Waandishi wanavyolisema Baraza Lao la Habari

May 29, 2012
89
38
Jana nilikuwa kwenye kijiwe changu hapa Morogoro. Nikabahatika kuwakuta waandishi wa habari wakigida kinywaji mahali. Si unajua kwa vya bure jamaa wanaongoza nchini. Nasikia ati walikuwa na semina hapa mji kasoro bahari. Lakini ambacho naomba wana JF wachangie ni malalamiko yao niliyonasa kwa mbali.
1. Walidai ati Baraza la Habari limekuwa kama genge la wajanja kuchuma
2. Bila kuwa na uhusiano wa kingono na wahusika wa MCT hasa kama ni mwanamke huwezi kuitwa kwenye semina. Wakadai wasichana hao wanapofika kwenye hizo semina wanawagawana kama njugu.
3. Kwamba ati mtendaji wao anatafuna mapesa ya baraza kama mchwa na ana kiwanda cha uchapaji ambako ndo anapeleka kazi za baraza.
4. Wakadai ati baraza badala ya kuwa wazi limegubikwa na usiri kibao, na wanaoalikwa kwenye hiyo mikutano ama semina ni walewale siku zote. Ni kama kampuni ya huyo katibu mkuu
5. Kimekuwa kituo cha wastaafu wa serikali, hasa majaji maana MCT lina ufadhili mnono
6. Kuna walioajiriwa hapo ambao mbali na degree zao hawana uwezo, wakamtaja mmoja kwa jina la Benzi.....
7. Wakagusia Tuzo ambazo walisema ulikuwa mradi wa wajanja kama ulivyo Miss Tanzania
Nilifanikiwa kunasa hayo machache, lakn inaonekana msemaji mshereheshaji alikuwa analijua fika Baraza hilo.
Nikabaki kushangaa kumbe hata waandishi wana ufisadi wa kutisha ingawa nilipata jibu kuwa na wao ni watoto wa mafisadi, na wanaishi kwenye jamii ya kifisadi.
 
Ukiona wameanza kulalamikia bar tena wakiwa pombe,watakuwa wamekosa mgao wao waliozoea kuupata.
 
Hii ni sanaa tu, wewe uliyeleta hii habari ni mwanadishi wa habari uliyekuwa ndani ya semina hiyo. Ndiyo maana unataka kujua Charles charles anafanya kazi ngapi! Tumeshakujua! Kaa kimya!
 
Back
Top Bottom