Wa-Tanzania Tujifunze Kubadilika Tabia: Mengine ni Matatizo Yetu Wenyewe!

Mkuu Willie, I think this is a generation problem and somehow the skewed and irrational thinking kwamba hela ndiyo kila kitu. Nikikumbuka miaka ile vijijini pamoja na vijumba kuwa vya nyasi lakini unakuta kuna uwanja umefagiliwa, some lawn na hata maua. Nenda vijiji vya sasa huwezi amini kinachoendelea. Ukija mijini ndiyo kabisaa mtu atakwambia maji hamna, serikali haijafanya hili wala lile etc. But something very funny akijichanganya mtu mwenye tabia ya usafi hata kule uswahilini kabisa utasikia ebanaaaeee hapa anakaa mzungu nini?

Lingine ambalo linaniwia ugumu kulipambanua but just some points to ponder.........Mkuu unakumbuka yale maeneo yalikuwa yakiitwa uzunguni miaka ileeee? So beatiful, clean and green leo hii sijui kumetokea nini it's just a shame viduka kila mahali na vijikontena vya bia.

U go in a place like Hillbrow in Joburg South Africa, inafanana sana na Harlem kwa maana kwamba ni inner city suburb, high rise buildings is the norm, dominated na watu weusi and has been there for ages. The major difference ni kwamba ilikuwa ikikaliwa na wazungu zamani na sasa hakuna mweupe hata mmoja. Hii sehemu ni chafu kuliko kariakoo. Taka kila mahali mpaka kwenye door steps.Few meters away kuna Bramftoein totally different kusafi na system ya usafi na ukusanyaji taka ni ile ile kama Hillbrow. Tofauti wakazi wa huko ni mchanganyiko (weusi, weupe, yellow u name it) na most areas ziko dominated na wanafunzi wa Witts uni. Niliwahi kumuuliza ofisa mmoja why such a huge difference? Akaniambia simple watu wa Hillbrow can live with it (uchafu) na wanaamini usafi wa mazingira yao ni responsibility ya serikali.

ptg01155682.jpg
 
- I mean nipo njiani hapa kwenye Treni, ninatokea Boston kurudi New York City, njiani humu ninajionea Wazungu masikini, lakini nyumba zao ni safi, maeneo yao ni masafi, nyumba za mbao na mabati lakini zimewekewa uzio, kwa majani senyenge, miti au hata waya tu kuzunguka nyumba!

- Na pia bara bara sio za lami, lakini zimepangiliwa na zinaonyesha Mlango wa mbele wa nyumba, kuna box la barua, sasa sisi Tanzania jamani tumemkosea nini Mungu? I mean uchafu, wanyama wanakimbia kimbia hovyo bila mpango, hujui mbele ya nyumba ni wapi na nyuma ni wapi?

- I mean haya mengine ni yetu wananchi sio ya Serikali bana, Tubadilike tukitoka hapa JF twende majumbani na kwenye society and do something to our Society please!,

- Tumezidi mno, tubadilike sasa!

Willie @ NYC, USA.
actually baada ya kuisoma tena hii post nimelazimika kukumbuka mchango wa viongozi wetu kwenye tabia zote mbaya uluzotaja inlcuding john samwel malechela

viongozi hao walishindwa kuongoza nidhamu unayoitaja hapo juu
 
- Sawa mkuu wa JF, what a genius!

Willie @ NYC, USA
 
Mkuu Willie, I think this is a generation problem and somehow the skewed and irrational thinking kwamba hela ndiyo kila kitu. Nikikumbuka miaka ile vijijini pamoja na vijumba kuwa vya nyasi lakini unakuta kuna uwanja umefagiliwa, some lawn na hata maua. Nenda vijiji vya sasa huwezi amini kinachoendelea. Ukija mijini ndiyo kabisaa mtu atakwambia maji hamna, serikali haijafanya hili wala lile etc. But something very funny akijichanganya mtu mwenye tabia ya usafi hata kule uswahilini kabisa utasikia ebanaaaeee hapa anakaa mzungu nini?

Lingine ambalo linaniwia ugumu kulipambanua but just some points to ponder.........Mkuu unakumbuka yale maeneo yalikuwa yakiitwa uzunguni miaka ileeee? So beatiful, clean and green leo hii sijui kumetokea nini it's just a shame viduka kila mahali na vijikontena vya bia.

U go in a place like Hillbrow in Joburg South Africa, inafanana sana na Harlem kwa maana kwamba ni inner city suburb, high rise buildings is the norm, dominated na watu weusi and has been there for ages. The major difference ni kwamba ilikuwa ikikaliwa na wazungu zamani na sasa hakuna mweupe hata mmoja. Hii sehemu ni chafu kuliko kariakoo. Taka kila mahali mpaka kwenye door steps.Few meters away kuna Bramftoein totally different kusafi na system ya usafi na ukusanyaji taka ni ile ile kama Hillbrow. Tofauti wakazi wa huko ni mchanganyiko (weusi, weupe, yellow u name it) na most areas ziko dominated na wanafunzi wa Witts uni. Niliwahi kumuuliza ofisa mmoja why such a huge difference? Akaniambia simple watu wa Hillbrow can live with it (uchafu) na wanaamini usafi wa mazingira yao ni responsibility ya serikali.

ptg01155682.jpg

- 100% Great thinking!

Willie @ NYC, USA.
 
Mkuu umenikumbusha mbali...Niliwahi kuishi Kurasini shimo la Udongo...na pia kule mwananyamala kisiwani..Watu wanachimba vyoo vya shimo kilimani na visima vya maji kwenye bonde....Maji yanayopatikana humo hutumiwa kuoshea vyombo, kuoga n.k!!
!!

- Inaeleweka sana mkuu!

Willie @ NYC, USA
 
- Afadhali ya utumwa wa mawazo ya usafi kwa wewe uliye "bongo" ha! ha! ha! ha! walioko bongo hawaongei lugha za kifedhuli kama zako, endelea tu huko Ughaibuni ha! ha!

Willie @ NYC, USA.

mkuu nipo bongo! sitarajii kwenda ughaibuni, natoka familia ya kifukara kweli kweli, kwa mimi kwenda ughaibuni ni mpaka tupate katiba mpya itakayotoa usawa wa kwenda popote bila upendeleo. kama kauli yangu imekuudhi nisamehe, nimeifuta.
 
- I mean nipo njiani hapa kwenye Treni, ninatokea Boston kurudi New York City, njiani humu ninajionea Wazungu masikini, lakini nyumba zao ni safi, maeneo yao ni masafi, nyumba za mbao na mabati lakini zimewekewa uzio, kwa majani senyenge, miti au hata waya tu kuzunguka nyumba!

- Na pia bara bara sio za lami, lakini zimepangiliwa na zinaonyesha Mlango wa mbele wa nyumba, kuna box la barua, sasa sisi Tanzania jamani tumemkosea nini Mungu? I mean uchafu, wanyama wanakimbia kimbia hovyo bila mpango, hujui mbele ya nyumba ni wapi na nyuma ni wapi?

- I mean haya mengine ni yetu wananchi sio ya Serikali bana, Tubadilike tukitoka hapa JF twende majumbani na kwenye society and do something to our Society please!,

- Tumezidi mno, tubadilike sasa!

Willie @ NYC, USA.

Mkuu WM:
Si jambo la kushangaa kabisa hilo...Utawala wa sheria, taratibu na tamaduni zetu. Natumaini ulishawahi kuishi Oystebay Tanzania. Sehemu kubwa ya viongozi wa taifa hili walikuwa/wanafuga wanyama kwenye maeneo ya makazi ya watu(soma: residential area). Kama viongozi wetu wenyewe ndo vinara wa uvunjaji wa maadili na utawala bora, unategemea nini?
Mipango miji inaendeshwa kijanja janja....kuna msemo unaosema:'samaki uoza kuanzia kichwani' na ndivyo taifa hili lilivyo
 
William unaweza ukawa una maanisha kitu kizuri sana. Usafi ni kitu kinachojengwa kutoka rohoni na mazingira na makuzi.
Ila hawa wenzetu vitu vingi vipo inforced na sheria. Texas ukitupa karatasi ukikamatwa unapigwa faini au kwenda jela. Ukinunua nyumba sehemu zinazoonekana ikiwa chafu unapata faini. ukishindwa kukata majani ya nyumbani kwako kutokana na sheria unapata faini.

Miji imepangwa, kuna sewage system kila mahali. Kuna vyoo vya public bara bara nzima. Sasa usafiwa ni tabia na sheria. Uhuru bila mipaka ni ukichaa.

Hatuwezi kujadili mada kama hii bila kulaumu viongozi na serikali iliyopo madarakani. Wameshindwa kwa kila kitu. Mipango miji sifuri, law enforcement zero. Viongozi wengi hawana upeo wa kufikiri, wanaona lakini vipofu, wanasikia lakini viziwi, wanasoma hawaelewi. Tunawasomesha nje ili waone na wasikie na wasome ila wakirudi nchini wanakuwa wapumbavu sana.

Wito kila mwenye upeo na anapenda maendeleo ya kweli Tanzania aombe kazi serikali kusaidia kuleta maendeleo kiutawala, mwelekeo, na mipango mizuri ya nchi yetu. Kama wataingia wengi wazuri kama hawa bila kujali itikadi za siasa na kuweza kuwa na lengo moja kuimarisha uchumi, mipango, kuchangia mfumo mzuri wa miji mitaa, ukusanyaji kodi na elimu kwa jamii tutaendelea. Wajitolee watu wenye ushawishi kutoa elimu ya viongozi na kuwapiga msasa. Kusaidia kutengeneza mifumo itakayosaidia kutuendeleza. Pamoja tunaweza
 
Hillbrow - Joburg SA

2rqomx0.jpg

Braamfontein - Joburg SA

28clgm9.jpg

Unaweza kuamini hayo maeneo yako umbali usiozidi km 5?
 
- Suala la usafi wa binafsi na mazingara yetu Serikali hahihusu, tufanye usafi wa mazingara yetu, tusafishe nyumba zetu, nimesema huku nimeona nyumba zimezungushiwa uzio wa miti, kuna nyumba zimezungushiwa uzio wa majani na michongoma, hii hahitaji hela ni ubunifu tu na kujituma, TUBADILIKE!

Willie @ NYC, USA.

Willie,
Wewe umeona wao hawajaona wewe unauwezo wao hawana.
Kutatua tatizo ni pamoja na kulielewa, huwezi kuzima moshi wakati shina la moto bado linatema. Mazingira, uchumi, elimu na mahitaji vinachangia maendeleo sana ya sehemu husika. Vijijini ni wasafi sana ingawa ni masikini. Kuna sehemu kubwa sana ya kutupa takataka, na kuna uwezo mkubwa wa kchimba vyoo hata vipya kila siku.

Kama umewahi kufika vijijini utaona wao wanajitahidi kwa usafi.
Mijini duniani kote lazima mipango miji imara na sheria za miji hiyo kufuatwa. Dar es salaam hakuna mipango miji, hakuna maji, hakuna magari ya taka. Hakuna ajira hivyo kila mmoja hubuni ajira alipo, kuuza dagaa, vitumbua, maziwa, kufuga hata juu ya ghorafa. kumbuka hapa kitu mhimu ni kupata kipato.

Shughuki zote hizo zinazalisha uchafu, utupwe wapi? Katikati ya manzese hakuna mifereji ya maji machafu, kwa umasikini wao inabidi wachimbe vyoo popote hata mbele ya mlango wa jirani. Ni kero na inasikitisha. Tatizo kubwa la uchafu kwenye miji yetu ni mifumo mibovu na usimazi wa miji unaosababishwa na mipango miji mibovu.

Kuna mambo yanahusu wananchi na kuna mambo yanahusu serikali. Huwezi kumlaumu mtoto kwanini amefeli wakati hukumpa vitendea kazi, vitabu, waalimu, umeme, muda wa kusoma nk. Ukimpatia mahitaji yake yote unabakia wajibu wake wa kusoma na kufaulu. Na uchafu wa sehemu husika lazima kuangalia pande zote za shillingi. Serikali ndio imeshindwa na inatupia lawama kwa wananchi. Njoo uswazi kaka uone maisha ya ukweli.
 
- I mean nipo njiani hapa kwenye Treni, ninatokea Boston kurudi New York City, njiani humu ninajionea Wazungu masikini, lakini nyumba zao ni safi, maeneo yao ni masafi, nyumba za mbao na mabati lakini zimewekewa uzio, kwa majani senyenge, miti au hata waya tu kuzunguka nyumba!

- Na pia bara bara sio za lami, lakini zimepangiliwa na zinaonyesha Mlango wa mbele wa nyumba, kuna box la barua, sasa sisi Tanzania jamani tumemkosea nini Mungu? I mean uchafu, wanyama wanakimbia kimbia hovyo bila mpango, hujui mbele ya nyumba ni wapi na nyuma ni wapi?

- I mean haya mengine ni yetu wananchi sio ya Serikali bana, Tubadilike tukitoka hapa JF twende majumbani na kwenye society and do something to our Society please!, - Tumezidi mno, tubadilike sasa!

Willie @ NYC, USA.

Hujaona ya black au mlatino?

Kama hujaona hizi I doubt kama utakuwa umepita maeneo ya 'tabaka la kina baba Kabwela' maana naamini naamini maeneo hayo lazma yawe na watu wa kila rangi na aina sio wazungu tu kama ulivyoona wewe. otherwize nahisi wewe upo kati ya wanaomini kila kizuri lazma kina 'mzungu'!

I doubt that may be you are using standard za @NYC kuangalia miji yetu.

Huko wanyama hawakimbii kimbii kwa sababu hao wazungu ni masikini kama ulivyosema kwa hiyo inawezekana hawana wanyama watakaokimbia.Wangekwepo ungewaona tu!

Kwetu sisi mbele ya nyumba ni pale unapoingilia na nyuma ni pale unapotokea sasa kama mtu anaingilia na kutokea hapo hapo ina maana mbele na nyuma ni hapo hapo, huelewi nini sasa hapo?

Ni kweli tumezidi mno (kwa viwango vyako) , nimebahatika kupita mtera ambapo mzee wako alikuwa Mbunge kwa muda mrefu, nimeona mtera pameendelea sana kama NYC. (mix with yours)
 
- I mean nipo njiani hapa kwenye Treni, ninatokea Boston kurudi New York City, njiani humu ninajionea Wazungu masikini, lakini nyumba zao ni safi, maeneo yao ni masafi, nyumba za mbao na mabati lakini zimewekewa uzio, kwa majani senyenge, miti au hata waya tu kuzunguka nyumba!

- Na pia bara bara sio za lami, lakini zimepangiliwa na zinaonyesha Mlango wa mbele wa nyumba, kuna box la barua, sasa sisi Tanzania jamani tumemkosea nini Mungu? I mean uchafu, wanyama wanakimbia kimbia hovyo bila mpango, hujui mbele ya nyumba ni wapi na nyuma ni wapi?

- I mean haya mengine ni yetu wananchi sio ya Serikali bana, Tubadilike tukitoka hapa JF twende majumbani na kwenye society and do something to our Society please!,

- Tumezidi mno, tubadilike sasa!

Willie @ NYC, USA.

Willie!
Nimeisoma thread yako na michango toka kwa wachangiaji wengi..first and foremost nakubaliana na ile main objective ya thread yako "tunapaswa kubadilika" ingawa nina vingi vichache vya kuchangia pia ambavyo nitatofautiana na wewe.
Binafsi nakubaliana na wewe kuna vitabia ambavyo bila majority kubadilika hatutofika kwa ujumla wetu kama watanzania-embu chukua mifano michache tu kama vile kukojoa barabarani,magari kutofuata sheria na hatimaye kusababisha foleni kubwa zaidi ambayo mwisho wa siku hata asiyefuata sheria anaathirika na foleni hiyohiyo..Nimeshashuhudia mara nyingi tu uwanja wa Taifa mtu anaacha njia ya kupita uwanjani na anapanda juu ya viti na hakuna anayeona kama hilo ni tatizo-tunajiuliza ilituchukua muda gani kupata uwanja kama ule?..Kweli tunapaswa kubadilika hiyo haihitaji serikali bwana,sisi tunaoona hayo yakitendeka tunachukua hatua gani??

Lakini nakuja upande wa pili-popote duniani sheria ndio mama wa mafanikio yote:sheria zinazokidhi mahitaji yetu lakini kuhakikisha pia kuwa sheria hizo zinafuatwa na anayezivunja anachukuliwa hatua bila upendeleo wala kuonewa...Naamini kuna watu wasiopenda kuona mambo yalivyo kwenye maeneo yao-vitu kama uchafu (wa taka na vitu vingine),wanapenda kuwa na fence kama hizo za nyaya,au majani/michongoma n.k Lakini embu chukulia mfano mtu ana kiwanja ambacho kiko jangwani pale au Tandale kwa mtogole (naamini wanaofahamu maeneo hayo wananielewa nini naamanisha) taka utatupa wapi pale...ukipanda hayo majani utmwagilia na nini pale?chochote unachoweka nje kimekwenda na wapi utakwenda kushtaki??Hakuna sewage system pale ndio hayo ya vyoo na uchafu kutapakaa kila sehemu-Hapo sasa utaweza vipi kuiweka serikali pemebeni??Hapo hata kama mtu una nia nzuri kiasi gani hutoweza peke yako bila juhudi za dhati na za wazi za serikali.
 
- I mean nipo njiani hapa kwenye Treni, ninatokea Boston kurudi New York City, njiani humu ninajionea Wazungu masikini, lakini nyumba zao ni safi, maeneo yao ni masafi, nyumba za mbao na mabati lakini zimewekewa uzio, kwa majani senyenge, miti au hata waya tu kuzunguka nyumba!

- Na pia bara bara sio za lami, lakini zimepangiliwa na zinaonyesha Mlango wa mbele wa nyumba, kuna box la barua, sasa sisi Tanzania jamani tumemkosea nini Mungu? I mean uchafu, wanyama wanakimbia kimbia hovyo bila mpango, hujui mbele ya nyumba ni wapi na nyuma ni wapi?

- I mean haya mengine ni yetu wananchi sio ya Serikali bana, Tubadilike tukitoka hapa JF twende majumbani na kwenye society and do something to our Society please!,

- Tumezidi mno, tubadilike sasa!

Willie @ NYC, USA.

Unajua tunawatazama wazungu na ustaarabu wao na kudhani umekuja tu automatically bila kuwa na nguvu za ziada nyuma yake...na hapa ndio suala zima la serikali na utawala wa sheria linapokuja.

Leo hii utasema wazungu ni wastaarabu sana barabarani wakifika kwenye red light wanasimama hata kama ni usiku wa manane! Lakini ukitaka kujua chanzo cha huo ustaarabu jaribu wewe kupita kwenye taa nyekundu ukione cha moto!!

Katika masuala ya usafi ni vile vile...bila kuwa na mipango miji inayoeleweka, sheria makini n.k. ustaarabu wa usafi hauwezekani!! Umewahi kujiuliza kwa nini mji wa Moshi ni msafi? Jibu ni moja tu...SHERIA!! Hata ukitupa chewing gum barabarani unapata msukosuko!!
 
Hamna jiji chafu kama Amsterdam though wanaoishi kule majority ni wazungu. Uchafu hauna mzungu wala mwafrika, ni tabia ya mtu tu na saa nyingine kipato duni kinachangia.
 
- I mean nipo njiani hapa kwenye Treni, ninatokea Boston kurudi New York City, njiani humu ninajionea Wazungu masikini, lakini nyumba zao ni safi, maeneo yao ni masafi, nyumba za mbao na mabati lakini zimewekewa uzio, kwa majani senyenge, miti au hata waya tu kuzunguka nyumba!

- Na pia bara bara sio za lami, lakini zimepangiliwa na zinaonyesha Mlango wa mbele wa nyumba, kuna box la barua, sasa sisi Tanzania jamani tumemkosea nini Mungu? I mean uchafu, wanyama wanakimbia kimbia hovyo bila mpango, hujui mbele ya nyumba ni wapi na nyuma ni wapi?

- I mean haya mengine ni yetu wananchi sio ya Serikali bana, Tubadilike tukitoka hapa JF twende majumbani na kwenye society and do something to our Society please!,

- Tumezidi mno, tubadilike sasa!

Willie @ NYC, USA.

Na mabadiliko ya kweli kwenye maisha ya binadamu yanaletwa na mabadiliko ya individuals...kweli tuanze kubadilika haraka iwezekanavyo!
 
Back
Top Bottom