Waandishi wa habari wa Dar, posho za wanasiasa zitawafanya muuze nchi

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
117
Tunatambua kweli kuna Taaluma ya waandishi wa habari. Kazi yao ni kuburudisha jamii, kuelimisha na kutoa habari. Bahati nzuri au mbaya siku hizi kila mkoa una wawakilishi wa kuandika habari kupitia karibu kila chombo. tunashindwa kuelewa kwanini wanasiasa wanapotoka Dar kuja mikoani Waandishi mnanunuliwa kuja kuandika kulingana na matashi ya hao wanasiasa.

Je mtajenga nchi kwa kutumia taaluma hivi. Juzi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Kijana anayetuhumiwa kuwa na uraia wa nchi mbili, ambaye amedhalilisha wadogo zake kwa kuwapeleka Arusha kuwaonyesha kwa wazungu eti anawasomesha, alikuwepo Singida.

Hakutumia waandishi wa Singida, badala yake anakuja na timu ya kukodi, timu ambayo haina ushahidi wa mambo wanayoandika ndo hao akaenda nao kijijini, wakatoka kule kutuletea habari za uongo. Tutumie taaluma vizuri, ila pia mnapokodishwa waandishi muwe mnajiuliza, mnasaidia taifa au kuangamiza.

MWANDISHI ANAYEPANDA STK, STJ, DFP kwenda katika Field, hataandika bila kuegemea upande wa yule aliyemleta. Lakini huyu Mwandishi anasaidia jamii. HABARI ZA KWELI, ZA UHAKIKA NA ZENYE USHAHIDI KUTOKA ENEO HUSIKA, WANAZO WAANDISHI WA MAENEO HUSIKA.

NI AIBU HATA WAANDISHI WANAOKODISHWA WAKIFIKA ENEO WALIKOPELEKWA HAWAWASILIANI NA WAWAKILISHI WENZAO KATIKA ENEO WALIPO. URAFIKI WA WAANDISHI NA WANASIASA UNATUHARIBIA NCHI.

HATUANDIKI UKWELI, TUNAANDIKA KULINGANA NA WALIOTUCHUKUA.............aibu sana
 
Hao sio waandishi bali ni makanjanja wenye njaa ambao utumiwa kwa muda baada ya hapo utupwa kama kapi la muwa.
 
Wadau mnakumbuka mwandishi mmoja alishushwa msituni huko Morogoro kwa amri ya Mkuu wa mkoa kisa aliandika ukweli wa mambo. Kuna haja ya waandishi kuwezeshwa kutumia vyombo vyao wenyewe vya usafiri badala ya kutegemea lift za wanasiasa. Otherwise wataishia kutishiwa, kukosa posho na lift za kufanya coverage..
 
Hapa Tanzania waandishi habari weredi wanahesabika na huwezi kuwakuta wakienda kusaka habari. Hao wasaka habari si waandishi ni wasaka posho. Ukiwa na kahabari kako mbuzi wewe waalike wape chips za kwenye mabox na ka posho kengine kadogo kakumpelekea mhariri wa habari. Basi habari yako utaiona imepambwa hata ambayo hukuongea yanawekwa ili mradi tu uonekane uliongea mengi na ya maana!
 
​waandishi wengi wa kibongo ni MAKAVIRONDO tu........................wanatumiwa.
 
Back
Top Bottom