Waalimu wamesahaulika au wamejisahau?

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Suala la waalimu kugoma sii jipia maskioni mwa watu wengi.
Tulishuhudia mgomo wa waalimu Tanzania, na sasa waalimu Kenya nao wako kwenye mgomo.

Miaka ya nyuma hatukuwahi kusikia waalimu wakigoma.

Najiuliza, hii migomo ya waalimu inaashiria kwamba waalimu wamesahauliwa au wamejisahau?
 
Taaluma ya Ualimu ilianza kuharibika na kusahauliwa mwaka ule walipo anzisha elimu ya UPE.
 
Sasa tufanye nini ili taaluma ya ualimu ifanyiwe ukarabati?

sehemu nyingi ziko katka hali mbaya. maslah yako chin, vitendea kaz na mazingira ya kaz si bora kias hicho.
kwenye sekta nyingine ndo maana rushwa kama kaz.
mwalim ataiba nin? chaki? michango ya shule?
au akaange na kuuza maandaz, vitumbua, alime (kwa walio maeneo ya shamba) na nk? it seems good.
mishahara yao ni midogo na mazingira ya kazi zao hayajarahisishwa na wakat huohuo wao ni watumishi wa moja ya sekta muhimu sana kwa nchi yetu.
ilikuwa muhim kujinyima na kuzibana sehem zingine ili sekta ya elimu ijengewe mazingira mazur.
jamii zilizo mbele kimaendeleo au kiteknolojia zilipata kutilia sana mkazo elimu huko nyuma. na ili ziendelee zinajua inabid ziendelee kuwekeza katka elimu kwa watu wake

ili mambo yaende sawa hapa inabid kuangalia upya maslahi ya mtu kufanya kaz ya ualimu. siamin kwamba mtu ataamua kwenda kufundisha eti kwa vile ni hobby. watu siku hiz cha kwanza wanachoangalia ni anapata shiling ngap katka kaz afanyayo? pato lisilokidhi mahitaj ya msing linavunja morali ya kaz na kupelekea walim wetu wawe bize kufanya biashara za ubuyu. ticha kama huyu hata ukimtishia kumtimua kaz wala hawez kubabaika.

kitu kingine ni mazingira ya kaz yenyewe. ni muhim madarasa yakawa madarasa kweli. darasa moja watachangiaje wanafunz wa madarasa mawili at the same time?
tunataka kuwafundisha nin wanafunz tunapokosa kuwapatia vitu kama vitabu vya kujisomea? au tunamaanisha nin tunapojenga mazingira kama vile kusoma kuwe kama adhab? well, kusoma sio starehe kwa wengi, lakin ni muhimu tukajenga mazingira yanayovutia kwa vijana wetu kias cha kwamba anapoenda shule au anapoamua kujisomea asione kama anajitumbukiza matesoni mara mbili. kwanza tunakuwa tunawapa shida ya kuelewa concepts mpya kutoka viabun halaf tunawatesa kwa kuwatembeza umbal mrefu kufuata hizo shule au tunawakalisha kutwa bila kuwapa hata uji. mambo haya tunayafanya kwa wahandis wetu, madaktar wetu, wahasibu wetu wa baadae wakat sis tumestaaf na hatuna nguvu tena za kufanya kaz hizo

walimu lazima wapigwe brashi mara kwa mara na wawe incouraged kujiendeleza. na ikiwezekana iwe kama lazima. si sawa mwalim anaanza kufundisha na diploma yake, anafundisha miaka 15 na bado hajaongeza chochote kitaaluma.
 
Hata hivyo,
Bajeti ya 2009/10 haikuonyesha wazi wazi itakavyowasaidia waalimu.
Kwani tatizo kubwa la waalimu ni kukosa nyumba za serikali za kuishi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom