WAALIMUMgomo HATARI Kuliko Mingine

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
1,488
908
AMAANDAMANO SONGEA  2.jpg ..... Tanzania-muhimbil-patient-e.jpg ... wanafunzi-waandamana-375x252.jpg

WAALIMU: mgomo HATARI zaidi Kuliko mingine


Katika Utumishi wa serikali kuna kada mbalimbali zikiwemo Jeshi, Uuguzi, watumishi wa serikali kuu na serikali za mitaa pamoja na mashirika yake ya Umma.

Mgomo wa Walimu ndio unaoongoza kwa uwezo mkubwa wa kutunisha misuli yake na kuleta maafa makubwa sana na athari ambazo si rahisi kuzibika kama ukiachiwa uendelee kwa zaidi ya wiki moja.
Kwa kifupi tuchambue migomo ya sekta hizi tukioanisha na mgomo wa sekta ya Elimu ndani ya nchi

JESHI:

Kwa Chambuzi zangu, Mgomo wa Jeshi, Mathalan Jeshi la Magereza, Polisi na Jeshi la wananchi. Wakigoma au wakaacha kufanya kazi zao za kila siku, hasara au madhara yatayotokana na mgomo wao yanategemea ustarabu wa jamii Husika, na nchi husika. Kwa upande wa Jeshi, Mipaka ya Ulinzi wa nchi na nchi kwa sasa ni Jukumu ya Umoja wa Kimataifa. Hata nchi yako ikivamiwa ni suala la jeshi la Umoja wa mataifa linaloundwa na nchi washiriki kwenye mabara husika na ndio wenye dhamana ya Kumtimua mvamizi. Hivyo kwenye ulimwengu wa saa Jeshi la Ulinzi sanansana ni chombo cha kukodiwa na kukodisha.

Magereza wakigoma kuna tutarajie kundi kubwa la wafungwa maskini hao ambao wengi wamefungwa kwa wizi wa kuku na shati, wengine wamebambikiziwa kesi, wengine husuda tu, na wengine na kakundi kadogo sana ambo kweli wamfungwa kwa makosa halali, wote hwa watakuwa HURU, huku watu waliotafuna keki ya taifa na kukwimba mamilioni na kufanya mauaji mengi ya kutisha wakiendelea kula bata kwenye taifa letu huru kabisa.

Tukijumlisha na mgomo wa Polisi, Nchi yetu kwa sasa sidhani kama kuna raia anayejivunia Jeshi la Polisi. Raia wengi wanajilinda wenyewe kwa Ulinzi shirikishi na wanalipia ulinzi huo kwa fedha zao. Jeshi la Polisi limekuwa adui kwa wananchi wake. Mtu akiwa na shida ya ain yoyote akikimbilia polisi anavuna machungu, kero na usumbufu wa kila aina. Polisi wetu hawana rekodi ya kukamata jambazi, ukivamiwa usiku, kwanza wanakuja muda mrefu baada ya tukio, na ni mahiri kwelikweli wa kuandika taarifa za tukio na kutimua zao. Barabarani napo watu watakuwa free ku-drive pasipo mikonomikono na kuombwa vijisenti all ways. So jeshi la Polisi kw Tanzania Likigoma Kutakuwa na Uhuru sana kwa raia.. kero wakati wa usiku zitashughulikiwa na Sungusungu, Ulinzi shirikishi na makumi ya makampuni ya Ulinzi yaliyopo.
Kwa Upande wa watumishi hao wa jeshi , mgomo huo utaendelea na wao bila kuathiri tabaka jingine la jamii.

UUGUZI:

Sekta hii nayo kwa upande wake ikigoma kuna madhara makubwa ya kitabibu ambayo yataathiri kipande cha jamii hasa kile kinachopitia nyakati za maradhi huku upande mkubwa wa jamii nyingine ukiwa Shwari. Kutokana na wigo mpana wa sekta ya matibabu, waathirika ambao ni wagonjwa wanaweza kujihifadhi kwenye wingi wa vituo na hospitali za binafsi zilizopo, ingawa gharama kwa baadhi ya wagonjwa wasio na uwezo mzuri zitawasumbua, lakini kuna ahueni kwamba walau kuna hospitali za binafsi ndani ya miji mikubwa na vijijini pia. Hivyo makali ya mgomo wa sekta hii kwa watumishi wa serikali walau unaweza kudhibitiwa kwa kiasi Fulani.

MGOMO KWA WATUMISHI WA SERIKALI KUUNA MITAA.

Kwa ujumla madhara ya mgomu huu ni kuchelewesha shughuli za kimaendeleo ambazo kwa jamii yetu sio tu hazionekani bali zimezimika kwa muda mrefu. Na pia vievile mgomo huu ni moja kati ya migomo isiyo na mshiko .

MGOMO WA WAALIMU.

Mgomo wa waalimu wa kada yoyoye huleta madhara makubwa sana ambayo si rahisi kuyadhibiti. Walimu wakigoma sekta ya Elimu ambayo huongozwa na mitaala na mitala huongozwa na Muda wa majira ya mwaka. Mgomo wa waalimu huathiri na kusimamisha mtaala wa taaluma wakati muda ukiendelea kuyoyoma. Hakuna mrahama (replacement ) ya Muda, mtaala ukipita umepita, kipindi kikiondoka hakirudi tena. Si rahisi kurudia mtaala. Mgomo wa waalimu hukatili taaluma ya wanafunzi, na kama ukidumu kwa zaidi ya wiki, Mtaala utaharibika. Na kama mfumo wa mtaala umeharibika, lazima uanze upya. Hii ina maana serikali inaahirisha masomo ya wanafunzi kwa mwaka mzima na kuanza tena upya. Hii ina maana wale wanaopanda na elimu ya juu, lazima liwepo Gap la mwaka mzima na wale wanaotaraia kuanza shule watawajibika kuahirisha na kurundikana baada ya mwaka. Si tu kuathiri wanaodahiriwa bali pia itaathiri wale wataoendelea na masomo kwenye private sc, maana italazimika ama wakae mwaka mzima wakisubiri kada nyingine ya mfumo wa serikali au wahitimishe taaluma zao kikatili.
Mgomo wa waalimu huleta Athari kubwa za kisaikolojia kwa wanafunzi ambao watalazimika kuhaha wakitafuta endelezo la elimu zao, si kwa wanafunzi tu bali hata wazazi wataingia kwenye wakati mgumu wa kulazimika kupanga jinsi ya kuwaendeleza watoto wao lakini pia kubadoilisha mtiririko wa mipango yao ya kifamilia.
Mgomo wa waalimu ni mgomo wa chi nzima na wadau wa kada zote. Unawaathiri madaktari, wanajeshi, watumishi wa serikali kuu na mitaa, wanasiasa, watumishi wa kada binafsi na wazazi kwa sababu kwa namna yoyote lazima watoto wao watakuwa kwenye mfumo wa kitaaluma hivyo itawakera na kuwasumbua sana. Mwalimu ni mtu wa Muhimu sana.
Mgomo wa waalimu huumiza kila sekta, Hatakama serikali italazimisha waalimu kuendelea na kazi zao bila kugoma pasipo kuwatimizia mahitaji yao, watafanyika vyombo hatari sana kwenye sahani la Elimu. Ni hatari mwalimu ambaye hakuridhishwa na mwajiri wake (discontented) Kutoa elimu kwa mwanafunzi. Lazima ataharibu na kuathiri baadae(future) ya watoto wa taifa hili la keshokutwa kama si la kesho.
Mgomo wa waalimuni janga la Taifa lolote makini, ila taifa la mabaradhuli, wazee wa liwalo na liwe, wasiojali utaifa wala wataifa, kwao ni POTELEAMBALI.

382454_338374539581848_645297104_n.jpg

 
Back
Top Bottom