Waandishi makanjanja na makala zao!

Status
Not open for further replies.

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
263
13
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi amedhihirisha kuwa ni kigeugeu kuhusu Baraza la Habari la Kislamu(BAHAKITA). Katika kipindi cha mwaka jana, Mwenyekiti huyo amekuwa akilalamikia baraza hilo kutumika kuchafua majina ya watu. Baraza hilo linaongozwa na Sheikh Chifu Msopa na Sheikh Mwaipopo. Katika kipindi hicho baraza hilo lilikuwa likifanya mikutano ya waandishi wa habari na ya hadhara kukemea wanaotumia vita dhidi ya ufisadi kwa malengo yao. Baraza hilo la waislamu lilianza ziara za mikoani na kufanya mikutano ambayo walihutubia kuwa Mengi ana malengo ya kisiasa ya kugombea urais ndio maana yuko mbele kwa kutumia vyombo vyake kuchafua wafanyabiashara na wanasiasa wengine. Katika kipindi hicho hicho, masheikh hao wamekuwa wakifanya ziara za kuibeza Operesheni Sangara inayofanywa na CHADEMA na kutaka waislamu waipuuze.

Baada ya kumaliza kuzunguka katika mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga na Tabora sasa wamerejea Dar e salaam. Na sasa Masheikh hao wameanza kampeni ya kumuuita Yusuph Manji fisadi. Masheikh hao wanaeleza kwamba Manji ametoa rushwa kwa baadhi ya viongozi wa BAKWATA ya shilingi milioni 80 na kumpa kiwanja cha Waislamu walichopewa na Nyerere katika eneo la Chang’ombe. BAHAKITA pia imetangaza kwamba huu ni mtindo wa kawaida wa Manji kwani alishafanya ufisadi huo katika ukarabati na uuzaji wa majengo ya NSSF. Kutokana na uamuzi wao wa kumshambulia Manji, Bwana Mengi amegeuka badala ya kutoka kuwalaumu BAHAKITA sasa anawaunga mkono.

Hawa ndio Masheikh wale wale, ambao ITV ilirusha hewani mkanda wa video ukiwaonyesha wakipanga mpango wa kuzunguka mikoani kumchafua mfanyabiashara mmoja(Mengi) na mwanasiasa mfanyabiashara wa chama cha upinzani(Mbowe). Uamuzi wake Mengi kukikumbatia kikundi hicho dhidi ya Manji umefananishwa kuwa sawa na kula matapishi yake. Manji ni mmoja wa wadhamini muhimu wa kifedha wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), na katika orodha ya wachangiaji jina la Mengi lilikuwa chini ya Manji kutokana na mchango wake mkubwa kwa chama.

………….ndiyohiyo
 
Ungesema Mhariri kala matapishi yake, Katika uandishi na kutafuta habari Mengi ni raia kama wewe na mimi
 
Mkuu angalia, si mashehe hao, ni wajasiriamali. Na kumbuka, anamlipa mpiga zumari...
 
Sorry mkuu sijakupata vilivyo hapa......! Mengi amekula matapishi yake vipi? Je, ni kwa ITV kurusha tamko la BAHATIKA kuhusu ''ufisadi'' wa Manji kny kiwanja wanachodai ni chao? Kwa Mengi ni msimamizi wa matangazo ya ITV? Hata angekuwa msimamizi, ulitaka wasirushe hiyo habari eti tu kwa sababu previous walikuwa na misunderstandings? Tena kwangu mimi hiki chombo (japo wewe unasema Mengi) kimeonesha objectivity ya hali ya juu sana kwa kurusha habari ile na ndivyo vyombo vyote vya habari vinatakiwa viwe! Habari zote zipewe uzito sawa hata kama inamhusu adui yako etc.
 
Ungesema Mhariri kala matapishi yake, Katika uandishi na kutafuta habari Mengi ni raia kama wewe na mimi

weweeee weeee anatenganishwa nani hapo? Fuatilia kwa makini.

Sorry mkuu sijakupata vilivyo hapa......! Mengi amekula matapishi yake vipi? Je, ni kwa ITV kurusha tamko la BAHATIKA kuhusu ''ufisadi'' wa Manji kny kiwanja wanachodai ni chao? Kwa Mengi ni msimamizi wa matangazo ya ITV? Hata angekuwa msimamizi, ulitaka wasirushe hiyo habari eti tu kwa sababu previous walikuwa na misunderstandings? Tena kwangu mimi hiki chombo (japo wewe unasema Mengi) kimeonesha objectivity ya hali ya juu sana kwa kurusha habari ile na ndivyo vyombo vyote vya habari vinatakiwa viwe! Habari zote zipewe uzito sawa hata kama inamhusu adui yako etc.

Mbona kwenye shghuli ya Tarime Masha alikuwa mgeni rasmi lakini wakati wa kutoa habari ITV haikuonyesha HATA KIVULI CAHKE?????
JUST THINKING LOUD.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom