Waandishi Kugomea Habari Za Kipolisi; Naomba Nichangie Haya...

Asante sana! Hoja kubwa anayosimamia ndugu Mjengwa ni kuwa 'HABARI ZA KIPOLISI ZINAIHUSU JAMII'!
Waandishi mnaogoma kuandika habari zinazohusu jeshi la polisi mtameza matapishi yenu. Mngesema hivi" WAANDISHI KUGOMA KUANDIKA HABARI ZA IGP SAID MWEMA" ningewaelewa na ningewaunga mkono.

Kwa mfano kituo cha Chanel 10, radio Country, Ebony FM, nk vikipata matatizo ama ya kuibiwa au kuunguliwa moto taarifa zao watapeleka wapi? Waandishi wakumbuke Godwin alipopigwa na kijana mdogo Diamond Platnum pale uwanja wa Samora Iringa ni polisi ndio waliomsaidia, Mwandishi Maregesi Gilshon alipopata ajali ya gari ni polisi haohao waliomsaidia.

BUSARA ITUMIKE WAANDISHI MSIPEWE MANENO. AJALI IKITOKEA POLISI WATAFIKISHAJE TAARIFA KWA NDUGU WA MAJERUHI. HAO MAITI TAARIFA ZAKE TUTAZIPATAJE?USITUKANE UKUNGA NA UZAZI UNGALIPO.
 
Asante sana! Hoja kubwa anayosimamia ndugu Mjengwa ni kuwa 'HABARI ZA KIPOLISI ZINAIHUSU JAMII'!

Ntaramuka,

Tuko pamoja, na kuthibitisha nguvu ya hoja hiyo ni ukweli kuwa hata muda huu tupo tunajadili habari za kipolisi. Na magazeti mengi ya leo yamepamba sura za pembele na habari za kipolisi (fanya utafiti wako utathibitisha).

Kimsingi jamii kwa sasa ina kiu zaidi ya kuzipata hizo 'habari za kipolisi' kutoka kwa wanahabari kwa vilw jamii inautafuta ukweli na kazi ya mwanahabari ni kuusaka ukweli.

Na mwandishi yeyote anarudi chumba cha habari kwa mhariri wake akiwa na 'Habari ya kipolisi' kuhusiana na kilichotokea Nyololo, basi ana nafasi kubwa ya kuvuta attention ya mhariri wake. Kimsingi habari ya kipolisi inaihusu jamii labda kama ni inahusu harusi za maafande wa polisi!
 
U DC????????????????????????/// jinamizi hili litakutesa mjengwa,,,,, if not for decades then generations.
 
mkuu nimeshasoma blogini, hapa hata sina haja ya kusoma.

lakini nadhani hauko sahihi, na siku moja utahukumiwa kwa haya.

hajui kesho aweza kuwa yeye...yaani yuko kinyume na mashirikisho yote ya habari, lazima kuna kitu hapa..tusubiri tuone
 
Njaa zako hizo!

Hapa wanachotaka wenzako ni kugoma kutoa taarifa zo zote ambazo polisi wanataka au wangependa wananchi wazipate na si habari ambazo polisi wametenda na wanataka kupotosha ukweli!

haswa hii ndio dhamira ya waandishi na sivyo kama wewe maggid unavyotaka kutuaminisha kwenye huu izi wako, tafakari hapa kuna great thinkers hatuingii kichaka tusichokijua
 
maggid,
Bahasha zitawagawa sana wanahabari! Kuendelea kutoa ushirikiano na jeshi la polisi ni sawa na kukubali kitendo alichofanyiwa mwenzenu. Wewe unasema kuna njia za kushambulia jeshi la polisi tofauti na kugomea kutoa habari zao, bahati mbaya unashindwa kusema hata njia moja ya kuishambulia. Mkuu Pasco na wewe ni kama maggid?
 
Last edited by a moderator:
Huyu ni mwandishi mmoja kati ya waandishi wote, na nadhani waandishi walikaa na kukubaliana kabla ya kufanya maamuzi sasa kama alikuwepo na akatofautiana na wenzake kwenye kikao kama ambavyo anasema sasa analalamika nini???, nadhani wengi tuwape. Issue kubwa hapa ni kuwaonyesha IGP, RPC na wengine kuwa waandishi hawakubaliani na jinsi mambo yanavyopelekwa ndani ya Jeshi la polisi.

Kikubwa ni ukandamizaji na unyama uliopitiliza, hivi huyu mjengwa angekuwa ni yeye au ndugu yake au mkewe kafanyiwa vile alafu zinatangazwa propaganda kuwa ni CDM ndiyo ilihusika na kifo cha mwandishi angejisikiaje????

Hawa ni miongoni mwa waandishi wanaoamini huu ni upepo tu na utapita...

Mimi namheshimu sana Mjengwa lakini kwa hili natofautiana sana... Mimi nafikiri wangeacha kabisa kuandika habari za serikali nzima pamoja na CCM maana ndiyo wanaobenefit na haya mauaji.

poleni sana waandishi kwani nyinyi ndiyo mnaojua ukweli....
 
Unafiki ni dhambi mbaya.Huwa adhabu sahihi kwa wasaliti ni kuuawa hata kama ni kwenye jeshi lolote duniani.Kwa ujinga kama huu wanahabari katu hawatapata haki yao.
 
Hizi ni zama za demokrasia, una uhuru wa kujiamulia ila tu usivunje sheria halali. Ninachokushauri ni kwamba, uwe na tahadhari, isije wenzio wakakuona kama msaliti. kumbuka hawa ni wenzio ktk tasnia ya habari. na uje hii serikali ya ccm ni watu ambao wamedhihirika kuwatumia watu na kisha kuwatosa hasa pale wanapoona huna tena maana kwao, wakati huo ukifika watakuwa waandishi wenzio ambao leo unawageuka ndo watakaokufariji.

Kumbuka D. Mwangosi alikuwa wakala wa chanel 10, kituo ambacho polisi wanatangazia kipindi cha POLISI NA JAMII, lakini hawakujali hilo, WAMEMUUA KINYAMA KWA KUMSAMBARATISHA UTUMBO WAKE KANA KWAMBA WALIKUWA WANAMSHAMBULIA MNYAMA KIBOKO.

INASIKITISHA SANA, HATA JAMBAZI SUGU HAJAWAHI KUULIWA KIFO CHA KINYAMA NAMNA HII.


Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili waling'oe madarakani hili li serikali la ccm MAONGO/MAFISADI/MAJAMBAZI/WAUAJI.
 
maggid

Nimeona nikisoma thread za watu wengine naweza kuwa na mtizamo tofauti, nitoe mawazo yangu kwanza kisha nitasoma wengine nao wamesema nini.

Bwana Majid, kwa serikali inayoogopa wananchi wake pamoja na kuheshimu sheria na haki za binadamu, uelekeo wako ni mzuri na ungepaswa kufuatwa na kila mwandishi wa habari na kweli tungefikia pazuri. LAKINI, kwa serikali tuliyonayo, nikuhakikishie kuwa kwa nguvu zote kwa sasa wanawalilia watu wenye mlengo kama wako, ni lini serikali hii imewajibika ipasavyo katika matukio ambayo imehusika?.

1) Suala la Ulimboka pamoja na nyinyi kutaka jamii ipewe majibu, wewe kama Majid umepata majibu gani,
2) Suala la mauaji ya Arusha mpaka sasa umepata majibu gani mimi kama mwanajamii nione huo mwelekeo wako kuwa ni sahihi kwa serikali hii,
3) Suala la Morogoro, wewe kama Majid umeiona hiyo taarifa ya Daktari aliyemfanyia postmortem na kuweka kwenye blog yako ni kuuliza maswali magumu ambayo sisi unaotuita wananchi tunastahili kupata taarifa na ufafanuzi huo;
4) Mzaha wa Waziri wa Mambo ya Ndani kumteua Jaji mstaafu ambaye tayari wananchi walishafahamishwa kuwa uwezo wake ni mdogo na hivyo lazima atakuwa amejenga chuki na waliomuanika unafikiri atamtendea haki nani, aliyemteua kwa sasa apate pesa au sisi walalahoi?,

Kwa kuwa umekuja hapa jamvini, nitapenda na kushukuru iwapo utanihakikishia kuwa serikali iliyohusika na mambo hayo manne na mengine mengi yakiwemo ya ufisadi imebadilika na tumechagua viongozi waadilifu wanaoogopa kalamu ya majid, tufanye kama msimamo wako, kama sivyo basi, chonde chonde acha kuandika habari zao kama wenzako walivyokubaliana.

uhuru wa kuamua na kutetea maslahi ni wa mtu binafsi, ukiona maslahi yako yatapotea, nakushauri uendelee na msimamo wako.
 
Last edited by a moderator:
Ni vizuri kama wanahabari wakatumia silaha walio nayo dhidi ya Polisi wenye silaha ambao wamekuwa hawana tofauti na utawala wa makaburu wa Afrika ya Kusini..

Mjengwa unaweza kuwa na mawazo yako binafci au mawazo ambayo yamekuwa influenced na sababu nyingine bt all in all kama wengi wameona hiyo ndio njia ya kuonyesha hacira zao ulitakiwa uwa-support maana maamuzi ya wengi ndo sheria hiyo..

Hii unayotoa sasa ni kuonyesha utakwenda njia tofauti na wao ni usaliti kwa Marehemu pamoja na familia yake.. Vile vile ni usaliti kwa jumuia yote ya waandishi wa habari.. Kumbuka mnahitajiana each other Broda..
 
ENYI WANAHABARI WA TAIFA LETU HAYATI DAUDI MWANGOSI (KEN SAROWIWA NA MOHAMED AMIN WA TANZANIA) ANAHITAJI MCHANGO WAKO KUSHITIRI FAMILIA YAKE KUPATA HAKI STAHIKI KUTOKANA NA MSHIKAMANO WENU TANGU LEO

Enyi Wana-CCM na mbinu hizi za danganya to za mwaka wa 47, nasema WaTanzania wa leo HATUDANGANYIKI kitu hapa hata tone!!!!!!!!!!!

Eti tu kwa sababu wakubwa wa dunia walipiga simu Magogoni wakihoji juu ya hili sasa ndio muibuke na hizi ngonjera za siku zote kama kawaida kutafuta kuokolea ufadhili usikatwe??????????

Mambo hapa mpaka tume huru kumhoji Mzee Wasira, Nchimbi, Saed Mwema na Kamuhanda kabla ya kumfikia hicho kidagaa kilichoamrishwa tu kutekeleza amri na kwamba kama kuna maswali eti anaweza tu kuuliza mara baada ya kuchukua roho kwanza kijana mwenzetu Mwangosi.

Meanwhile, vyombo vyetu vya habari yafaa kuonyesha mshikamano kama ule wa wakati ule dhidi ya Magereza kukata kushiriki wala kushirikishwa habari zozote za jeshi la polisi mpaka siku watoto yatima na mjane wa Daudi Mwangosi atakapotendewa haki na kuonekana na kuhisiwa kwamba kweli hapa kuna haki imetendeka.

Kumbukeni leo kaondoka Mwangosi kwa njia hii mkononi mwa CCM na kesho hatujui ni zamu ya naani kwa mikono ya hii serikali dhalimu katika historia ya taifaa hili.

Na enyi ndugu zetu wamiliki wa vyombo vya habari na wanahabari wote, ukweli wa mambo ni kwamba fadhila pekee unayoweza kumfanyia Mwangosi hadi hivi sasa akiwa amelala kule kijijini kwao Itete ni kule tu kushinikiza kwa nguvu zote ili mjane wake na wale mayatima wa kuchongewa na CCM wapate haki wasiishie kuwa omba omba na kudhalilika katika maisha haya.

Hapo ndiyo litakapozimwa jambo hili la kuuzunisha. Wakati watawala (Serikali na viongozi wa CCM) wakiwatupia lawama mojakwamoja vyama vya upinzani, pasi tusitegemee jipya hapo.

naona unalilia ubunge wa viti maalumu kama mbatia... keep it up mnafiki na msaliti wa wanahabari wenzako....
 
Ndugu maggid,

Wazo lako linaweza kuwa zuri ila sina hakika kama umepima upepo na kujihakikishia kuwa umelileta katika wakati muafaka.

Jambo ambalo nimejiuliza sana ila sipati majibu, labda nitapewa msaada, ni ujumbe unaotumwa kwa ndugu na jamaa za marehemu wakati huu wanapozidi kupitia mateso makubwa sana. Wameshuhudia unyama mkubwa baada ya kumpoteza ndugu yao aliyeteuawa kama mnyama pori (tena wa hatari sana). Na tukio lenyewe lilitendwa na watu waliotakiwa kumlida na kumhakikishia usalama wake. Nadhani kwa sasa ndugu wa marehemu wanahitaji kauli za kuwafariji na pia kuwaonesha kuwa sisi kama jamii na wanahabri waliokuwa karibu na marehemu wameguswa sana na tukio hili. Na pia jeshi la polisi linabanwa ili lichukue hatua kwa ajili ya kutenda haki, kwa kuwashughulikia watu wote waliomuua marehemu Mwangosi.

Sina hakika kati ya msimamo wa Maggid na ule wa wanahabari wengine upi unapeleka ujumbe huo.

Maggid unaonaje??
 
Last edited by a moderator:
Baada ya kusoma thread za wengine pia, nimegundua kiasi kikubwa ambacho maggid unataka kuturubuni kwa kutumia maneno matamu kuwa kususia kuandika taarifa za polisi ni kujimaliza wenyewe, kama nimesoma vizuri wanzako walikubaliana kuwa kuandika taarifa zinazohusu polisi kwa mfano kujisafisha, kutoa maelekezo yoyote yanayowahusu wao ni Marufuku, lakini ikitokea IGP kajisaidia pale Posta, basi waandishi wote wamwandike, hilo ndilo lililokubaliwa. Baada ya hayo, kwa heshima kubwa naomba ujibu hoja zangu kwenye post iliyopita.

There are currently 77 users browsing this thread. (23 members and 54 guests)
 
Last edited by a moderator:
Ndugu Maggid,

Wazo lako linaweza kuwa zuri ila sina hakika kama umepima upepo na kujihakikishia kuwa umelileta katika wakati muafaka.

Jambo ambalo nimejiuliza sana ila sipati majibu, labda nitapewa msaada, ni ujumbe unaotumwa kwa ndugu na jamaa za marehemu wakati huu wanapozidi kupitia mateso makubwa sana. Wameshuhudia unyama mkubwa baada ya kumpoteza ndugu yao aliyeteuawa kama mnyama pori (tena wa hatari sana). Na tukio lenyewe lilitendwa na watu waliotakiwa kumlida na kumhakikishia usalama wake. Nadhani kwa sasa ndugu wa marehemu wanahitaji kauli za kuwafariji na pia kuwaonesha kuwa sisi kama jamii na wanahabri waliokuwa karibu na marehemu wameguswa sana na tukio hili. Na pia jeshi la polisi linabanwa ili lichukue hatua kwa ajili ya kutenda haki, kwa kuwashughulikia watu wote waliomuua marehemu Mwangosi.

Sina hakika kati ya msimamo wa Maggid na ule wa wanahabari wengine upi unapeleka ujumbe huo.

Maggid unaonaje??
 
inabidi aangali na afikirie mbali zaidi chukulia ungekuwa ni wewe umetendewa unyamaa huu na uko ahela ungefikiriaje kuona wanahabari wenzako wanaendelea kulipoti taarifa za wauaji wako? fikiria sana tena kwa mapana zaidi
 
maggid

OK I GIVE YOU THIS ONE... I CRITICIZE YOU IT WILL NOT HAPPEN... NOW IT HAPPENED...

Uhasama wa polisi, waandishi wa habari waanza

ALHAMISI, SEPTEMBA 06, 2012 06:24 NA WAANDISHI WETU, IRINGA NA DAR

*Waandishi wa habari wasusa mkutano wa DC Manumba
*Wamtaka awaondoe kwenye kikao maofisa wa Polisi Iringa
*Yeye akataa, asema masharti hayo kamwe hawezi kuyafanya
*Tendwa atangaza kufuta vyama vya siasa vinavyosababisha mauaji
WAANDISHI wa Habari mkoani Iringa, jana walionyesha hasira zao mbele ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, baada ya kususa mkutano wake.

Pamoja na kususa mkutano huo uliokuwa ufanyike Mjini Iringa, katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa jana, waandishi hao wa habari walikataa kupokea taarifa ya awali ya uchunguzi ya mauaji ya Mwandishi wa Habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi, aliyefariki mwanzoni mwa wiki, baada ya kuuawa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu.
Pamoja na kuonyesha hasira zao kutokana na kifo cha Mwangosi, waandishi hao walionyesha kutoridhishwa na taarifa za Jeshi la Polisi kuwasaka waandishi wa habari watatu mkoani humo.

Kabla mkutano na waandishi hao haujavunjika, DCI Manumba, alianza kukanusha taarifa zinazodai kuwepo kwa waandishi wa habari watatu kusakwa na Jeshi la Polisi ili wauawe, baada ya mmoja wa wanahabari hao Francis Godwin, kumhoji sababu za kutakiwa ajisalimishe polisi.

Katika kikao hicho ambacho kiliitishwa saa sita mchana, wanahabari hao walisema hawatakuwa tayari kupokea taarifa yoyote kutoka kwa DCI Manumba, kama maofisa wa polisi wanaofanya kazi mkoani hapo, wataruhusiwa kushiriki mkutano huo.

"Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Iringa, walikwishatangaza katika tamko lao, kwamba wamesitisha ushirikiano wa kihabari na Jeshi la Polisi mkoani hapa, mpaka pale tume huru zilizoundwa kuchunguza kifo cha mwanahabari aliyeuawa zitakapotoa majibu yao," alisema Frank Leonard ambaye ni Katibu Mtendaji wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC).

Katika mkutano huo, Leonard alimwambia DCI Manumba, kwamba waandishi wa habari hawana tatizo lolote na yeye na kwamba wapo tayari kupokea taarifa yake hiyo ya uchunguzi, ila kwa sharti la kuwataka maofisa wa polisi wote wanaofanya kazi mkoani hapa kutoka nje ya ukumbi wa mikutano.

"Huu ndio msimamo wetu, hatupo tayari kufanya kazi na maofisa wa jeshi lako na tunamuomba IGP Said Mwema, ampumzishe kazi kwa muda Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda mpaka pale tume huru zilizoundwa zitakapotoa taarifa za matokeo ya uchunguzi wao," alisema Leonard.

Baada ya DCI Manumba kuona upepo unavuma vibaya, aliwasihi wanahabari hao kuendelea kushirikiana na jeshi hilo, kwani tayari tume imeshaundwa kuweza kufanya uchunguzi wa jambo hilo.

"Leo nilikuwa nataka niwape taarifa ya uchunguzi wa awali juu ya mauaji hayo, lakini kwa sharti mnalonipa sidhani kama hilo litawezekana," alisema DCI Manumba.

Akitoa ufafanuzi, ofisa huyo wa polisi alisema kila mtu ameguswa na mauaji ya mwandishi huyo na kwamba kosa lililofanywa na wahusika haliwezi kuwa kosa la kila mtu.

Bila kufafanua, alisema matukio ya aina hiyo yapo katika jamii yetu na yanaweza kuendelea kutokea ikiwa ni pamoja na kwake au maofisa wengine wa jeshi hilo.

"Jambo hili baya limetokea na sisi polisi tuna majuto pamoja na Serikali, ndiyo maana tume imeundwa na mara moja tukakimbia kuja hapa, ili kupata ukweli baada ya kupeleleza na tukaona ni vizuri uchunguzi tuliofanya tuutoe kwenu.

"Hata hivyo, kwa kuwa huu ni msimamo wa waandishi na wote mmeuunga mkono mbele yangu, nadhani uchunguzi uliofanywa na jeshi letu, itabidi upitiwe na tume nyingine badala ya kuutoa kwenu," alisema DCI Manumba.

Alisema pia kwamba, tume iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, inatakiwa iachwe ifanye kazi yake kwa hiyo itapata fursa pia ya kupitia uchunguzi wao huo.

Kuhusu kuwepo kwa taarifa ya orodha ya waandishi wa habari wengine watatu wanaotakiwa kushughulikiwa na jeshi hilo, alisema taarifa hizo hazina ukweli, kwani mbali na kufanya kazi na wadau wengine, jeshi hilo linawategemea sana wana habari katika kazi zake.

"Kwa hiyo, ndugu zangu mkutano umefungwa na sasa tuiache tume ifanye kazi yake," alisema.

Pamoja na kutoa maelezo hayo, waandishi hao wa habari waliendelea na msimamo wao, kwamba hawako tayari kumsikiliza ofisa huyo wa polisi.

"Pamoja na majibu haya, lakini bado hatuna haja ya kuendelea kukusikiliza na ili kuwepo usawa ndani ya tume hiyo, ni lazima Waziri Nchimbi, amuongeze mwanachama wetu mmoja kutoka UTPC awepo katika tume hii," alisema Leonard.

TUCTA yataka uchunguzi huru

Wakati hayo yakiendelea, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limetoa onyo na kuwataka wanasiasa wote nchini kuwa makini na kuhakikisha wanashirikiana kwa karibu na walinzi wa usalama kwenye harakati zao za kisiasa, ili kuepusha vurugu zinazoweza kutokea.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA, Hezron Kaaya, alisema TUCTA imepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwangosi.

"Kama kweli Jeshi la Polisi limediriki kufanya mauaji hayo kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari, basi linaipeleka nchi pabaya, kwani tabia hii kamwe haiwezi kuvumilika," alisema Kaaya.

Alisema pia kwamba, Jeshi la Polisi kama litaendelea na tabia hii, litaiweka nchi katika mazingira magumu, kwani matukio mengi yanayoonekana ni madogo baadaye yanaweza kusababisha machafuko makubwa.

Kaaya alisema, mambo kama hayo yamezoeleka kusikika na kuonekana yakitokea katika nchi mbalimbali duniani na kwamba TUCTA haitopenda kuona nchi inafika huko.

"TUCTA ingependa kuona hatua kali zinachukuliwa kwa upande wowote utakaoonekana kuhusika na kifo cha mwandishi huyo, ikiwa ni pamoja na kuwajibishwa kwa jukumu la kulipa fidia kwa familia ya marehemu," alisema Kaaya.


TCJ yalaani

Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari wa Kujitegemea Tanzania (TCJ) Mobini Sarya, amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mwangosi.

Sarya alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Tendwa atangaza kufuta vyama

Wakati huo huo, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, amesema atavifuta vyama vya siasa vinavyokiuka maadili na kusababisha mauaji ya raia wasio na hatia.

Tendwa alitoa onyo hilo Dar es Salaam jana mbele ya waandishi wa habari kuhusu mpango wa ofisi yake kuvifuta vyama vinavyofanya fujo.

Bila kutaja ni vyama gani atakavyovifuta, alisema kutokana na mauaji yanayoendelea kutokea kwenye shughuli za kisiasa, hatasita kuvifuta vyama hivyo kwa maslahi ya taifa.

Alisema vyama vya siasa vimejisahau na kusababisha mauaji ya raia wasio na hatia na kujenga picha mbaya kwa jamii kwa kuonekana kama majambazi.

"Sitasita kukifuta chama chochote ambacho kinaenda kinyume na maadili, kwani mamlaka ya kufuta chama ninayo, sheria inasema kuwa, kama chama chochote kinavunja maadili, kinatakiwa kifutwe ili nchi iwe na amani.


"Hatutaki mauaji ya waandishi wa habari na raia yaendelee kutokea nchini, kwa kusababishwa na mikutano ya wanasiasa, hatuwezi kusema nchi yetu ina amani kwani tunashuhudia vifo vinavyotokea nchini kutokana na siasa, nakataa kabisa mambo ambayo yanafanywa na wanasiasa, mikutano yao iwe ya amani na furaha sio vifo," alisema Tendwa.

Aliongeza kwamba, tume zinazoendelea kuundwa nchini baada ya kutokea madhara ya vifo, haziihakikishii jamii na kuweka wazi mambo yanayotokea.

Wakati huo huo, alisema Jeshi la Polisi nchini, linatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ikiwemo kulinda raia na mali zao, kwani tangu mwaka jana matukio ya mauaji yamekuwa mengi.

Habari hii imeandaliwa na Sebastian Mparazo, Oliver Osward, Ruth Mnkeni na Adelina Rutale, Maneno Selanyika, Dar es Salaam na Oliver Richard Iringa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom