Waandishi mngekuwa na umoja tangu mwanzo Mwangosi asingeuliwa

nkisumuno

JF-Expert Member
May 22, 2012
208
72
Kabla ya Mwangosi kumetokea mambo mengi ya kuashiria manyanyaso kwa wandishi wa habari kama vile kumwagiwa tindikali kwa Saed kubenea jambo ambalo lilikuwa kiashiria kibaya na endapo mngeungana na kupaza sauti kama mnavyofanya sasa pengine haya yasingetokea. Nadhani mlifukiri yeye ni yeye na nyie ni nyie. Matokeo yake mmeyaona.

Gazeti la Mwanahalisi limefungiwa wakati ambapo linahitajika mno kwa watanzania lakini wandishi wa habari mmeshindwa kupaza sauti kwenye vyombo vyenu na ninahisi kuna watu wamefurahia kufungiwa kwake ili muuze yenu jambo ambalo mimi naona si haki. Mungekuwa kitu kimoja naamini leo hii polisi wasingethubutu kuwachezea.

Nawashauri kifo cha Mwangosi kiwe chachu ya mabadiliko muungane zaidi, mudai gazeti la Mwanahalisi lifunguliwe. Kuna wale waandishi walipewa tuzo wakati fulani lakini kutokumuona Kubenea akipewa tuzo nilijiridhisha kuwa zile tuzo hazikuwa na mshiko kwa upande wangu kwani makala zake zilikuwa nzuri na ziliibua uozo mwingi.

Nawaomba badilikeni kuweni kitu kimoja kama mlivyoonyesha umoja kwenye maandamano ya jana japo mmechelewa ndiyo maana yametokea yaliyotokea.

Au wadau mnasemaje?
 
Akili kichwani, mambo mengine mkiyaendekeza mtakufa njaa. Hayo waachieni wana harakati wao wana wafadhili, na wana siasa nao wanajua wanavyoishi, nyie endeleeni na kazi zenu za kutafuta habari na matukio mengine, tuko pamoja.
 
Back
Top Bottom