Waandishi Kugomea Habari Za Kipolisi; Naomba Nichangie Haya...

Sasa mimi nina hisia Nyingine. Hivi sasa natamani nione msimamo wa Mwandishi Mwingine baada ya Maggid Kuuliwa na Polisi. Yaani maggid ajifanye yeye ndo Mwangosi alafu atoe Msimamo wake kuhusu kuwasusia Polisi.
 
Ndio maana sishangai watoto wa Maggid kutumia ubini wa Mama yao. Kumbe Wananwake wa Kizungu wanaona mbali sana. Huyu jamaa ni Bogus kabisa na narudia kusema asingeolewa na mwanamke mzungu huyu jamaa angekuwa ni mchawi sasa hivi.

Tunashukuru kwa taarifa Mkuu. Wengi wetu tulikuwa hatujui hili swala..

TUMBIRI (PhD, HULL University, HULL City - UK),

tumbiri@jamiiforums.com
 
maggid ni kwa nini umekuwa mnafki kiasi hiki? watu tumeccoment kwenye blog yako na commet zikawa reviewed na kuwa published, je ni kwa nini wewe umezifuta? ndio maana unatetea udikteta kwa sababu hata wewe ni Dikteta kwenye blogu yako?

kuna maana gani wasaidizi wako wanaziaprove comment halafu wewe unakuja kuzifuta kwa sababu umekosolewa na kuambiwa ukweli? kwanza who are you by the way mpaka uone unalowaza wewe ndio sahihi kuliko Umma wa Watanzania? wewe jamaa ni mshamba kweli kweli na ndio maana hata mwili wako unaonesha kabisa ni mtu mwenye roho ya kimaskini kabisa. Appearance speak itself.
 
Ndugu zangu,
Ukweli wengi mmeelezea fikra zenu kwa hisia, lakini kwangu hakuna hata mmoja wenu aliyejenga hoja ya kunishawishi kuamini kuwa kwa waandishi kugomea habari za polisi ni jambo sahihi, nasikitika kusema hilo na msimamo wangu unabaki pale pale, kuwa ni mkakati wa kimakosa.

Sasa Maggid utashawishika vipi wakati hujibu post za wadau ambazo ziko against your idea? Umebaki tu kugonga kitufe cha like na kujibu comments ambazo zinakuunga mkono, tukuelewe vipi? Ni wazi kabisa hutaki kubadili msimamo kwa sababu zako binafsi.

Hivi unakumbuka tarehe 19/10/2008, rafiki yangu na Naibu Mhariri Mtendaji wa Tanzania daima,
Ansbert Ngurumo aliandika makala yenye kichwa kisemacho "Wananchi wamechoka, watawala wamekwisha" kwenye safu yake maarufu ya Maswali Magumu?. Unakumbuka ulikurupuka kutoka uvunguni na kuanza kuipotosha ile makala kwamba inachochea vurugu na uvunjifu wa amani kwenye gazeti la Raia Mwema. Unakumbuka?

Unakumbuka pia kwamba asingejitokeza
Ngurumo kukutetea kwenye Makala yake ya wiki iliyofuata iliyobeba kichwa cha habari "Hatuvunji nyumba, tunabomoa mlango" ya tarehe 26/10/2008 ulikuwa umepoteza imani ya wasomaji makini wa Makala nchini?

Rejea haya maneno machache aliyoandika
Ngurumo kwenye ile Makala. Nanukuu:
.. .... .... .... ..... .. ... ... .. ... ... .... .... ... ..... Bahati mbaya, wiki hii alipojitokeza rafiki yangu Maggid Mjengwa, akaandika makala ya kunikosoa katika gazeti linaloheshimika la Raia Mwema, baadhi ya wasomaji wa safu hii ya Maswali Magumu wamekosa uvumilivu, wakamsakama wakidhani naye yu miongoni mwa kundi lile chafu. ..................... ............ ........ ........ ......

Hiyo paragraph kwenye hiyo makala ndiyo iliyokuokoa kuondoka kwenye genge la kina Balile, Salva, etc. Maana tulikuwa tayari tumeshakujumlisha. Sasa leo umekuja tena na truck mpya. Kama umekubali kuharibu taaluma yako kwa pesa chafu endelea kivyako. Usiwalazimishe na wenzio wakufuate.

Nakala kwa:- nyabhingi, KIJOME, JB WISER, bambino, Chilipamwao, babuwaloliondo, Mungi, mchemsho, nyakato, STEIN, Molemo, Ng'wanangwa, Kimbunga, nk

TUMBIRI (PhD in Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form Six National Exams)
tumbiri@jamiiforums.com
 
Hivi kuna mtanzania ana kuwa na hamu ya kuangalia/kusoma habari za police, yaani kova kila baada ya mwezi au miezi lazima atokeee kwenye TV na bunduki kubwa akidai wamekamata jambazi!

Msipotoke, polisi kimsingi siyo source ya information za matukio, ila wao mara nyingi hujulishwa juu ya matukio na kuyatolea taarifa. Mkitaka kupata taarifa za uharifu kwanini msiende kwenye source ya tukio lenyewe? mara nyingi polisi wanakuwaga hawana detail zozote mpaka uchunguzi ufanyike kwa kuwahoji watu walewale ambao nyie waandindishi mngeweza kuwahoji kupata details za tukio. Kwa mfano mtu anakutwa amekufa na kutupwa polini, halafu polisi wanapewa taarifa na wapita njia, nyie waandishi mnawafuata polisi wa nini wakati mnaweza kufanya uchunguzi maeneo ya tukio kupata detail zaidi?

Sioni sababu za msingi za kuwasaliti wenzenu katika hili la kukataa kutoa taarifa za polisi kwa ajili ya kushinikiza polisi waheshimu haki za waandishi na raia.

Polisi wanatoa ufafanuzi juu ya matukio mbalimbali ya kihalifu na wanawatahadharisha wananchi na kuwaelimisha juu ya usalama wao. Taarifa hizo zote haziwezi kuwafikia raia kama waandishi wamegoma.

Hebu fikiria unasikia kuna matapeli au wauaji wanaibuka na kufanya uhalifi maeneo tofauti na nyakati tofauti kama mara 4 au 5, unategemea ni nani atatoa ufafanuzi juu ya hatua za tahadhari wananchi wanazopaswa kuchukua na hatua zilizohukuliwa kudhibiti huo uhalifu kam sio polisi?

Hivi isipotolewa taarifa yoyote haooni kuwa wananchi watakuwa kwenye hofu ya hali ya juu na sintofahamu?

Huo ni mfao mmoja tu wa atahri watakazopata wananchi kutokana na mgomo hou.
 
Sasa Maggid utashawishika vipi wakati hujibu post za wadau ambazo ziko against your idea? Umebaki tu kugonga kitufe cha like na kujibu comments ambazo zinakuunga mkono, tukuelewe vipi? Ni wazi kabisa hutaki kubadili msimamo kwa sababu zako binafsi.

Hivi unakumbuka tarehe 19/10/2008, rafiki yangu na Naibu Mhariri Mtendaji wa Tanzania daima,
Ansbert Ngurumo aliandika makala yenye kichwa kisemacho "Wananchi wamechoka, watawala wamekwisha" kwenye safu yake maarufu ya Maswali Magumu?. Unakumbuka ulikurupuka kutoka uvunguni na kuanza kuipotosha ile makala kwamba inachochea vurugu na uvunjifu wa amani kwenye gazeti la Raia Mwema. Unakumbuka?

Unakumbuka pia kwamba asingejitokeza
Ngurumo kukutetea kwenye Makala yake ya wiki iliyofuata iliyobeba kichwa cha habari "Hatuvunji nyumba, tunabomoa mlango" ya tarehe 26/10/2008 ulikuwa umepoteza imani ya wasomaji makini wa Makala nchini?

Rejea haya maneno machache aliyoandika
Ngurumo kwenye ile Makala. Nanukuu:

Hiyo paragraph kwenye hiyo makala ndiyo iliyokuokoa kuondoka kwenye genge la kina Balile, Salva, etc. Maana tulikuwa tayari tumeshakujumlisha. Sasa leo umekuja tena na truck mpya. Kama umekubali kuharibu taaluma yako kwa pesa chafu endelea kivyako. Usiwalazimishe na wenzio wakufuate.

Nakala kwa:- nyabhingi, KIJOME, JB WISER, bambino, Chilipamwao, babuwaloliondo, Mungi, mchemsho, nyakato, STEIN, Molemo, Ng'wanangwa, Kimbunga, nk

TUMBIRI (PhD in Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form Six National Exams)
tumbiri@jamiiforums.com

Umemaliza yote TUMBIRI huyu Maggid ni binadamu wa ajabu kuliko ajabu yenyewe, labda tu umesahau kumpa nakala Mzee Mwanakijiji.
 
Last edited by a moderator:
Bwana maggid nakuunga mkono na kutoa ushauri ili kuboresha kazi ya uandishi wa habari hasa kuhusu hawa mbwa mwitu wanaoitwa polisi, chonde chonde wanahabari andikeni habari zao kwa wingi zinazohusu ubaya wao tu mkiacha mazuri yote wanayofanya hapo mtakuwa mmewatendea haki watanzania kujua kwamba hawa jama ni sawa na mbwa wa kufugwa aliyekengeuka na kuanza kung'ata hata bwana wake.

POLISI TANGU SASA HAWANA TOFAUTI NA LUCIFER NA HAYAWANI KAMA NGURUWE NA FISI.
 
Last edited by a moderator:
Samahani lakini, sipendi kuwa personal katika kujadili issues, ila kwa hili naomba niulize: Hivi Mjengwa ulisomea wapi na kwa hatua(level)ipi uandishi wa habari?i.e. una diploma, una degree, cheti au ni wale waandishi wanaojigamba wameingia kwenye fani kwasababu ya kipaji(talent)?kutoka hapa ndipo tutaanza kujadiliana.Na-declare interest katika hili, mimi ni mwandishi wa habari (wa kusomea na ku-practice).
 
TUMBIRI (PhD in Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form Six National Exams)
tumbiri@jamiiforums.com


Du!!!! kama Idd Amini!!!
 
Kimsingi nakubaliana nawe. Mashambulizi hayo yatushirikishe sote. Linapotokea la uozo wa polisi tuwajulishe waandishi mara moja. Wekeni namba zenu hapa ili muwasulubu vilivyo. Muwasakame ili watoe wajibu.
 
Mkuu TUMBIRI kitu kingine ninachoipendea Jamiiforums ni kumbukumbu. Mtu akijichanganya tu historia inavutwa na kuwekwa hadharani.

Ukidhani kuwa ya mwaka 2008 yamesahaulika loooo umekosea jamaa wa JF wanaibuka na archieve na mambo yanakuwa hadharani. JF mtambo wa kurekebisha tabia.

JF ni tanuru - Regia Mtema (RIP)
 
Waandishi ni sawa na wauza nyanya huwezi kuahirisha kula kwa kukosa Kachumbari!
 
maggid mimi ni mtanzania niliyekupenda hasa makala zako za mwanzo.

Ila kila taifa letu lilipoonekana kuzama katika majanga makubwa ya umaskini unaotokana na watawala kunyang'anya maskini nilianza kuona kuunga kwako mkono mfumo huo. Sikuwa nimejua kama umeoa mzungu nilipoona hiyo nikajua labda ni wa mlengo huo sikuacha kusoma makala zako.

Taifa letu lilipoanza kukubwa na jinamizi la ukabila, ukanda na udini ulijipambanua wazi kuwa ni wa milengo ipi nalo si jambo baya lakini pale ambapo hayana maslahi kwa taifa ukajitambulisha kwayo hapo ndipo nilipoanza kutilia mashaka makala zako. Kwa sasa sina shaka kuwa sasa u wa mlengo huo maana wasaliti wengi hutumia mianya ya kusema wao wanataka kuwajua vema maadui wao kumbe ndo kumezwa nao.

Tunakutakia kila jema katika kuwaunga mkono mapolisi kwa silaha yako (kalamu) kuendelea kuwaua watanzania wasio na hatia na hata huyo Manumba amewahakikishieni kuwa mauaji ya Mwangosi hayatakuwa ya mwisho nawe wasema vema!!!! Huu ni usaliti...
 
Last edited by a moderator:
Asante sana! Hoja kubwa anayosimamia ndugu Mjengwa ni kuwa 'HABARI ZA KIPOLISI ZINAIHUSU JAMII'!

Zinaihusu jamii ndiyo maana zimegomewa.Ndo maana walimu wakigoma,wanaigomea serikali na si wanafunzi kama wengi wanavyoweza kudhani.Same thing with mgomo wa madaktari.

Tumia akili ndugu Maggid,ndo maana watu wanaona uko kimaslahi binafsi tu.
 
Na Maggid Mjengwa,

HUWEZI kutawala miili ya watu ukaacha mioyo yao. Ndiyo, mjumbe hauawi, ni kauli ya hekima ya tangu enzi za wahenga wetu.

Mwandishi wa habari na Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa Habari mkoani Iringa, Daud Mwangosi ameuawa. Polisi wanatuhumiwa kuhusika na mauaji hayo.

Jumapili ya Septemba 2, 2012 itabaki katika kumbukumbu za Watanzania kwa mamilioni kwa kufikiwa na taarifa za kutisha za mauaji ya mwandishi wa habari. Haya yanaingia katika historia kuwa ni mauaji ya kwanza kwa mwandishi wa habari kufanyika hadharani tangu nchi hii ipate Uhuru.

Wengi watakuja kukumbuka walikuwa wapi na walifanya nini siku walipopata taarifa hizo za kutisha. Binafsi, taarifa ile ya mauaji ya Daud Mwangosi siku ile ya Jumapili ya huzuni kwa Taifa ilinikuta nikiwa Iringa, umbali wa mwendo wa saa moja kwa gari kufika eneo la tukio, Nyololo, Mufindi.

Jioni ile nilikuwa nikifundisha soka ya watoto. Mara baada ya kupata taarifa zile kwa simu, nilisitisha mazoezi yale ya watoto. Nikawapa taarifa zile. Nilipowaambia kuwa nimepata taarifa sasa hivi kuwa mwandishi wa habari ameuawa Mafinga, mtoto mmoja akaniangalia na kuniuliza; " Kwanini?"

Ndiyo, swali la mtoto yule ndilo umma wa Watanzania unapaswa kujiuliza sasa; KWA NINI?

Mwandishi wa habari ni mjumbe katika jamii. Anapokuwa akifanya kazi yake hapaswi kuwa na hofu ya kudhuriwa kwa kukusudia na waliopata mafunzo ya kutumia silaha. Ndivyo ilivyo kwa watumishi wa Msalaba Mwekundu, wanapokuwa kazini kwenye maeneo hata ya vita.

Askari asiyejua kutofautisha kati ya mwanahabari aliyeshika kamera, mtu wa Msalaba Mwekundu aliyeshika mkoba wa Huduma ya Kwanza na raia anayefanya vurugu au adui aliyeshika silaha vitani, huyo hawezi kuwa ni askari makini.

Polisi katika nchi ni moja ya viungo muhimu vya dola kuu. Polisi ni mkono mrefu wa dola ( State's extended arm). Inapofika mahali, mkono huu muhimu unapoonyesha udhaifu wa ndani katika mfumo wa utendaji kazi wake, basi, umma nao unakosa imani na mkono huu mrefu. Ndipo hata raia wa kawaida niliyemsikia kwenye runinga ya ITV akitamka; " Kama polisi si makini, basi ni heri wasiwepo watuache wenyewe tuendeshe mambo yetu, maana sisi wananchi tunaishi kwa amani na utulivu".

Kauli kama hizi ni kiashiria cha umma unaopungukiwa imani na dola na viungo vyake, ikiwamo polisi. Hili haliwezi kuwa jambo jema.

Na hakika, kama Taifa, tunafanya makosa kuamini, kuwa nchi yetu ni ya amani kwa vile wananchi wetu hawagombani.

Kama watu hawagombani basi maana yake ni nchi ina amani yaweza kuwa tafsiri potofu ya maana nzima ya amani. Maana, kama watu hawagombani mahali pasipo na haki, usawa na uadilifu wa viongozi; mahali palipojaa dhuluma,unyanyasaji na maovu mengine wanayotendewa au wanaotendeana wanajamii, basi, amani hiyo itakuwa ni ya muda tu.

Maana, kwa watu wenye kuishi kwenye mazingira hayo bila kugombana wala kutokea uvunjifu wa amani, hiyo itakuwa na maana ifuatayo; ama watu hao hawaelewi kuwa wanaishi katika mazingira hayo ya dhuluma na maovu mengine wanayotendewa au kutendeana, au wamejawa na hofu.

Hivyo basi, kwa hilo la mwisho, itakuwa ni amani iliyojengeka katika misingi ya hofu. Na hofu hiyo haiwezi kuwa ya kudumu. Kuna siku mwanadamu hufikia ukomo wa kuhofia. Ukimwandama sana mjusi, mwisho hugeuka nyoka! Ndipo hapo tunapoona nchi zinalipuka na watu kuchinjana.

Tumefika mahali hata wawakilishi wa wananchi kwa maana ya wabunge , wanatiwa mbaroni na polisi katika mazingira ya kudhalilisha, tulishuhudia hili likimtokea Mbunge wa Viti Maalumu, CUF, Tabora Mjini. Mbunge ni mwakilishi wa wananchi. Mbunge ni mjumbe aliyetumwa na wananchi. Ana kinga ya kikatiba.

Kwa polisi kumdhalilisha mjumbe wa wananchi ina maana pia ya kuwadhalilisha waliomtuma. Haya ni matendo ya aibu.

Kilichomtokea mwandishi Daud Mwangosi ni aibu pia ya Taifa hata kimataifa. Kupunguza aibu hii ni kufanyika kwa uchunguzi huru, na kwa wote watakaobainika kuhusika na aibu hii wachukuliwe hatua za kisheria. Na wenye kustahili kuwajibika wawajibike kulinda heshima ya serikali iliyo madarakani.

Hii ni nchi yetu. Katika tofauti zetu hizi za kiitikadi tusifike mahali tukashindwa kuongea kama Watanzania kwa kutanguliza maslahi ya Tanzania. Kuna umma uliopo na unaokuja. Umma unaotegemea sana busara katika uongozi wetu.

Tuanze sasa kujenga utamaduni wa kuitumikia nchi yetu kwa kufanya na kuamua yale yenye maslahi kwa Tanzania. Hivi vyama vya siasa vipo leo na kesho havipo. Vinakuja na kuondoka, lakini Tanzania kama nchi itakuwapo daima.

Tusifike mahali tukabaki tunawaangalia wanasiasa wetu, kwa maslahi yao binafsi, ya makundi yao na vyama vyao, wakashinikiza au kuelekeza yale yenye kuchochea machafuko makubwa ya kijamii. Ni wajibu wa viongozi wa kisiasa kutanguliza busara katika kila maamuzi wayafanyao.

Na tunafanyaje pale tunapowaona viongozi wa kisiasa na watendaji wakifanya maamuzi yasiyo na busara na kusababisha Watanzania wenzetu kupoteza uhai na hata kuchochea machafuko?

Jibu; Kama Watanzania wazawa na wazalendo wa nchi hii, tuna wajibu wa kuyalaani matendo yao maovu.

Na katika nchi zetu hizi, ni kazi rahisi sana kuanzisha vurugu na kujenga mazingira ya chuki na uhasama, lakini ni kazi kubwa sana kumaliza vurugu na kuondosha mazingira hayo ya chuki na uhasama. Na nchi yetu kamwe haiwezi kupiga hatua za maana za maendeleo katikati ya mazingira ya vurugu, chuki na uhasama, uwe wa vyama vya siasa au wanajamii.

Kihistoria, Watanzania tumeishi kwa amani na upendo bila kuwa na chuki na uhasama miongoni mwetu unaotokana na tofauti zetu za kidini na kikabila. Tunaziona sasa, dalili za baadhi ya wanasiasa, kwa malengo ya kisiasa, kutaka kupandikiza miongoni mwetu uhasama na chuki kwa kutumia tofauti zetu za kidini na kikabila, tofauti zetu za kiitikadi. Wanafanya hivyo mara ile wanaposhindwa kujenga hoja za kisiasa kwenye majukwaa ya kisiasa. Hawa ni watu hatari sana kwa maslahi ya taifa letu.

Katika nchi zetu hizi, ni wanasiasa wa aina hii ambao, katika kufanikisha malengo yao, huwa tayari hata kuwalipa vijana wasio na ajira na kuwavutisha bangi ili washiriki vurugu za kisiasa, kidini na kikabila. Tumeyaona hayo Liberia, Ivory Coast na hata katika nchi jirani na kwetu.

Tusipokuwa makini, yako karibu kupisha hodi kwenye nchi yetu, kama si tayari kuwa yameshaingia ndani ya nchi yetu.

Hii ni nchi yetu. Tutafanya makosa makubwa kuwaachia viongozi wa kisiasa pekee, jukumu la kulinda maslahi ya nchi yetu. Tunapita sasa katika kipindi kigumu tangu tupate Uhuru.

Dunia imebadilika, na nchi yetu inapitia kwenye kipindi cha mabadiliko. Hakuna mtu au chama cha siasa kinachoweza kuyazuia mabadiliko haya. Kufanya hivyo ni kutuletea machafuko na kuvunja amani yetu. Tuna jukumu la kufanya tunayoweza, na kwa kutanguliza busara, kuipitisha salama nchi yetu katika kipindi hiki cha mabadiliko.

Maana, tukiingia kwenye machafuko, basi, hakutakuwa na mshindi, maana, sote tutashindwa.

Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika.
 
Maggid msimamo wako nauunga mkono kwasababu kususia kuandika habari za polisi ni adhabu kwa raia wasio na hatia.
Mi nadhani busara ni kuandika zaidi polisi hasa pale wanapokosea ili wabadilike.

Kuwasusia kunaweza kuwapa nafasi ya kufanya madudu zaidi kwakuwa hakuna atakaye jua.
Pia umeonyesha ujasiri kwa kutafakari uamuzi wa wanahabari wenzako na kuwa na msimamo tofauti wa kufanya kile unachoamini ni sahihi. Watanzania wengi tmezoea kufuata mkumbo bila kutafakari.

Naomba hao wanaosusia polisi watuambie faida anazopata mtanzania wa kawaida kutokana na mgomo wao. Mi si mtaalam ila sidhani kama kuna kipengele katika maadili ya uandishi wa habari kinacho wafundisha kugoma.
Faida wanazopata wagonjwa madaktari wakigoma ni zipi?
 
Kuna vyombo vya habari na waandishi wa habari. Bahati nzuri waandishi wengi wa habari ni free lance wanaishi kwa kuuza habari katika vyombo vya habari.

Polisi walikuwa wanazungumza na waandishi wa habari ili habari hizo ziwafikie wananchi kwa kupitia vyombo vingi vya habari kwa gharama nafuu, hata hivyo jeshi la polisi linaweza kupeleka habari muhimu kwenye vyombo vya habari kama matangazo, tangazo ktk ukurasa mmoja ni mamilioni ya pesa, je ni mhariri gani atasusia kupokea matangazo toka polisi kwa kuwa wanahabari wamegoma?

Hali kadhalika kuna magazeti ya serikali au vyombo vya habari vya serikali, mwandishi aliyeajiriwa akitumwa na mwajiri wake aende kwa RPC, au OCD atagoma? Hataki kazi?

Nadhani mgomo huu unawahusu zaidi freelancer. Waandishi wangekuwa specific kwa mathalan RPC wa Iringa, au Morogoro, au Ruvuma au Arusha ingeeleweka lakini mmmm..haya..!!!
 
Back
Top Bottom