Wa Tz Wanafundishwa kiswahili na Wakenya!!!

GAMBLER

JF-Expert Member
Nov 22, 2009
303
11
Mtoto wangu anasoma Saint Marry, Na walimu wa pale karibu wote ni wakenya na waganda, cha ajabu sasa wanawafundisha mpaka kiswahili watz, walimpa homework ya kiswahili mtoto wangu, wakamuandikia wingi wa neno la mama=wamama, kaka=wakaka. ...kwa kweli imenishtua sana, hawa watu hawajui kiswahili, halafu ndio wanatufundisha kiswahili...hii si hatari jamani!!..wadau Great thinkers mnaionaje hii issue??
 
Fasta Mwamishe mtoto. Shule zipo nyingi. Vipi maeneo ya kwenu hakuna shule hata ya kata? Mpeleke huko akafundishwe kiswahili fasaha! Si lazima mtoto asome St. Mtakatifu school jamani! LOL!
 
Pole sana ndugu!
Ila toka 2006 serekali ilishapiga marufuku wafanyakazi wakigeni wasio na vibali kufanya kazi nchini, hasa hao waalimu toka kenya!!
Kwa vyovyote huyo siyo mwalimu, hata huko kwao kenya hafai. Isaidie serikali kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama baada ya kubaini uhalali wa kufanya kazi hapo St Mary.
 
asante sana ndugu Kilemi
 
pole. uongozi wa shule ufanye hima kupitia uwezo wa kitaaluma wa waalimu hao
 
kwani wingi wa mama ni nini? mie nadhani wamama eti.LOL.. Kiswahili kigumu lakini.
 
Smatta ukishindwa kujua wingi wa neno mama, itakubidi utafute darasa

natania tu ndugu yangu, wingi wa mama si ni mama. jambo ambalo huwa linachangia wakenya wasiweze kuongea ama kuandika kiswahili sanifu ni kizungu na sheng na adhari ya lugha ya mama. lakini twaipenda lugha hii sana.
 
hahaha.. nimekupata
 
Tukisema Wakenya wengi ni vihiyo watu wanakataa ,na St Mary inavihiyo kibao toka Kenya,pia kwao kuongea kiingereza ni sawa na sisi tunavyoongea kiswahili na je ina maana kwa vile sisi wa TZ kila mtu anajua kiswahili anaweza kuajiriwa na shule kufundisha kiswahili? jibu ni hapana kiswahili kama somo inatakiwa lifundishwe kitaaluma na ndio wasiwasi wangu kwa wale wa wenye shule "International"kuajiri Wakenya na Waganda kutufundishia watoto wetu kiingereza ilihali hao "walimu hata vyuo hawajaenda"
 
watakikwemkapa ni hawafikirii kabisa wakishaona mtu anaongea kiingereza basi wanajua kuwa kasoma na anaweza akafundisha lol!!
 
Pole sana ndugu!
Ila toka 2006 serekali ilishapiga marufuku wafanyakazi wakigeni wasio na vibali kufanya kazi nchini, hasa hao waalimu toka kenya!!
Kwa vyovyote huyo siyo mwalimu, hata huko kwao kenya hafai. Isaidie serikali kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama baada ya kubaini uhalali wa kufanya kazi hapo St Mary.

Mkuu usitegemee chochote hapo, mwenye shule "kingunge", wewe unafikiri kwa nini alitafuta nafasi ya kisiasa? Teh teh!
Ila mkuu wa shule hiyo naye kilaza,ilibidi azuie hii move kabla haijawekwa kwenye ratiba, automatically mbongo akisikia mwanaye anafundishwa kiswahili na Mkenya lazima atakuwana wasiwasi. Sijui kama unafahamu kuwa Idara ya Kiswahili UON wako far much advanced kwenye Research za kiswahili kuliko TATAKI.
 
Aisee samahani nilishasahau "Ukitaka biashara yako ikunyookee jiunge na....."
 
Fasta Mwamishe mtoto. Shule zipo nyingi. Vipi maeneo ya kwenu hakuna shule hata ya kata? Mpeleke huko akafundishwe kiswahili fasaha! Si lazima mtoto asome St. Mtakatifu school jamani! LOL!
Haya ndo matatizo ya kukimbilia hizi shule za engilish medium, hawana lolote hawa, wanachojali sana ni kukudai pesa haraka sana na ukichelewesha hawana simile na kumrudisha mtoto nyumbani,

Pia serikali ilisha sema kuwa wawekezaji wanatakiwa kuwaajiri wazawa kwanza kabla ya wageni, ebu wizara ya elimu tuiombe ipitie shule zote hizi za binafsi
 
Hiyo ni hadaa na ujinga wa kutupwa. Nadhani Mchungaji mhesimiwa Dr Getrude Rwakatare anawajibu wa kuingilia kati. Akijibaraguza..awajibishwe kwa ujinga huo!!!
 
Jamani ST. Marry kumeoza siku nyingi. Nenda uone madarasa yalivyobaki tupu shule zote. hakuna walimu wa kitanzania pale wanakimbia kwa kuogopa dhuruma. Wanaajiriwa waganda na wakenya wasiokuwa na vibali, pia sifa ya ualimu. Walimu hupewa vyumba vidogo kuishi.

St. marrys ni balaa tupu.
 
Ni kweli hili ni tatizo, ukizingatia shuleni hususan ni hizi za awali hatujifunzi tu kusoma na kuandika, bali pia tunajifunza UZALENDO NA KUIJUA VYEMA HISTORIA YA NCHI. SASA WALIMU WENGI WA SHULE HIZI ZA AWALI WAKITOKA NJE YA NCHI, KUNA HATARI WATOTO WETU HAWATAKUWA WAZALENDO HALISI NA MAADILI YETU YA ASILI. WATAKUWA WANAJUA TU KUSOMA NA KUANDIKA.

PIA KUHUSU WALIMU WA SHULE HIZI ZA AWALI ZA BINAFSI KUCHUKULIWA TOKA NCHI JIRANI NI KUTOKA NA KUPUNGUZA GHARAMA, MAANA WALIMU WENGI WAGENI HULIPWA KWA KIASI KIDOGO KULIKO WAZAWA. NINA MIFANO MINGI TU YA SHULE ZA AINA HIYO MKOANI ARUSHA.
WENYE SHULE NI WAJASILIA MALI, LENGO LAO NI KUPUNGUZA GHARAMA, NA PALE NAFASI INAPOPATIKANA WANAITUMIA VILIVYO. UTAONA WENGI HATA WANASHIRIKI KUWAFICHA WASIJULIKANE NA MAAFISA UHAMIAJI MAANA WENGI HAWANA VIBALI VYA KUFANYA KAZI NCHINI NA PENGINE HATA VIBALI VYA UKAZI.
NI HAYO TU WAJUMBE.
NAOMBA KUWAKILISHA.
 
Back
Top Bottom