Wa Siku nyingi:NAACHANA na UWAKILI

ile thana ya kuwa na clean hands before the court kwa mawakili now days haipooooo! mawakili wanasimamia hata kesi za kijinga ambazo sometimes zinakandamiza haki ya mnyonge tena waaaazi kabisa.kiufupi hii profsn imeingiliwa,mtu akidaka mhuri tu ye anawaza dili apige hela naye awe na mkoko mkali,tena vijana wa sasa ndio balaaaaa.
 
TLS inahitaji uongozi mzuri wa kusimamia taaluma na kuipa taaluma sauti na msimamo. Kiwe chombo chenye kuonekana uwepo wake katika jamii.
 
Sio kingereza..tatizo ni kuwa hatuna namna tunaweza kuverify,that‘s why hata wewe unaweza tu kupost ukadai ni engineer.

Lakini kingine ukiangalia reasoning yake unaona syllogysm haiko sawa.Ok,kuna matatizo mengi katika taaluma hiyo,so what?
Hayo matatizo yanahitaji collective responsibility ama individual responsibility?

Yeye ni private practitioner ama la? Kama private practitioner wajibu wake ni nini? Angejua na kutimiliza asingekuja kupost hivo humu ndani.

Na kama sio, je job decription yake alipoajiriwa ni nini?

Anyways,he still has the benefit of doubt!

Ndo hayo mnayoambiwa......umeacha topic na unaanza kumjadili yeye....

Maoni yako nini juu ya hizo weakness mlizoambiwa????
 
Sasa kama Riz moko nae ni Wakili hii taaluma ni chaka bovu...mkiangalia ukweli wa mambo kama mtu ni mzalendo wa kweli kabisa mawakili hawa wangekataa kabisa kufanya utetezi dhidi ya majizi na mafisadi..ila sasa sheria imekaa kinafiki sana,,,maana inasema Every body is pressumed to be innocent until proven otherwise.....

Mawakili na Wanasheria wengi wanasaka ulaji, na TLS haina umoja wa mshikamano hata wao wana tuhuma kibao, sasa ukija kwa idara pacha ya hii yaani Mahakama baasi ndio kumeoza kunuka kabisa...sasa ukiwa mzalendo hutafanya hii kazi ila njaa ni noma...

Shivji ni prof mkubwa na msomi wa kweli ila hatetei mafisadi na wala hataki...
 
Hauna maana.Kazi yetu ni kutuna tu na mabegi yaliyosheheni nyaraka za kulinda wezi. Hapa Arusha(kwenye mkutano wetu wa Mawakili) hakuna la maana tunalolizungumza zaidi ya kutambiana kwa matumizi na magari ya kifahari.Heri yake Wakili Msomi Tundu Lissu ambaye muda huu 'anatutukana' kwa kutuita waoga na walinda vibovu.

Katiba mbovu;tuko kimya.Serikali mbovu;tuko kimya.Sheria mbovu;tuko kimya.Wananchi wanauawa;tuko kimya.Sisi ni wanafiki wakubwa.Hatufai. TLS,punde nawaleteeni ombi langu la kujitoa kwenye Orodha ya Mawakili(Roll of Advocates). Msinijuejue...

mkuu bora uache tunaokuja tupate nafasi
 
Back
Top Bottom