Wa TZ tutaendelea kupata viongoz wanaotaka kuweka Historia na si Uzalendo na nchi yetu.

augustino ameri

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
267
57
Wengi wa viongozi wetu wanagombea urais si kwa kuwa wanakerwa na matatizo yanalolikabili taifa letu na wananch wake,bali wanataka uongozi ili waingie kwenye rekodi kuwa waliwahi kuwa viongozi wa taifa hili.
Tutaendelea kupata viongozi wa namna hii kwa kuwa sisi wenyewe wapiga kura tunawapigia kura wagombea bila kuwa na vigezo.mtu anampigia mtu kura ukimuuliza sababu hata moja hana au atakwambia ana sura nzuri.Bila shaka inawezekana hata wapambe au wapiga debe huwa hawana sababu ya maana ya kumpigia debe mgombea zaidi ya kutegemea au kuahidiwa nafasi na mgombea.Tuache kupiga kura kwa lengo la uchama na udini,kiongozi mbovu athari zake ni kwa wote wa dini yako na dini nyingine,wa chama chako ni kingine athari hazichagui.Ukiingia kwenye gari la abiria wote nauli ni moja,ukienda sokoni wote nauli ni moja.
Kwa mtindo huu wa kukosa vigezo tunapata viongozi dhaifu kwani anashinda uongozi kwenye midaharo amekimbia, wananchi wamekosa fursa ya kuona uwezo wake wa kupambanua mambo na kujieleza.
NI VIZURI KUWA MAKINI hasa anapochukua uongozi kwa mara ya kwanza(URAISI) Kwani akiingia mhula wa kwanza viongozi wetu hapa Africa hutumia vyombo vyote kushinda(yaani vyombo vya dola)
Dalili za kiongozi dhaifu aliyeingia madarakani kwa lengo la kuweka hitoria ni nyingi sana miongoni ni hizi hapa:-

Kusimika viongozi dhaifu katika taasisi mbalimbali za serikali ili wamulinde na watii maagizo yake,kwani wanajua kuwa hawakustaili hizo nafasi hivyo kuingia kwa uongozi tofauti ni kuhatarisha vyeo vyao mfano vyeo vya majaji,wakuu wa vyombo vya dola,bungeni nk.

Kupiga,kuua,kutesa,na kubambikia kesi ,Kuwekea sumu,kumwagia tindikali watu wenye mitizamo tofauti na serikali kwa njia za kijambazi au ajali za magari na ndege.

kunapokuwa na tatizo na yeye kulalamika badala ya kutoa muongozo au suluhisho juu ya tatizo lililopo,anakuwa na lengo la kuonyesha kuwa na yeye anaathiriwa aonewe huruma huku akijua siku zinakwenda.

Kuwa kama mtalii muda mwingi safarini na kupenda kupiga picha na watu wenye majina makubwa duniani ili kujiwekea kumbukumbu.

Wakati wa uchaguzi na baada hutoa ahadi hata akijua haitimiziki ilimrad shinde atimize lengo lake mtajijua wenyewe baadaye.
kufungia vyombo vya habari vyenye mtizamo tofauti na serikali yake kama redio ,magazeti na tv.

.WATANZANIA TUTAKUWA MIAKA YOTE TUNATHAMINIWA WAKATI WA UCHAGUZI TU,KWA MBOLEA ZA RUZUKU,KUONEZEWA MISHAHARA VIZURI,POLENI SANA PIA WAZEE WA AFRIKA MASHARIKI.
 
Back
Top Bottom