"Waamuzi wa Azam na mtibwa waondolewa kuchezesha mpira"

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
Habari za hivi punde kutoka tff zinasema kwamba waamuzi wa mechi ya Azam na Mtibwa iliyovunjika wameondolewa kwenye list ya waamuzi wa tff.Lakini pia kamati ya nidhamu imeipa Azam point3 na magoli3,pia imeipiga faini mtibwa sugar kwa kutia mpira kwapani.
Chanzo radio uhuru kipindi cha michezo.
 
Hapo ndipo TFF wanapojichanganya! Unatoaje adhabu mbili kwa Mtibwa (Fine na kunyang'anywa point) wakati huo huo unawaadhibu waamuzi (kwa kutomudu mchezo)?

......hovyo kbs!
 
Mimi nawakubali Azam kwa mipango yao. Shida yao ni moja tu wanatumia sana pesa kuhonga waamuzi. Mechi zao zote ni utata tupu.
 
Kwangu mimi mechi hii ingerudiwa ndo ningeona TFF wametenda haki, maana hawa jamaa wanajifanya wanatumia kanuni halafu wanashindwa kuzifuata sijui kwa nini, kanuni inasema refa atasubiri hadi dakika kumi na tano ndo avunje pambano, nini kilimfanya asisubiri hadi huo muda na je labda Mtibwa walikuwa wanashauriana halafu warudi na kanuni pia inasema kama timu itasababisha vurugu na pambano kutoendelea timu hiyo itapoteza pambano na itakuwa imefungwa magoli matatu pamoja na kushushwa daraja, kama kweli waliona Mtibwa wana makosa kwa nini hawajawashusha daraja?
 
Nakuunga_Mkono
 
Azam wanaleta vurugu kwenye soka letu,ipo cku mtu atakufa uwanjani
 
Habari za hivi punde kutoka tff zinasema kwamba waamuzi wa mechi ya Azam na Mtibwa iliyovunjika wameondolewa kwenye list ya waamuzi wa tff.Lakini pia kamati ya nidhamu imeipa Azam point3 na magoli3,pia imeipiga faini mtibwa sugar kwa kutia mpira kwapani.
Chanzo radio uhuru kipindi cha michezo.
Uamuzi wa kuwafungia marefa wasiojua kanuni na wanaoharibu mpira wa Tz ni sahihi kabisa, kwa sababu kihalali na kwa mujibu wa kanuni alitakiwa kumaliza mpira baada ya dk 15. Ila linaloshangaza hapa ni mtibwa pia kuadhibiwa. Kimsingi mchezo ulitakiwa kurudiwa, period. Inakuwaje refa aadhibiwe kwa kumaliza mechi kabla ya muda halafu hapohapo unaiadhibu timu kuwa iligomea mechi hiyo hiyo, hee..!!, huu si uchizi??!
 
Haya ndo tunayozungumza kila siku kwamba tff wbnatoa maamuzi through vyombo vya habari. wametoa hayo maamuzi coz,baadhi ya vyombo vya habar vilitangaza '"mtibwa wamegomea mechi'' kumbe haikuwa hivyo!
 
Kwangu mimi mechi hii ingerudiwa ndo ningeona TFF wametenda haki, maana hawa jamaa wanajifanya wanatumia kanuni halafu wanashindwa kuzifuata sijui kwa nini, kanuni inasema refa atasubiri hadi dakika kumi na tano ndo avunje pambano, nini kilimfanya asisubiri hadi huo muda na je labda Mtibwa walikuwa wanashauriana halafu warudi na kanuni pia inasema kama timu itasababisha vurugu na pambano kutoendelea timu hiyo itapoteza pambano na itakuwa imefungwa magoli matatu pamoja na kushushwa daraja, kama kweli waliona Mtibwa wana makosa kwa nini hawajawashusha daraja?

Mkuu
Kanuni inasema kama timu itashindwea kufika uwanjani timu pinzani itawepa usshindi wa magoli matatu na point tatu baada ya refa kusubiri dakika kumi na tano ila kama timu imegomea mchezo ndani ya dakika tisini za mchezo basi refa atasubiri hadi muda wa kawaida wa mchezo kuisha ndipo amalize mchezo,
kwa kesi ya Azam na Mtibwa mchezo ulikuwa umebaki dakika 6 tu ili mechi iishe kwahiyo alichokifanya refa ni kumaliza mchezo ndani ya dakika sita.
Ila TFF wanajichanganya kumpa adhabu refa kwa kumaliza mchezo kabla ya muda ila wangemuadhibu refa kwa kosa la kutokumudu mchezo wakati huo huo kuipa adhabu Mtibwa lwa kugomea mchezo.
Mtibwa wanaweza kukata rufaa kwa kosa la refa ambalo TFF itawagarimu kwa kujichanganya kutoa adhabu amabo sio sahihi kwa refa
 
Nashukuru kwa kunipa hiyo shule, lakini bado maamuzi ya TFF ya utata, kwa nini wamwadhibu refa at the same time waiadhibu Mtibwa na bado kama Mtibwa walikuwa wana makosa adhabu yao kwa nini haikukamilika?
 
Back
Top Bottom