Waajiri wanaobana michango ya NSSF, PPF waadhibiwe

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Waajiri wanaobana michango ya NSSF, PPF waadhibiwe

KITENDO cha waajiri kutopeleka fedha za michango ya wafanyakazi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii ni tatizo sugu linalotakiwa kupatiwa ufumbuzi wa haraka na mamlaka zinazohusika, ikiwa ni pamoja na serikali kuingilia kati.

Kwa kipindi kirefu yamekuwepo malalamiko kutoka kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kwamba, waajiri kadhaa hawapeleki kwa wakati michango ya wafanyakazi wao, licha ya kuwakata katika mishahara, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.


Kwa mfano, mwishoni mwa wiki iliyopita, Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kilichoko Morogoro, kilishtakiwa kwa Rais Jakaya Kikwete alipokuwa kwenye ziara mkoani humo, kuwa tangu mwaka 2006 hakijapeleka michango ya wafanyakazi wake kwenye Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF).


Mbali na kiwanda hicho kuna waajiri wengi nchini wanawanyanyasa wafanyazi kazi wao kwa kutowapelekea michango yao kwa wakati, kiasi kwamba baadhi yao wanapofikia muda wa kustaafu na kudai haki zao, huambulia kuambiwa kuwa michango yao haijawasilishwa, licha ya mishahara yao kukatwa.


Huo ni unyonyaji na udhalilishaji wa wafanyakazi, tunaomba waache tabia hiyo na hatua za kisheria zichukuliwe kwa waajiri wote wanaochelewesha kupeleka michango hiyo kwa kuwatoza fidia kubwa na hatua nyingine kali kwa watakaokaidi.


Tunasema hayo kwa sababu fedha hizo ni jasho la wafanyakazi, na mtu yeyote anayejaribu kuwadhulumu ni sawa na kwamba anawaibia kwa kuwa ni dhahiri kwamba, hawawezi kupata faida inayotolewa na mifuko hiyo kulingana na michango wanayotoa na kusumbuka wakati wa kuzidai.
 
Back
Top Bottom