Dondola,
Sijui kama nimekuelewa vizuri lakini nadhani una maanisha kuwa sisi rangi yetu ndio nuksi yenyewe au sio?.....
Hapana ndugu yangu sii rangi yetu isipokuwa sisi Waafrika kilichotuangusha hadi leo ni kama nilivyotaja hapo juu. Mbali na fikra binafsi nadhani mchango mkubwa wa udhaifu wetu umetokana na ULIMBUKENI. Katika mataifa yote unayoyafahamu ebu nambie race hata moja ililopoteza kabisa culture zake na kubeba za kigeni?...hakuna...
Waafrika peke yetu bob na kibaya ni kwamba hatukubaliki na hao tunaowaiga. Wale waliotawaliwa na Mfaransa basi hao hujifanya Wafaransa kuliko hata Wafaransa mwenyewe. Na tunaamini kabisa kuwa hatuwezi kukubalika bila kujifunza culture za hawa watu. Huyo Mmarekani mweusi imechukua karne nzima kuweza yeye kukubali kuwa ana asili na Afrika tena baada ya wazungu kuwatema. Huko South ndio kabisa hawakubali kama Maspanish, bado tu wameshikilia kuwa wao ni maspanish!...hawataki kabisa kujishirikisha na Afrika. Lakini huyaoni haya ktk race nyinginezo, Mchina amebaki Mchina popote pale alipo hata kama atazungumza lugha yako fluent. Na atafanya juu chini uanze kula wali kwa vijiti, kumwabudu Budha na hata ujifunze Kung fu na Karate.
Tazama Kariakoo, si wamejaa Wachina hao wamachinga lakini subiri sii muda Chinese food itakavyoanza kupata soko!.. they sale Chinese product! Mtu mweusi tunaona Uafrika ni uchawi tu unatia kiza! Wahindi vile vile leo hii chakula chetu kikuu cha kumkamatia mgeni utasema Biryani... tumeiga wapi?
Tazama, Hata taifa la zamani kihistoria kama Misri wamepoteza kabisa lugha na culture zao zoteeee! leo hii wanajullikana Wamisri kama Waarabu hakuna tena Mu - Misri wala culture zake zaidi ya kusimuliwa hao akina Pharaoh.
Ulimbukeni mshikaji na leo hii kiswahili kinaonekana choo kabisa tena tumeanza hata kukiwekea mashaka kuwa ni lugha ya utumwa maadam tu Kiingereza kipate nafasi ya kwanza tujisikie nasi binadamu - wazungu.
Kifupi sidhani kama matatizo yetu yanatokana na laana ya rangi. Isipokuwa mambo muhimu hapo juu yakichangia na Kushindwa kusamehe Utumwa kama ni jambo lililokwisha tokea na tuangalie mbele. Wagonjwa wa Dipresheni huendelea kudhoofika kila siku wanaposhindwa kusamehe matukio yaliyopita ili wapate mwanzo mpya. Na wengine hufa bila gonjwa kwani wakipimwa hospital huonekana wazimaaa! basi Afrika ndio maradhi yetu hayo!