Waandishi wa Habari wanavyosalitiana na kujidhalilisha

tatizo letu waTz wengi hatuelewi maana halisi ya uzalendo,,, leo kauawa mwanahabari suala limepata uzito kwenye tasnia ya habari HATUONI kuwa kesho atauawa askari msemakweli, mwalimu, injinia, bodaboda e.t.c TUTAMBUE VITENDO VYA UKATILI HAVIBAGUI
 
Mkuu jigoku naunga mkono hoja yako. Udhamini wa itv/radio katika wiki ya usalama barabarani haiwezi kuwa na thamani kubwa kuliko uhai wa binadamu, mtanzania mwenzetu aliyeuwawa kinyama na hao hao polisi.
 
Last edited by a moderator:
navipongeza sana vyombo vyote vilivyo ripoti wiki ya usalama barabarani.
Huo ndio uzalendo,
waachane na mambo ya kukurupuka bila kufikiri yanayofanywa na baadhi ya wanahabari uchwara.
 
Maggid hakosi kwenye hilo kundi la wasaliti!

Right toka mwanzo maggid alishatangaza kutoungana na waandishi wenzake kususia habari za polisi. Kwahiyo yeye alikuwa wa kwanza kujitenga na wenzake na hakuna anayeshangazwa na yeye kuripoti habari za polisi.
Aibu ni kwa wale waliotangaza kususia habari za kipolisi lakini ndani ya muda mfupi sana wameshazungukana na kusalitiana kwa kulipamba jeshi la polisi hata kabla ya arobaini ya Mwangosi!
 
Last edited by a moderator:
navipongeza sana vyombo vyote vilivyo ripoti wiki ya usalama barabarani.
Huo ndio uzalendo,
waachane na mambo ya kukurupuka bila kufikiri yanayofanywa na baadhi ya wanahabari uchwara.

peri Kama walijua kwamba kutangaza habari za kipolisi hata pale lilipoua mwanahabari mwenzao ni uzalendo kwanini walitutangazia kususia kuandika habari hizo hadi arobaini ya Mwangosi?
Usaliti na kuzungukana ndio tafsiri mpya ya uzalendo?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mwita Maranya, hili tumeshalizungumza sana humu jukwaani.
Kwenye tasnia ya habari, kuna kitu kinaitwa "pressures shapping the news", hizi sio habari bali determinant factors zinazofanya habari fulani iandikwe na habari fulani isiandikwe!.

Moja ya factor kubwa kuliko zote ni "money matters"!. Survival ya vyombo vingi vya habari sio circulation, readership, viewership au audience bali ni matangazo!. Watangazaji wakubwa wanaitwa sponsors!.

Hawa sponsors are the ones calling the shots!. "He who pays the piper, may call the tune". Wiki ya Usalama Barabarani ni "sponsored event" hivyo mdhamini lazima atokee na huko ndiko mshahara unakopatikana!.

Uandishi wa kuajiriwa ni kazi ya kitumwa, waandishi ni watumwa tuu, kazi yao ni kutumwa!. Mtumwa hana uhuru wala ridhaa jukumu lake ni kutekeleza tuu matakwa ya masters wake!.

Kumlaumu mtumwa ni kumuonea bure!. Mtumwa ni mtu wa kuhurumiwa!.
Pasco!.

Ulichosema ni sawa kabisa! Sasa kwa nini mlitoa maazimio makali makali wakati mnajua nyie ni watumwa tu, hamna uwezo wa kuyatekeleza?
 
Ulichosema ni sawa kabisa! Sasa kwa nini mlitoa maazimio makali makali wakati mnajua nyie ni watumwa tu, hamna uwezo wa kuyatekeleza?

Kwetu Iringa hiyo ndio hoja ya msingi hapa. Kama kweli wanajijua wao ni watumwa kwanini wakakimbilia kutoa matamko makali kiasi kile huku wakitambua kwamba hawana uwezo wa kusimamia maamuzi yao?
 
Last edited by a moderator:
Ulichosema ni sawa kabisa! Sasa kwa nini mlitoa maazimio makali makali wakati mnajua nyie ni watumwa tu, hamna uwezo wa kuyatekeleza?
Mkuu Kwetu Iringa,

Hili nilishalijibu kwenye mada hii Waandishi Kugomea Habari Za Kipolisi; Naomba Nichangie Haya ...

Mkuu Matola,
1. Niko very specific, waandishi wa habari waajiriwa, hawana jeuri ya kususia habari za kipolisi kwa sababu ni watumwa, huko kususa, ni hasira za uchungu, zikipoa, wataendelea kuandika!, Maggid yuko right!.

2.Waandishi wa kujitegemea, tuko wa aina mbili, aina ya kwanza ni "freelance journalist", hawa wanaandika na kuitegemea hiyo habari ndio imlipe, newsroom nyingi zinalipa 3,000, 5,000 kwa habari moja itakayotoka, na labda 10,000 kama habari itakuwa ndio lead story!, huyu mwandishi akifanikiwa ku file story 1 tuu kwa siku na ikatoka, mwisho wa mwezi atavuta 90,000 tuu!. Waandishi wa kada hii ndio hutegemea "bahasha" to survive!.

3. Kada ya pili ni "independent journalists", kada hii ndiko mimi niliko, inahusisha kuandika just for the love of it, wengi wa kada hii tunazo shughuli zetu za kufanya to make our living, hivyo hatutegemei malipo yoyote kwa stories tunazotuma, mfano mimi silipwi hata senti tano kwa stories ninazofile kwenye media. Kundi hili ndio kundi kama la kina Mjengwa, Mzee Mwanakijiji etc, etc, enzi zile Mwanakijiji akitoa kile kijarida cha Cheche, alikitoa bure nasi tulikitawanya bure!. Kwa sasa Mjengwa, Mwanakijiji na wengine, ni waandishi wa makala mbalimbali kwenye magazeti mbalimbali. Kwa kawaida magazeti yanapaswa kuwalipa, sidhani kama wanaandika ili kujipatia hivyo vijisenti na I doubt hata kama wanachukua!. Kundi hili ndilo hatutumwi na mtu na hatumtumikii mtu zaidi ya jamii!.

5. Mwisho bado naendelea kulia na tatizo kubwa humu jukwaani, watu wengi humu tuna tatizo la kuukubali ukweli halisi baina ya "is" and "ought". Mjengwa ni mkweli wa "is" and so do I, wengi humu ukweli wenu mnaoukubali ni "ought" ambao sio ukweli halisi!. Nikukumnbushe mifano michache.

  • Habari za kipolisi ni habari za jamii, kuzisusia ni kuinyima jamii haki ya kupata habari, mwandishi makini, anaweza kwenda polisi na kuripoti habari za kipolisi kwa angle ya jamii bila kuwapa promo polisi, na bado kuitumikia jamii. Habari za kipolisi ni ukweli wa "is" na kususia ni "ought"!.

Pasco.

Pia niliongelea kwa kirefu, kwa nini waandishi hawawezi kususia habari za kipolisi!.
mimi namsupport maggid, ila pia nazama deep zaidi kidogo kuliko maggid,

1. Kisuso cha waandishi, sio kisuso cha kweli, ni kisuso cha hasira na uchungu wa kufiwa, siku zikipita, uchungu utapungua, hasira zitapungua na kwa RPC waandishi wataripoti!.

2. Wengi wa waandishi ni watumwa tuu, hawafanyi kazi kwa utashi wao bali hufanya kwa utashi wa editor na edotors ambao sio wamiliki wa vyombo vyao, nao pia ni watumwa tuu wa wamiliki, au waajiri wao, hivyo nao hawafanyi kazi kwa utashi wao bali utashi wa wamiliki "he who pays the piper may call the tune"!.

ila mimi kama Pasco wa JF, ni mwandishi wa kujitegemea, sijaajiriwa na yoyote, wala situmwi na yoyote, na siitegemei media yoyote kutumia habari zangu kwa sababu mwamuzi ni mimi ndio ninaamua habari gani niandike na media ipi nipeleke, kama ni gazeti, huamua gazeti gani nipeleke, au kama ni kwenye TV na redio, mimi mwenyewe ndio huamua pa kuipeleka!, hivyo nikiamua kugoma, naweza kugoma kiukweli kweli!, hivyo waandishi wenye uwezo wa kususia habari zozote sio za kipolisi tuu, ni wale tuu ambao sio "watumwa" yaani wale waandishi wanaojitegemea na sio hawa "watumwa" wanaotegemea vyombo vya habari!.

 
Right toka mwanzo maggid alishatangaza kutoungana na waandishi wenzake kususia habari za polisi. Kwahiyo yeye alikuwa wa kwanza kujitenga na wenzake na hakuna anayeshangazwa na yeye kuripoti habari za polisi.
Aibu ni kwa wale waliotangaza kususia habari za kipolisi lakini ndani ya muda mfupi sana wameshazungukana na kusalitiana kwa kulipamba jeshi la polisi hata kabla ya arobaini ya Mwangosi!
Mkuu Mwita Maranya, mara baada ya maggid kulizungumzia hili, kwenye uzi huu, Waandishi Kugomea Habari Za Kipolisi; Naomba Nichangie Haya ...mimi nilimsupport na kueleza kwanini waandishi wameamua kususa, na kwa nini hawataweza kususa!.
P.
 
Tanzania hakuna waandishi wa habari waandishi walikuwa zamani saizi kila muandishi anataka cheo cha kisiasa na kujipendekeza kwa watawala...waandishi wa Tanzania ni vodafasta.
 
Tanzania hakuna waandishi wa habari waandishi walikuwa zamani saizi kila muandishi anataka cheo cha kisiasa na kujipendekeza kwa watawala...waandishi wa Tanzania ni vodafasta.
Mkuu Ritz, ukisema siku hizi hakuna, unakuwa hujasema kweli, unamaanisha hawa waliopo sasa ni kina nani?!, naamini unajua wazi, waandishi wapo japo sio kama wale wa zamani, lakini wapo!. Kitendo cha kukanusha ukweli halisi uliopo ni kujifariji!. If it makes you happy kujiaminisha kuwa siku hizi hakuna waandishi, ilhali ujajua fika wapo!, then be happy!.

Hiyo hoja yako ya hakuna mwandishi, imekuwa defeated na hoja yako ya "kila" mwandishi, anataka cheo na kujipendekeza, sasa kama hakuna mwandishi, sasa huyo anayetaka cheo na kujipendekeza ni nani?!, au ulimaanisha wote waliopo sio waan dishi, bali ni vimbelembele wataka vyeo wanao pose kama waandishi?!. Hapa napo tuwe wa kweli, hivi ni waandishi wote kabisa wanajipendekeza?!, hakuna exceptions?!. Mimi nakiri, kweli wapo wanaojipendekeza ila ni baadhi tuu na sio wote!.
Pasco.
 
Mkuu Pasco,
Ninaposema hakuna waandishi nadhani umenielewa vizuri, mkuu angalia magazeti yetu ambao ndio kipimo cha kuwajua waandishi wetu.

Unategemea nini waandishi wa habari wana kadi za vyama vya siasa wanapigana vikumbo na wanasiasa kuchukuwa fomu za kugombea ubunge mfano angalia waandishi wa magazeti ya Tanzania Daima, Rai, Uhuru, Mzalendo, Nipashe, Majira.

Kuna waandishi wa habari ambao ndio viongozi wa chama waandishi wa habari hawamtambui Rais Kikwete, wanamuita jina lake Kikwete na rais wao ambae ni Dr Slaa.

Waandishi wa magazeti Uhuru, Mzalendo, hawa wao ni kuisifia CCM na serikali.
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana nawe kabisa, umeliangalia hili jambo kwa mapana yake.... Biashara, ajira, habari kama habari, ushindani, sponsors interests, audience..... etc
 
Back
Top Bottom