Waandishi Mbeya walivyotia aibu wakati wa ziara ya Dk. Slaa mkoani Mbeya, wagombeana mshiko

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,890
382
Kumezuka malumbano makali miongoni mwa wanahabari wa mkoa wa Mbeya wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroard Slaa kufuatia waandishi wa habari wa magazeti ya NIPASHE na TANZANIA DAIMA kudaiwa kuweka kibindoni mshiko wa Sh.300,000 uliotolewa na viongozi wa chama hicho ili wagawane wanahabari wote walioshiriki ziara hiyo. Taarifa kutoka katika ziara hiyo zinadai kuwa Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima, Angelica ndiye aliyekabidhiwa Sh.300,000 akiwa na Mwandishi wa Nipashe Emmanuel Lengwa ili wakawagawie wenzao. Hata hivyo katika hali ya kushangazai waandishi hao wawili wakaamua kugawana wenyewe mshiko huo kitendo ambacho kimeudhi waandishi wengine.
 
Yale yale ya bungeni na wizara ya Ngeleja. Waandishi wa habari wanapewa pesa ili iweje? Waajiri wao mbona wanawalipa?
 
Hao wengine walionyimwa ni wa magazeti gani?

Kama unaanzisha thread na kusema wamegombea mshiko, halafu unawataja waliopata bila kuwataja waliokosa, hapo maana halisi ya "kugombania" haina mantiki.
 
Hao wengine walionyimwa ni wa magazeti gani?

Kama unaanzisha thread na kusema wamegombea mshiko, halafu unawataja waliopata bila kuwataja waliokosa, hapo maana halisi ya "kugombania" haina mantiki.

Hii ni tuhuma iliyotungwa kwa akilisana!
Nia ya mleta mada ni kuwadhalilisha CDM, lakini ameweka heading inayokwepa asijulikane na mchezo wake wa hovyo!
Watu wa namna hii ndio wananunuliwa kwa bei ya mafungu na Ndugu Manywele!
 
basi samahani mkuu..yaishe nakuomba usibonyeze hio kitu kwani ndio nimetoka tu kifungoni

yap,.................. afadhali umnekuwa muungwana.................. manake mtu ukilinganishwa na bongo yetu ilivyo sasa, ikibidi kupigana we pigana tu................... heri lawama kuliko ................. halafu unabahati sana wewe mtakatifu, nilisahau kubonyeza nikapitiwa na usingizi.................. teh teh ............hail Saint Ivu.......................
 
Back
Top Bottom