Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa

Mkuu The Boss, bahasha ni dunia nzima mpaka Ikulu inatembeza bahasha, hiyo PCCB yenyewe na mpaka Polisi wanatembeza bahasha halali kama wanavyotembezewa!.

dunia nzima kivipi?
waandishi wa kenya wanapokea bahasha?
marekani?
uingereza?
south africa?????
 
msipo kuwa waangalifu juu ya hizi bahasha unazoziongelea,mwisho wa siku mtajikuta mkiishia jera baada ya kuandika habari za uchochezi na zenyekuleta vita kama ilivyotokea rwanda na burundi

muwe makini sana na hizo bahasha,kwani wananchi hawataelewa kama ipi ni bahasha halali na ipo ni bahasha rushwa,zote hizo wananchi tunaziita ni rushwa tu

Pasco,mimi nakuhakikishia kama wewe binafsi utajikita ktk uandishi wa habari za kiuchunguzi,huna haja hata ya kuomba bahasha,watu ama vyombo vya kimataifa,mahakama zitahitaji kununua habari zako na wazitumie kama ushahidi ktk mambo yao na hapo ndipo utaona faida ya uandishi kuliko hivi sasa mmekuwa kama watumwa wa vibahasha
 
dunia nzima kivipi?
waandishi wa kenya wanapokea bahasha?
marekani?
uingereza?
south africa?????

hiyo ni kweli nakubaliana nae,inafikia kipindi mamlaka inapotaka habari zake zisikike na ziandikwe vyema hupitisha bahasha za kukirimu waandishi ama tv,kama ilivyotokea ktk lile sakata la Mauaji ya ARUSHA
 
na wasi wasi hawa waandishi wa TZ tunawapa heshima wasiostahili...
binafsi ningeona mtu ananitukana kunipa bahasha kwa kazi ambayo naamini ina heshima na mshahara wa kutosha...

kitendo cha mtu ambae sio muajiri wako kukupa pesa kinadhalilisha hasa kama unajiita na kujiona ni 'proffesional'...
 
Mkuu Lunyungu, ni kweli waandishi wa habari hupokea bahasha, na mimi kama mwandishi, nimeishazipokea sana, mpaka sasa mimi ndio nazigawa, ila ukweli halisi wa mambo, sio kweli kila bahasha mwandishi anayopokea ni rushwa!. Ziko bahasha waandishi wanapokea sio rushwa na zipo bahasha kweli ni rushwa. Sasa tuanzie hapa, na mimi nitaendesha hilo somo kidogo kidogo kwa kutoa dozi ndogo ndogo mpaka hatimaye mwisho wa siku tutaelewana na mtatuelewa sisiado tunazungumzia bahasha kama bahasha na hakuna uthibitisho kuwa bahasha hizi ni rushwa!.[/COLO!.
Una bahati ndugu yangu, bahati nzuri ni kuwa PCCB wamelala na wanakoroma. Hii aya ni admission of the offense of corrupt transaction. Kupokea na kutoa vyote ni kosa.
 
hiyo ni kweli nakubaliana nae,inafikia kipindi mamlaka inapotaka habari zake zisikike na ziandikwe vyema hupitisha bahasha za kukirimu waandishi ama tv,kama ilivyotokea ktk lile sakata la Mauaji ya ARUSHA

ukweli upi?
nchi zoote hizo kuna bahasha????
 
Una bahati ndugu yangu, bahati nzuri ni kuwa PCCB wamelala na wanakoroma. Hii aya ni admission of the offense of corrupt transaction. Kupokea na kutoa vyote ni kosa.

Tena wanabahati sana wamewakuta hao PCCB ni toothless au kwa kiswahili wapo butu kisu chao hakikati hata keki, kama wangekuwa nchi nyingine Pasco na Walarushwa wenzake wanopenda vibahasha wangekuwa histori katika fani ya uandishi wa habari.

Halafu tunategemea wakina Pasco waandike habari za walarushwa wakti wao wenyewe ni walarushwa wa vibahasha. Siwezi kumtofautisha kati ya Pasco na lile Jeshi la CCM la Polisi au TRA na walio Magogoni wote ni wamoja na waangamizaji wa Taifa letu.

Shame on them
 
I can't believe this...kweli adui muombee njaa. Ndio maana magazeti na tv zetu zimejaa upupu maana habari haitoki mpaka bahasha
 
Waandishi wa Tanzania wapo useless kama walivyo viongozi wa magogoni, wavivu wakutafuta habari na wapumbavu kwenye kuuliza maswali magumu, hawajijui wala hawajielewi wapo wapo tu wanasubiria bahasha kutoka kwa mafisadi waliokubuhu kwa rushwa ndio waandike
 
Tena wanabahati sana wamewakuta hao PCCB ni toothless au kwa kiswahili wapo butu kisu chao hakikati hata keki, ]

Toothless bulldog, to say the least. Waandishi wanachofanya ni Kupokea rushwa per se na wanaotoa wanatoa rushwa kwa sababu Mtu anatumia ofisi na wadhifa wake baada ya kupata kitu kidogo
 
Mkuu The Boss, bahasha ni dunia nzima mpaka Ikulu inatembeza bahasha, hiyo PCCB yenyewe na mpaka Polisi wanatembeza bahasha halali kama wanavyotembezewa!.
Pasco,
Hapana. Bahasha si dunia nzima. Mimi nimefanya kazi ya uandishi kwa mashirika mawili makubwa ya Kimarekani. Ilikuwa ni marufuku kupokea bahasha ya aina yeyote ile kutoka kwa mtu, shirika, au kampuni yoyote ile unayoripoti juu yake. It is unethical. Huwezi kuchukua hela kutoka kwa mtu au kampuni unayoripoti juu yake. Hapa Marekani wale waandishi habari wanaofuatana na Obama ambao wana "cover" White House, wakisafiri kwenye Air Force one, kampuni yao hupelekewa bill na White House. Hata waandishi habari wa Uingereza nina hakika hawaruhusiwi kuchukua bahasha. Tulichokuwa tunaruhusiwa ni kuhudhuria luncheon, tuseme kama Thabo Mbeki amekaribishwa kutoa mhadhara kwenye taasisi moja ya Kimarekani, sisi waandishi wa habari tunaohudhuria tunashiriki pia kwenye luncheon hizo au dinner, depending kama ni mchana au jioni, na ofisi zetu zinakuwa na taarifa. Lakini hatuwezi kupokea gratuity yeyote kutoka kwa mbunge, senetor, gavana au CEO tunayekwenda kufanya mahojiano naye. It is illegal and unethical.
Kama hayo yanatokea katika third world usiseme ni duniani kote.
 
Pasco anataka kuhalallisha Rushwa ya vibahasha kama ndio wajibu wa waandishi wa habari, nimesema na ninasema kuwa waandishi wa habari wa Tanzania ni wapumbavu na wajinga, wengi wao hawajui hata kuuliza maswali hasa wanapo wa-Interview Viongozi wa Serikali unaona kabisa kuwa wanafanyakazi kwa woga, kujipendekeza, kujichekeshachekesha hovyo na maswali wanayoyauliza ni ya kipumbavu sana mpaka muangaliaji au msikilizaji unaboreka. Tanzania hatuna waandhi wa habari bali tuna wachumia tumbo na kama wapo ni wachache hawafiki hata 10 nchi nzima.
 
Je hao watoa vibahasha wananufaika na nini kama unavyosema ni zawadi, haiwezekani kila siku hao watu wanakupeni vibahasha kwa kazi mnazolipwa na waajiri wenu au makampuni yenu. Au ndio tuiite posho?

Pasco najua utavitetea vibahasha kwa nguvu zako zote ndio vinavyokunufaisha katika kupunguza makali ya maisha lakini ujue hiyo ndio Rushwa ambayo sisi Watanzania walalahoi tunaipiga vita kwa nguvu zote. Hivi umeshapokea vibahasha vingapi kutoka kwa Lowassa? na Je hizo pesa wanazitoa wapi hao wanaokupa hizo bahasha?
Mkuu Mzalendo80, kwa vile ndio kwanza niko kwenye mada ya bahasha zipi ni halali na zipi sii halali, kwenye bahasha halali, pia naelezea uhalali wake, lengo la hizo biashara halali, ni ama usafiri, "transport", ama chakula "lunch" ama posho "allowance", ama ni masurufu "per diem", ama ni maduhuli "imprest" etc. Matumizi ya posho na marupurupu ni halali!, sasa wanaotoa hayo marupurupu wanapata nini, jibu ni nothing, kama wa wabunge wanavyolipwa posho ya laki 200,000 kwa siku, anayewalipa anapata nini?.
 
Naona Tanzania tumekuza culture ya kuhalalisha vitu ambavyo ni kinyume cha maadili. Sasa kama hata TAKUKURU wanatoa bahasha ni nani atakayemfunga paka kengele? Katika uandishi tunafundishwa kabisa na Pasco anajua, kwamba ni unethical kuchukua payments kwa kuandika ripoti za habari. Kwa hiyo haijalishi Pasco ataipambaje, iwe gratuity, au takrima, ni rushwa pure and simple. Tulifundishwa hivyo na ndivyo inatakiwa iwe. Vyombo vya habari vinapaswa kuwa na expense accounts za kulipia usafiri wa waandishi wao ikiwa wanafanya coverage, na vinapaswa kutoa hela ya posho ikiwa mwandishi atashinda nje akitafuta habari. So, Pasco, whichever way you cut it, it amounts to corruption. Just think, how can you write anything critical of a minister or ministry that has given you a stuffed envelope? Na ndio maana wanakimbilia kutoa bahasha kwa sababu wanajua hamtawauliza maswali magumu. Badala ya kuwa waandishi mnakuwa public information officers wa wakubwa hao.
 
asante
ndo maana nimeuliza huu utamaduni ni wa kimataifa au la?
taaluma ya uandishi wa habari ni taaluma universal....haiwezekani waandishi wa TZ
wakajiundia utaratibu wao wa kipekee
naoja hakuna anaenijibu hilo swali.....
 
dunia nzima kivipi?
waandishi wa kenya wanapokea bahasha?
marekani?
uingereza?
south africa?????
The boss, kama nilivyosema ni dunia mzima, na kwa vile mada zinashuka kidogo kidogo, kotye huko nitafika!. Bahati nzuri nimefanya kazi ya uandishi huko Marekani, Uingereza, Uswisi, Italy, Sweeden, India na most African countries, hivyo sibahatishi bahasha halali zinatembea mwanzo mwisho!, Endelea kuvuta subira nitakufikisha mpaka huko!.
 
asante
ndo maana nimeuliza huu utamaduni ni wa kimataifa au la?
taaluma ya uandishi wa habari ni taaluma universal....haiwezekani waandishi wa TZ
wakajiundia utaratibu wao wa kipekee
naoja hakuna anaenijibu hilo swali.....
The Boss,
Mwaka 1998 niliendesha semina ya waandishi wa radio na TV pale DSM na Arusha. Tulipofika katika mada ya ethics nikazusha hili suala la kupokea bahasha kutoka kwa mawaziri au watu wakubwa. Waandishi wote pale walikuwa na msimamo kwamba bahasha ni essential kwa kazi zao, nikasema hapana. Tulibishana mpaka nikaona heri tukubaliane kutokukubaliana. Lakini niliwakumbusha kuwa huwezi kuwa partial unaporipoti juu ya mtu anayekupa bahasha. Utatoa ripoti nzuri tu juu yake. Ni kweli kama usemavyo wenzetu Tanzania, na nchi nyingine zinazoendelea ambazo zimeendekeza mtindo huu, zinajiundia utaratibu wa kipekee, na ndio maana Pasco amekazana kuziweka hizo bahasha katika mafungu mbalimbali. Ningepata fursa nyingine ningependa kukutana na wale wanaomiliki magazeti, radio na tv niwaambie kuwa lazima watenge fungu la expenses za waandishi wa habari kwa sababu kuendekeza hii tabia ya kutegemea vibahasha ndiko kulikopelekea waandishi wetu wawe wavivu, wasiwe critical, na washindwe kutimiza wajibu wao kama fourth estate.
 
Huyu Pasco ni muandishi wa habari Uchwara na mchumia tumbo, njaa itampeleka pabaya kama anaacha professional yake kwa kuendekeza vibahasha vya Mafisadi, basi hata kudharauliwa ni haki yake kwa kuwa ameshajidharaulisha mbele ya Jamii ambayo wengi wao ni sisi walalahoi. Tunawapiga vita Mafisadi kumbe hata ndani yetu kuna Mafisadi wanaopokea rushwa kwa vibahasha. Kweli kwenye msafara wa Mamba, Kenge hawakosekani. Siajabu hata vocha za kuingilia JF amepewa na Mafisadi, who knows? I feel sorry for Pasco na waandishi wa habari uchwara kama yeye kwa kutumikia Mafisadi na kupindisha ukweli. Watanzania tunasafari ndefu ya kupiga vita rushwa, tusife moyo tutashinda hii vita dhidi ya Mafisadi na watuchumia tumbo wao kama Pasco
 
Back
Top Bottom