Waandishi wa habari arusha kukutana na wadau kujadili mitafaruku baina yao

BigMan

JF-Expert Member
Feb 19, 2007
1,096
135
kutokana na mitafaruku iliyojitokeza hivi karibuni ikiwemo tukio la polisi kuharibu vitendea kazi vya wanahabari na kuwapiga wakati wa maandamano ya chadema jijini arusha januari 05,2011,waandishi wa habari wa arusha wa arusha kwa kushirikiana na muungano wa klabu za waandishi wa habari nchini sasa wamepanga kukutana na wadau wote ambao pia watapata fursa ya kuwanyooshea vidole waandishi wote wanaolazimisha mishiko na kuwatisha.WADAU WOTE MANATAKIWA KUTOKOSA KABISA JUMUIKO HILO.


ARUSHA PRESS CLUB (APC)
P .O. BOX 6011
ARUSHA- TANZANIA
TEL;0713-231752/0754-299861​
Email;arushapressclub@gmail.com​

clip_image001.gif
20/1/2011

YAH: MKUTANO BAINA YA WADAU NA WAANDISHI WA MKOA WA ARUSHA

Unaalikwa kuhudhuria mkutano baina ya waandishi wa habari na wadau wa mkoa wa Arusha, utakaofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Azimio la Arusha tarehe 28/1/2011 kuanzia saa 2.30 asubuhi.

APC kwa kushirikiana na UTPC wameamua kuitisha mkutano huo, ili kutoa fursa kwa wadau na waandishi wa habari, kukutana kujadiliana changamoto zinazowakabili.

Hivi karibuni mahusiano baina ya wadau na waandishi yamezorota sana, ambapo kila mmoja anamtupia lawama mwenzie. Yapo malalamiko mengi toka kwa wadau dhidi ya mwenendo mbaya wa waandishi, na pia yapo malalamiko ya waandishi dhidi ya wadau kuwapiga na kuwavunjia vifaa waandishi.

Kutokana na umuhimu wa wadau na waandishi, imeonekana ni vyema kuwakutanisha kwa azma ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo haya.
Kwa kuwa wewe ni mdau muhimu unaombwa usikose kuhudhuria mkutano huu.

Ratiba ya mkutano utaikuta ukumbini.

Natanguliza shukrani


Katibu Mkuu
Eliya Mbonea
 
Back
Top Bottom