Wa zamani bado ni wako?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,216
113,520
Hebu niwaulize wana JF. Wewe ukiona wako wa zamani (ex) anatoka na mtu mwingine eti utajali? Kuna jamaa mmoja kwa kweli simwelewi. Sielewi kabisa mantiki yake na jinsi mchakato wake wa kufikiri ulivyo.

Eti huyu jamaa huwaga anamaindi aonapo wanawake aliowahi kutoka nao wana watu wengine. Eti kwa mtazamo wake hao ni "mademu" wake na iweje jamaa mwingine atoke nao.

Mimi nimeshindwa kabisa kumwelewa. Mtu ukishaachana na mpenzi wako na miaka ikapita bado utadai tu kuwa huyo mpenzi ni wako? Haiingii akilini kabisa. Mimi nilidhani mkishaachana ndo basi tena kila mtu anakuwa huru kutoka na yeyote yule ampendaye.
 
Hata sijui niseme mshkaji ana matatizo gani..labda anadhani ukiwa na mtu mara moja ndo ataitwa wako milele...basi nae asiongeze "demu" mwingine maana tayari ni bwana wa wengi!Mwambie chako ni chako ukiwa nacho ..usipokua nacho si chako tena!
 
...kalumanzila... huenda jamaa yako ni mganga wa kienyeji
 
NN hiyo ipo sana yaani kuna jamaa liliwahi kusema nikikukuta na mtu naua yeye na wewe kha???

Mie nikikuacha ndo mchezo umeaishia hapo yaani sitaki longolongo tena
 
Nyani ngabu. Asante. Ninae rafiki anakuwa na demu baa lakini akiona demu aliyetoka nae hata mara moja anahakikisha anamharibia demu huyo kwa vyovyote vile. Huwa anatushangaza.
 
Hee!!hii tena kali, hata simwelewi na sitaweza kumwelewa,
yeye kuacha na kuanza uhusiano mwingine RUKSA,
ILA wenzie HAPANA hata wakiachwa waendelee tu kumsubiri,,,hii tena kali,
wanawake wenyewe wepi? hawa wa karne hii??, hawa ambao wana full kujitambua na kujiamini kwa kila siku,
huyu aandike tu maumivu.....akitaka wasiwe na mahusiano mengine basi na yeye awe mtulivu asiwaudhi hata kidogo....
 
namaanisha kwa kila kitu.
sorry!.
 
Hebu niwaulize wana JF. Wewe ukiona wako wa zamani (ex) anatoka na mtu mwingine eti utajali? Kuna jamaa mmoja kwa kweli simwelewi. Sielewi kabisa mantiki yake na jinsi mchakato wake wa kufikiri ulivyo.

Eti huyu jamaa huwaga anamaindi aonapo wanawake aliowahi kutoka nao wana watu wengine. Eti kwa mtazamo wake hao ni "mademu" wake na iweje jamaa mwingine atoke nao.

Mimi nimeshindwa kabisa kumwelewa. Mtu ukishaachana na mpenzi wako na miaka ikapita bado utadai tu kuwa huyo mpenzi ni wako? Haiingii akilini kabisa. Mimi nilidhani mkishaachana ndo basi tena kila mtu anakuwa huru kutoka na yeyote yule ampendaye.

Jamaa kweli ana matatizo..kwangu mie tukiachana ndiyo imetoka na ikirudi pancha!! Hata nimwone x'bf na gf/mke wake, najua wakati wetu ulishapita hivyo ni historia hamna zaidi!!
 
NN hiyo ipo sana yaani kuna jamaa liliwahi kusema nikikukuta na mtu naua yeye na wewe kha???

Mie nikikuacha ndo mchezo umeaishia hapo yaani sitaki longolongo tena

Kwa kweli ni danger ya hatari sana. Watu wa dizaini hiyo ndo huwaga wanaapa kama hutaki kuwa naye basi atahakikisha hakuna atakayekuwa na wewe. Mapenzi haya bana.
 
Jamaa kweli ana matatizo..kwangu mie tukiachana ndiyo imetoka na ikirudi pancha!! Hata nimwone x'bf na gf/mke wake, najua wakati wetu ulishapita hivyo ni historia hamna zaidi!!

Ana matatizo si kidogo. Halafu hata ku-reason naye inakuwa ngumu.
 
kazi kweli kweli...ila waga inauma fulani but since tulishaachana sina la kufanya,naheshimu mahusiano yao na wao wanaheshimu yangu.....!!!
 
Hebu niwaulize wana JF. Wewe ukiona wako wa zamani (ex) anatoka na mtu mwingine eti utajali? Kuna jamaa mmoja kwa kweli simwelewi. Sielewi kabisa mantiki yake na jinsi mchakato wake wa kufikiri ulivyo.

Eti huyu jamaa huwaga anamaindi aonapo wanawake aliowahi kutoka nao wana watu wengine. Eti kwa mtazamo wake hao ni “mademu” wake na iweje jamaa mwingine atoke nao.

Mimi nimeshindwa kabisa kumwelewa. Mtu ukishaachana na mpenzi wako na miaka ikapita bado utadai tu kuwa huyo mpenzi ni wako? Haiingii akilini kabisa. Mimi nilidhani mkishaachana ndo basi tena kila mtu anakuwa huru kutoka na yeyote yule ampendaye.

Kuna mahali Bible inasema . . . .

Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye?

If its true ulikula zamani . . . does it mean bado ni wako?
 
Michelle;1880761] kazi kweli kweli...ila waga inauma fulani but since tulishaachana sina la kufanya,naheshimu mahusiano yao na wao wanaheshimu yangu......!!!

Kwa hiyo unatamani kama mgekuwa pamoja mnaendelea au? Kuumia roho inamaana bado unampenda huyo mtu, na kwa maana nyingine akije kubembeleza kuna uwezekanao wa kurudiana!
,
 
mie Ex wangu namchekigi kila siku facebook ingawa yeye hajui,u unless mtu hukumpenda kama ulipenda kikweli kweli karoho kanauma,ila wengi wetu tunamezea huwezi ukaharibu future ya mwenzio kwa wivu wako:yawn:
 
Dah hiyo si ni cyber stalking au?
 
Mkiachana kila mtu na hamsini zake ,

,ila jamani vipi kama uliachwa ukiwa bado unapenda??????????/ sii kawivu katakuwepo ukimuona na mwingine?????????????? Just said!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
Kwa hiyo unatamani kama mgekuwa pamoja mnaendelea au? Kuumia roho inamaana bado unampenda huyo mtu, na kwa maana nyingine akije kubembeleza kuna uwezekanao wa kurudiana!
,

jibu la kama natamani kuwa nae bado ni NDIYO NA HAPANA....waga inatokea najisikia hivyo...siwezi kusema mwanaume niliyeachana nae bila visa namchukia.....kama tulipendana dini ikazuia kwenda hatua moja zaidi kwanini nimchukie???

Uwezekano wa kurudiana na mwanaume niliyeishaachana nae ni mdogo na si kwa kubembelezwa bali kwa yeye kufanya maamuzi magumu kama kubadili dini yake etc
 
Back
Top Bottom