Waalimu kufanya kazi ya sensa badala ya waliomaliza form 6 walioko nyumbani wakisubiri kwenda chuo

Inanambo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
3,975
2,755
Nimesikitika sana baada ya kukosa hata kibarua cha muda mfupi cha kusaidia serikali kufanya sensa mwaka huu. Nilimaliza form 6 mwaka jana niko tu home na wazazi wangu nawategemea kwa kila kitu from chakula, mavazi kunyoa na kusuka nywele, nauli ya kwenda na kurudi. Nimetafuta tempo kila pahala hata ya kuuza duka sijapata angalau na mimi nizoea kidogo kupata kwa jasho langu. Nikasikia kuna watu wanatafutwa wa kufanya sensa. Nikaenda kwa serikali za mitaa kuulizia nikaambiwa eti lazima uwe mwalimu ndio utapewa kazi hiyo. Nikajaribu kwenda wilayani nikapewa jibu hilo hilo. Nauliza hivi sisi tuliomaliza form 6 hatuwezi kusaidia serikali kufanya kazi hiyo? Waalimu tayari wana ajira yao na wanapata mshahara. Wao kila ikija sensa, uchaguzi ndio huwa wanapewa nafasi tuu. Watu wengine hata kama tuna identity zinazojulikana hutupewagi hizo nafasi. Ni bora waalimu wafunge shule wanafunzi wakose masomo ili wao wapewe kazi hizi. Mimi nimeona ingekuwa bora kwa kipindi hiki cha sensa na kuandikisha vitambulisho serikali ikawatumia vijana tuliomaliza sekondari tunaosubiri kwenda chuo
ili tusiendelee kuwa jobless wakati kuna shughuli tunaweza saidia serikali kufanya tena kwa ujira kidogo tu wa kununulia hata boxaa.
 
dogo subiri tangazo litoke utume maombi sensa kila raia anaruhusiwa kutuma maombi. sifa ni za kawaida uwe unajua kusoma na kuandika tatizo mnazidiwa kwenye sifa za ziada kama kuwa professional , kuwa mvumilivu na uzoefu sasa we na njaa yako utakuwa mvumilivu? walimu ni wavumilivu na wazoefu wa kazi za serikali. kuna uchaguzi mmoja wa raisi na wabunge walichukua wanajeshi mbona serikali ilijuta kuzaliwa!
 
Hayo matangazo yamepita chini kwa chini ndio sababu mimi na wenzangu tuliamua ya kuyatafuta hata huko serikali za mitaa tukakosa tukaambiwa ni nafasi ya waalimu tu. Bro kwa njaa hii na mimi nimejifunza uvumilivu hata nikiambiwa niende huko masaini nitaenda ili mradi nipate kidogo tu changu na mimi.
 
Usikate tamaa, safari ya maisha huwa inachangamoto sana, ulijaribu kutafuta hata kibarua cha kufundisha?Maana kuna hizi shule za kata bado zinaupungufu sana wa walimu, ungejaribu hata kusafiri kutoka hapo ulipo.Maisha ni kupambana kabisa usikae tu sehemu moja, ulizia hata rafiki zako uliosoma nao wanaweza kukupa wazo la kupata kibarua cha mda kabla ya kwenda chuo.Yangu ni hayo tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom