu vizazi vilivyomfuata.

Amandla........
 
TIPPU TIP AJIELEZA

╞ Nalipopata miaka thenashara ,nalishika safari za karibu.Hafanya biashara ya sandarusi pamoja na ndugu yangu Muhammed bin Masud el Wardi na mjomba wangu Bushiri bin Habib wa Abdallah bin Habib el Wardijan.Nachukua bidhaa kidogo,maana kijana.Nao wao ndugu yangu na wajomba wangu wakichukuwa bidhaa nyingi kidogo.Hafanza biashara ya sandarusi mwaka mmoja╡ (12)

TIPPU TIP AWALIPA MSHAHARA WAFANYAKAZI

1.╞Hapagaza watu saba mia nefer,nikatoka Unguja na mali,tukaenda Mbwa Maji.Tukafunga mizigo.Ilipokuwa tayari,wakaja jemia wapagazi.Tukakaa siku saba,tukaondoka,tukafika Mkamba.Na wakati huu vyakula muhindi,watu wanakula.Tulipofika Mkamba tukanunua mpunga mwingi,kasidi kuwapa chakula chingi.Njia ya Lufiyi hamna vyakula ila ufike Lufiyi.Na wapagazi walikuwa wengi.Tukawapa kula mtu chakula cha siku sita min gher chakula cha pale.╡

2.╞Na wakati huu yalikuwa njaa mrima.Nasi hupita njia ya Urori na wapagazi wa Kinyamwezi hawakubali kupita Urori,mbali na kwao.Na wazaramo hawapagazi.Lakini walipoona njaa taabu,wakaazimu kupagaza,mtu reale kumi makta,kwenda na kurudi.Wakataka takdimu robo,wengine thuluthi.Wakataka mtama na chakula.╡(18)

WALIPWA NA KURUDI MAKWAO

3.╞Hawaacha jemaa Mambwe,haenda Ruemba……Waruemba wakatoa watu wakachukuwa pembe Ruemba hata Mambwe.Na watu wa Mambwe wakachukuwa pembe hata Nyamwanga,na watu wa Nyamangwa wakachukuwa hata Nyika,na watu wa Nyika wakachukuwa hata Usafwa na watu wa Usafwa wakachukuwa hata auwali ya Urori.Tulipofika Urori bassi,tukachukuwa wenyewe kidogo kidogo…..
Tulipofika Urori,wapagazi si maujudi,kuja pwani Warori.Nikaazim kwenda Tabora kuleta wapagazi Wanyamwezi.Hawaacha jemaa na pembe….╡ (28-30)

Hicho ni Kiswahili cha kale. Kuna baadhi ya majina ya miji hayasikiki sasa,na baadhi ya maneno baadhi yetu yawezekana tusiyaelewe.Baadhi ya miji ni miji ya Kongo.
Kwa kifupi Tippu Tip alikuwa akifanya biashara halali ya vitu vya matumizi ya kila aina kama vile sandarusi na pembe.Alikuwa akiwalipa wafanyakazi wake ama chakula au pesa.
Stanley aliwahi kufanya urafiki mkubwa na Tippu Tip kwa nia ya kumdhuru baadae ili aipige vita dini yake,na wala hakuwa na nia ya kupinga biashara ya Utumwa.Stanley anaikumbuka siku Tippu Tip alipokuwa mkali pale wafanyakazi wake walipotaka kumwibia na kumuharibia biashara zake huku akiwa tayari keshawalipa "advance".Siku hiyo anasema akili ilimruka hatimaye akaamua kupambana nao kwa kutengeneza minyororo na kuwafunga ili wammalizie kazi yake kumfikishia mizigo yake pwani.Tukio hili ndilo walilolitumia wamishionari kumpakazia Tippu Tip mpaka leo mashuleni.
Katika maandishi yake Tippu Tip anasifiwa kwa kueleza ukweli wote.Angekuwa alikuwa akiuza watu angesema.

Mbona hakukana kuwa alikuwa akifanya biashara ya utumwa? Mbona umetoa sehemu tu bila ku-cite jina la kitabu ulikotoa quotation hiyo? Unataka kutuambia jaribio la kumuibia lilitokea mara moja? Huyu alikuwa ni mfanyabiashara na biashara iliyokuwa ikilipa kuliko zote ilikuwa ni utumwa. Atakuwa ni mtu wa ajabu sana kama hakufanya biashara hiyo iliyokuwa halali wakati ule!

Stanley kwa taarifa yako hakupinga utumwa. Yeye alikuja kumtafuta Livingstone. Livingstone ndiye aliyekuwa akipinga utumwa ingawa wazungu wengi walikuwa bado wanaukubali. Msitake kuingiza suala la ukristu na uislamu humu ndani. Uarabu si uislamu kama vile uzungu si ukristu. Hapa wanalaumiwa waarabu waliojihusisha na biashara hiyo. Hakuna anayekana kuwa wazungu na waafrika nao hawakujihusisha na biashara hiyo. Wote hao wanastahili kulaumiwa.

Amandla...........
 
Swali la msingi ni " je kulikuwa na biashara ya utumwa katika eneo hili ambalo leo tunaliita TANZANIA? Na ni nani walihusika na biashara hiyo?"

Amandla.........
 
Waarabu ni watu waliofanya biashara ya utumwa kwa muda mrefu sana na victim wakubwa wa biashara hiyo haramu ni Waafrika! Wazungu pia walifanya biashara hiyo kwa muda mrefu. Kwa upande wa Wazungu wao walizaa na Waafrika ambao walichukuliwa utumwani na ndio maana kuna Wamarekani wenye asili ya Kiafrika. Hata hivyo sijawahi kusikia Waarabu wenye asili ya Kiafrika! Tuseme kwamba waarabu hawakuzaa na Waafrika au kilitokea nini hasa?
Kwani asili ya sehemu fulani inatokana na kuwa na mzazi mmoja wa asili ya sehemu ile au kuzaliwa kwenye sehemu ile hata kama wazazi wako si wa sehemu ile? Mfano, kuwa Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika ni kuwa wazazi wako ni Kama wa Obama, au hata kama baba na mama yake Obama wangeamua kuishi US na kumzaa Obama huko US. Watu ambao ni matokeo ya 'race' mbili tofauti wana asili mbili kwa sababu ki-biolojia wazazi uchanga 'genes' nusu kwa nusu kupta mtoto kamili. Kijamii ndio shida inakuja kwani 'race' moja ujiona superior kuliko nyingine - Obama ni Mmarekani mweusi au mwenye asili ya Afrika na sio Mmarekani mweupe mwenye asili ya Afrika. Kwa kifupi race superior uchafuliwa na tunda haliwekwi kwenye race hiyo.

Waarabu wenye asili ya Kiafrika tunao wengi tu hapa Tanzania, tena tumewapa jina zuri kweli "waarabu koko"! Mbona race nyingine haulizii kama Wahindi? Kuna mji huko Nzega unaitwa Bukene ambao una waarabu koko kibao mpaka umepewa jina Maskat! Wewe ulitaka kilichotokea Bukene kingetokea Uarabuni?
 
Hivi unaamini kuwa habari za Tippu Tip alliandika huyo Jameson peke yake? Hicho kitabu alichoandika mwenyewe kinaitwaje?Unaposema alikuwa mfanyabiashara wa kawaida ulikuwa na maana gani? Huyo unayemuita mmachinga alipataje utajiri wake katika nchi ambamo biashara yake kuu ilikuwa utumwa? Unataka kutuambia alikuwa akifanya biashara gani? Hiyo mizigo ilikuwa mizigo ya nini? Na hao waliombebea aliwatowa wapi na baada ya safari walienda wapi? Ukiangalia umbali alikokuwa akitoa hiyo biashara yake basi hao wafanyakazi wote nao wangakuwa matajiri? Au mnataka kurudia tena uongo wenu kuwa hata biashara ya utumwa haikuweko Zanzibar?

Usitake kuandika historia upya. Hamuwatendei haki wale ambao waliumia kutokana na uovu wa utumwa. Si suala la uislamu au ukristu. Yeyote aliyehusika na biashara hii inabidi alaaniwe, awe mzungu, muarabu au mwafrika. Lakini laana hiyo haihusu vizazi vilivyomfuata.

Amandla........
Hili suala limekushtua,lakini ni tabia ya haki na ukweli hata zikipita karne ngapi huwa vinakuja juu kuzima uongo.
Wewe una hasara gani historia ikiandikwa upya iwapo iliyopo ni ya uongo.Unaposema Hamuwatendei haki wale ambao waliumia kutokana na utumwa na uovu wa utumwa.Yawezekana wapo lakini wewe wala mimi hatuwajui,kilichobaki ni kisingizio tu cha kuupiga vita uislamu.
Hizi picha za watu waliofungwa minyororo zilizochorwa na wamishionari ni vyema muzibandike makanisani kwenu mutakuwa mumeeleweka lakini kuziingiza mashule zimeidhuru sana Tanzania.Ni sababu ya mapinduzi ya Zanzibar,sababu ya uchafuzi wa uchaguzi wa kidemokrasia,sababu ya vifo vya watu wengi na kadhalika.
Eti kinachotetewa ni kuzuia kurudi kwa waarabu waliowatumikisha mababu zetu.Hakuna aliyetumikishwa kwa nia ya kutumikishwa mbali na mfumo wa maisha wa siku hizo.Hivyo wewe leo ukijenga ghorofa lako Kariakoo ukawalipa kwa kuwapunja vibarua wako,hilo ghorofa litakuwa si la kwako kwa kuwa uliwalipa hivyo.Hapo zitakapokuja mashine za kufanya kazi za kubeba kila kitu bila vibarua itakuwa nongwa kwa wajukuu kwamba babu zao walijenga ghorofa yako.
Nakuhakikishia mashamba yaliyotaifishwa Zanzibar kwamba ni ya mababu zetu,zile zilikuwa mali halali za waislamu zilizochumwa na wenyewe akina Tippu Tip.Ushahidi wa kiroho juu ya hili huna ubavu wa kuupinga.Ikiwa huyu sheikh alifanya makosa katika biashara yake wewe huwezi kuwa hakimu wake na nakushauri ukubali hivyo.
Maelezo hapo juu kuhusu Tippu TIP yako wazi kabisa.Kwanini hutaki kuyaamini na unalazimisha kuamini yaliyoandikwa na akina Livingstone tu!.
Akili yako ikoje wewe?,kwamba huoni kwamba Tippu Tip hakuwa mfanyabiashara ya utumwa?.Kama wako wenzake waliofanya biashara hiyo basi ilikuwa ni wachuuzi tu wa maagent wa biashara hiyo ambao ni wazungu-wakristo na wahindi.Nani mwenye kosa zaidi kati yao.?
Kuwazushia waarabu kwa nia ya kuipiga vita dini ya uislamu vitu ambavyo viko hai ni kutotenda haki zaidi kuliko kutetea kwa uzushi watu ambao huwajui.
 
Hili suala limekushtua,lakini ni tabia ya haki na ukweli hata zikipita karne ngapi huwa vinakuja juu kuzima uongo.

Hazijanistua. Hata Himmler akifufuka leo si ajabu atadai kuwa hakuhusika na Final Solution!

Wewe una hasara gani historia ikiandikwa upya iwapo iliyopo ni ya uongo.Unaposema Hamuwatendei haki wale ambao waliumia kutokana na utumwa na uovu wa utumwa.Yawezekana wapo lakini wewe wala mimi hatuwajui,kilichobaki ni kisingizio tu cha kuupiga vita uislamu.

Jizungumzie mwenyewe. Nimesimuliwa na bibi na babu zangu kuhusu namna walivyokuwa wakishikkwa. Watumwa walioachiliwa walikuwepo mpka karne iliyopita. Kwangu mimi hii biashara ilinigusa. Kama victim.

Kwa nini unapenda kuchanganya uislamu na uarabu? Wakina Jefferson walikuwa na watumwa, lakini mbona hatusemi kuwa walifanya hivyo kwa sababu walikuwa wakristu? Hapa tunamzungumzia mtu mmoja, Tippu Tip, ambaye alijihusisha na biashara ya utumwa. Alijitambua kama mwarabu na utawala wa kiarabu uliokuwepo wakati huo uliruhusu na kuendeleza biashara ya utumwa. Sijasikia mahali ambapo usultani ulilinganishwa na utawala wa kiislamu! Au ndio unataka kutuambia hivyo?

Hizi picha za watu waliofungwa minyororo zilizochorwa na wamishionari ni vyema muzibandike makanisani kwenu mutakuwa mumeeleweka lakini kuziingiza mashule zimeidhuru sana Tanzania.Ni sababu ya mapinduzi ya Zanzibar,sababu ya uchafuzi wa uchaguzi wa kidemokrasia,sababu ya vifo vya watu wengi na kadhalika.

Kwa sababu haufanani nao ndio maana unaona hazikugusi. Mambo ya mapinduzi Zanzibar yameingiaje humu? Kwani nani amedai kuwa kulikuwa na utumwa 1963 Zanzibar? Tubakie kwenye hoja inayohusu historia ya utumwa Zanzibar. Ulikuwepo au haukuwepo? Wakina Seyyid Said, Barghash, Majid walihusika na utumwa au hawakuhusika? Kulikuwa na soko la watumwa Zanzibar au halikuwepo? Yale majengo Bagamoyo yalihifadhi watumwa au hayakuhifadhi?

Eti kinachotetewa ni kuzuia kurudi kwa waarabu waliowatumikisha mababu zetu.Hakuna aliyetumikishwa kwa nia ya kutumikishwa mbali na mfumo wa maisha wa siku hizo.Hivyo wewe leo ukijenga ghorofa lako Kariakoo ukawalipa kwa kuwapunja vibarua wako,hilo ghorofa litakuwa si la kwako kwa kuwa uliwalipa hivyo.Hapo zitakapokuja mashine za kufanya kazi za kubeba kila kitu bila vibarua itakuwa nongwa kwa wajukuu kwamba babu zao walijenga ghorofa yako.

Kwa mantikk yako ni kuwa hapakuwa na biashara ya utumwa Zanzibar? Watwana wote walifanya kazi kwa hiari yao na wengine wakapanda madau kwenda uarabuni kwa kupenda wenyewe? Wakajifunga minyororo shingoni na wale waarabu waliosimama pembeni mwao wamebeba bunduki na mijeledi walikuwa wakiwalinda ili watu wabaya wasiwadhuru? Hauna hata aibu?

Nakuhakikishia mashamba yaliyotaifishwa Zanzibar kwamba ni ya mababu zetu,zile zilikuwa mali halali za waislamu zilizochumwa na wenyewe akina Tippu Tip. Ushahidi wa kiroho juu ya hili huna ubavu wa kuupinga.Ikiwa huyu sheikh alifanya makosa katika biashara yake wewe huwezi kuwa hakimu wake na nakushauri ukubali hivyo.

Nikubali udhalimu? kwa sababu muungwana ameniambia nifanye hivyo? Hata siku moja.

Mababu zenu waliwatendea maovu mababu zetu. Hilo hatutalisahau. Lakini si sababu ya kujenga chuki na vizazi vyao ili mradi havitaki kuandika historia upya na kujaribu kurudisha yaliyopita. Mimi si mzanzibari na wala hayo mashamba hayanihusu lakini jambo moja nilalijua. Ni kuwa walionitangulia walimwaga damu, walichapwa bakora, waliuawa, walihasiwa na kuuzwa kama bidhaa na waarabu waliokuwa wakiishi Zanzibar kwenye karne ya 19.

Maelezo hapo juu kuhusu Tippu TIP yako wazi kabisa.Kwanini hutaki kuyaamini na unalazimisha kuamini yaliyoandikwa na akina Livingstone tu!.

Yako wazi kwa vile ametajwa Tippu Tip? Hauwezi kubandika kitu bila kueleza kimetoka wapi, kitabu gani, kilichapishwa lini na nani halafu ukataka tukuamini. Tunajuaje kama uliandika mwenyewe? na hata kama ni kweli Tippu Tip aliandika , inategemea ni wakati gani aliandika. Kama aliandika baada ya biashara ya utumwa kupigwa marufuku na kulaaniwa bila shaka nae atataka kujisafisha! Au nyie bado mnatuona sisi mazezeta basi chochote ambacho mtatubandikia tutawaamini?
Akili yako ikoje wewe?,kwamba huoni kwamba Tippu Tip hakuwa mfanyabiashara ya utumwa?.Kama wako wenzake waliofanya biashara hiyo basi ilikuwa ni wachuuzi tu wa maagent wa biashara hiyo ambao ni wazungu-wakristo na wahindi.Nani mwenye kosa zaidi kati yao.?

Akili yangu iko safi kabisa, asante. Aha, sasa ndio umezungumza. Kwa hiyo biashara hiyo ya watumwa walikuwa wakiendesha wazungu wakristu na wahindi wahindu, na waarabu walikuwa ma-agent tu? Yaani wewe unayejiona mwenye akili safi unaamini kabisa katika nchi ambayo iko chini ya utawala wa waarabu wa Oman basi waarabu wote walikuwa ma-agent na hii biashara lucrative ilishikw na wazungu na wahindi! Na hao wazungu na wahindi hao watumwa waliwafanya nini? Au nao walikuwa na mashamba Zanzibar? Au waliwasafirisha kuwapeleka Marekani, Ulaya na India? Kwa hiyo hayo mashamba Unguja mliyanyang'anya kutoka kwa wazungu! Na, ndio, wote waliohusika na biashara ya utumwa walikuwa waovu, kuanzia machifu wetu walioshirikiana na babu zenu, wachuuzi, wahindi waliokuwa financiers, waarabu waliokusanya kodi kutokana na mauzo ya watumwa, waarabu waliowasafirisha watumwa wengine kwenda uarabuni n.k, wachina waliochukua watumwa hata kabla ya waarabu. Huko Afrika magharibi nako vile vile. Laana ziwaendee machifu na watu weusi wote waliowezesha hiyo biashara pamoja nawazungu walionunua na kuwasafirisha hao watumwa. hakuna aliye na afadhali. Wote walikuwa waovu.

Kuwazushia waarabu kwa nia ya kuipiga vita dini ya uislamu vitu ambavyo viko hai ni kutotenda haki zaidi kuliko kutetea kwa uzushi watu ambao huwajui.

Hatuwazushii waarabu na hakuna mahali ambapo nimehusisha uislamu na utumwa. Wewe ndiye unayefanya. Uislamu si uarabu kama vile uzungu usivyo ukristu. Usiyeitendea haki dini yako ni wewe kwa kuiingiza mahali ambapo haikuwemo. Kulikuwa na waislamu pande zote mbili, perpetrators na victims kama vile ilivyokuwa kwa wakristu.

Amandla.......
 
Kimsingi waarabu wenye asili ya kiafrika wapo japo si wengi. Angalia Tabora kigoma na sheilui. Hivi hawa kina rage siyo asili hiyo? Nadhani sababu ya kuwa wachache ni ile tabia ya waarabu kupenda mgongo zaidi badala ya sehemu maalumu.:angry:
 
Hivi unaamini kuwa habari za Tippu Tip alliandika huyo Jameson peke yake? Hicho kitabu alichoandika mwenyewe kinaitwaje?Unaposema alikuwa mfanyabiashara wa kawaida ulikuwa na maana gani? Huyo unayemuita mmachinga alipataje utajiri wake katika nchi ambamo biashara yake kuu ilikuwa utumwa? Unataka kutuambia alikuwa akifanya biashara gani? Hiyo mizigo ilikuwa mizigo ya nini? Na hao waliombebea aliwatowa wapi na baada ya safari walienda wapi? Ukiangalia umbali alikokuwa akitoa hiyo biashara yake basi hao wafanyakazi wote nao wangakuwa matajiri? Au mnataka kurudia tena uongo wenu kuwa hata biashara ya utumwa haikuweko Zanzibar?

Usitake kuandika historia upya. Hamuwatendei haki wale ambao waliumia kutokana na uovu wa utumwa. Si suala la uislamu au ukristu. Yeyote aliyehusika na biashara hii inabidi alaaniwe, awe mzungu, muarabu au mwafrika. Lakini laana hiyo haihusu vizazi vilivyomfuata.

Amandla........
Hiki kitabu nitakutajia lakini kwanza ngoja tujadili huu utumbo wako:
1.Mfanyabiashara wa kawaidi kwa mujibu wa hii thread ni yeyote mwengine ambaye hakufanya biashara ya utumwa.
2.Hii nchi hivi sasa ina biashara nyingi za halali na haramu.Kwani lazima watu wote wafanye biashara ya pombe ndipo watajirike?.Tippu Tipu wakati wengine wakifanya biashara ya utumwa yeye alikuwa akifanya biashara halali ya kusafirisha na kuingiza bdhaa nyengine kama vyombo vya nyumbani na shanga.
3.Mizigo ni kama hiyo hapo juu (3).
4.Inaelekea hukusoma yale maelezo pengine kwa kutilia shaka juu ya kuwepo kweli.Hata hivyo ungepaswa uyasome.Waliombebea ilikuwa ni vibarua ambao alikuwa akiwapata vijiji tofauti alivyopita.Wengi walikuwa wanabeba na kulipwa halafu wakarudi makwao kwa watoto wao kusubiri safari nyengine.Watumwa hawabebwi.
5."Ukiangalia umbali alikokuwa akitoa hiyo biashara yake basi hao wafanyakazi wote nao wangakuwa matajiri?".Hapa ndio kabisa huelewi unalosema!.Huu uchumi wa kila anayefanya kazi kutajirika umeusomea wapi?.
6.Humu hakuna aliyekanusha kuwa biashara ya utumwa haikuwepo.Lakini kuzipeleka lawama hizo kwa waarabu ni njama za kuupiga vita uislamu wa wamishionari kupitia mitaala ya kiinchi.Jengine aliyechorwa kuwafunga watu minyororo siye aliyefanya biashara ya utumwa.Hasa hasa Tippu Tipu anayetajwa kama icon ya biashara hiyo Afrika Mashariki hahusiki kabisa.

Hapa wewe na wenzako binafsi munakanusha kwamba uislamu si uarabu lakini nyinyi hamujui kwamba muko kwenye jamii yenye akili kali za kutambua mambo kama za kwenu.Iwapo thamani ya A=B na B ukaambiwa ni sawa na C (B=C). Basi lazima A=C.
Sisi huwa tunawasikia nyinyi mukishutumu Utumwa kwa kutumia kauli za wamishionari. Wamishionari walikuja kuupiga vita uislamu.Uislamu si uarabu,lakini huku kwetu uliingia zaidi kupitia waarabu.Sasa munaposhikilia kuwa waarabu walifanya biashara ya utumwa ni lugha nyepesi kwamba waislamu ni watu wabaya waliowatia utumwani mababu zetu pamoja na takwimu nyingi kupinga hilo.
Katika hii vita nyinyi ni watu wadogo sana kuelewa habari hii na mengi hamuyajui.kama ambavyo mimi ni mdogo sana kuwajibu nyinyi.
Hivi kwanini somo hili la utumwa unadhani ni kwanini linaendelezwa mashuleni?,magazetini,redioni na kwenye TV zenu katika dunia hii ya sayansi na teknolojia,iwapo si vita vya kisaikolojia kuwatoa watu katika uislamu na kuwaingiza katika ukristo?.Kwa upande mwengine kuzidi kuwatala waislamu hata wakibaki na uislamu wao.
 
Pamoja na kuwa haukutaja jina la hicho kitabu nitakujibu uongo wako.

1. Hii nchi ina watu milioni karibu 40 na eneo kubwa sana kulinganisha na ilivyokuwa Zanzibar. Hata hivyo hakuna mkazi wa Tanzania ambae anaweza kusema kuwa hafaidiki na biashara halali zote zinazofanyika humu. Kodi kutoka pombe, sigara zinachangia kwa kiasi kikubwa kujenga barabara zetu, hospitali, kulipa wafanya kazi wa serkali n.k. Zanzibar biashara yake kubwa ilikuwa ni hizo karafuu, meno (?) ya tembo, watumwa. Watumwa walitumika kubeba hayo meno ya tembo na walipofika Zanzibar walipigwa bei. Ni uongo kudai kuwa Tippu Tip alitumia vibarua peke yake kumbebea mizigo. Haiwezekani mfanyabiashara tajiri kama Tippu Tip aliyekuwa na mashamba makubwa tu asiwe na watumwa! Mwaka 1953 mashehe kutoka Qatar walihudhuria kusimikwa kwa Mallkia Elizabeth II wakiongozana na watumwa wao. Mwaka 1958 walifanya hivyo tena. Utumwa haukuwa kama biashara nyingine maana ulipenyeza kila nyanja za jamii. Watumwa hawakufanya kazi za thuluba tu. Watumwa wanawake walifanya kazi za ndani na wengine walihudumia haja za kimwili za wakuu wa nyumba. Watoto waliozaliwa walihesabiwa kama waarabu.

2. Wewe ndiye usiyejua. Kazi ya kubeba mizigo hiyo ilikuwa ya thuluba. Kwa hiyo mara nyingi walitumiwa watumwa kuifanya. Hawa ambao unawaita vibarua walipofika mwisho wa safari waliuzwa pamioja na mizigo waliyobeba.

3.Meno ya tembo yalitolewa kutoka maeneo ya mbali kama Kigoma, Tabora n.k. unataka kutuambia huyu nduguyo kila akifika mahali alikuwa akiwaachia hao unaowaita vibarua na kuajiri wengine? Ni mfanyabiashara gani ambae angekubali kulipa vibarua lukuki wakati angeweza kuwanunua na kuwauza ili kurudisha gharama zake?

4. Kama unakubali kuwa utumwa ulikuwepo nani basi ndiye aliyekuwa akihusika? Hao wamishionari walikuja karibuni sana na walikuta biashara hiyo haramu ikishamiri. Kusema kuwa walipinga utumwa kwa sababu waliupinga uislamu ni uongo mkubwa. Ukiangalia sehemu ambako umisheni ulishamiri ni sehemu ambako hapakuwa na himaya ya kiislamu. Kwa mfano,Wachaga hawakuchukuliwa kama watumwa ingawa walihusika katika biashara hiyo. Wamishionari nia yao ilikuwa ni kuongeza himaya ya watalwala wao na kueneza ukristu. Mara nyingi walifanya hivyo katika maeneo ambako uislamu haujashamiri.

5. Hata useme vipi, nduguyo Tippu Tip alihusika sana na biashara hii dhalimu.

6.Wewe ndiye unayeona kuwa wakiguswa waarabu basi wameguswa waislamu. Wamishionari walitoka ulaya wakaleta dini ya kikristu lakini mbona wakristu hawalalamiki mnapousema utawala wa kikoloni? Mbona utawala wa wajerumani na wareno unajulikana kwa ukatili wake? Mbona Mfalme Leopold wa Belgium anasemwa ssana kuhusu unyama alioufanya Kongo? Kwa hiyo wote hawa nao wasilaumiwe kwa sababu ni wakristu? Waislamu wabaya ni wale wanaotetea utumwa. Kama vile wako wakristu wabaya ambao wanatetea biashara ya utumwa. Biashara hii dhalimu haikuwa na dini. Ni wewe ndiye unayetaka kuipa dini.

7.Samahani lakini sentensi yako ya mwisho inaonyesha jinsi ulivyo mpuuzi. Utumwa ni sehemu ya historia yetu kama vile ilivyokuwa ukoloni. Watoto wetu ni lazima wafundishwe yaliyotokea katika nchi yao. Hivi wakifndishwa kuhusu wakina karl Peters na jinsi alivyokuwa akikata wat mikono ina maana wanafundishwa kuchukia wajerumani, na wakristu? Na hao wanaofundisha somo hilo la historia wote ni wamisheni? hauna hata aibu?

Hicho kitabu cha Tippu Tip kinaitwaje? nani alikiandika? Kilichapishwa na nani na mwaka gani?

Amandla......
 
Back
Top Bottom