Wa-Africa weusi hatarini zaidi ndani ya Libya

H.O.V

Member
Jan 30, 2011
5
1
Wakati mataifa mbalimbali yakiendelea kuwaondoa raia wake kuwaepusha na vurugu za machafuko nchini Libya, wafanyakazi wahamiaji wengi wao wakiwa ni wa-Afrika weusi ni walengwa kwa sababu wengi wao ni watuhumiwa kwa kuwa vibaraka walioajiriwa na Muammar Gaddafi, kiongozi wa Libya.

Wafanyakazi kadhaa kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaogopa kuuawa, na mamia kujificha kutoka kwa raia wa Libya wenye hasira ya kupambana na serikali kwa kuwawinda "vibaraka weusi wa Ki-Afrika," kulingana na mashahidi.

Zaidi ya raia 90 wa Kenya na raia wengine 64 kutoka Sudan Kusini, Uganda, Zimbabwe, Lesotho, Zambia, Rwanda, Afrika Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sierra Leone na Burundi wametua mjini Nairobi Jumatatu hii, kulingana na viongozi.

"Tulikuwa tukishambuliwa na na raia wa Libya ambayo walisema kwamba sisi tulikuwa askari wa kukodiwa kwa ajili ya kuua watu. Labda niseme kwamba hawakutaka kuona watu weusi," Julius Kiluu, 60 msimamizi wa majengo, aliiambia Reuters.

"Kambi yetu iliteketezwa kwa moto, na tulisaidiwa na ubalozi wa Kenya na kampuni yetu kuweza kufika uwanja wa ndege," alisema.

Mashirika ya haki za binadamu yanasema kwamba maelfu ya wafanyakazi wamekwama katika makambi na nyumba zao binafsi zinalindwa na marafiki zao kutokana na serikali zao kushindwa kuwaokoa kutoka machafukoni.

"Lakini kwa nini hakuna mtu yoyote anayejihusisha na hatma ya wahamiaji kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika ndani ya Libya? Kama waathirika wa ubaguzi na unyonyaji, ndani ya Libya mazingira magumu zaidi. Wahamiaji wengi serikali zao zimeshindwa wala kuwapa msaada wowote," Hein de Haas ,Afisa mwandamizi wa Kimataifa toka Taasisi ya Uhamiaji, anaandika katika blogu yake.

Mwandishi wa Al Jazeera, Nazenine Moshiri, alikutana Seidou Boubaker Jallou, raia wa Mali, ambaye alisema aliikimbia Libya baada ya wahamiaji wengi wenye asili ya u-weusi kuanza kushambuliwa.

"Hali ni ya hatari zaidi kwa wageni kama sisi - na pia sisi watu weusi - kwa sababu Gaddafi kaleta askari kutoka Chad na Niger ambao wanaripotiwa kuuawa Waarabu," alisema.

Wataalam wanasema kwamba Gaddafi amekuwa na uhusiano kwa muda mrefu na wapiganaji wa Afrika ambao sasa walikuja kwa msaada wake.

Wafanyakazi wanaolipwa ujira mdogo

Mamia ya wahamiaji weusi kutoka mataifa maskini ya Afrika, ambao hasa hufanya kazi katika sekta ya mafuta nchini Libya kama vibarua nafuu, pia wamejeruhiwa katika ghasia hizo. Wengine walikuwa hawawezi kutafuta matibabu kwa hofu ya kuuawa.

Saad Jabbar, naibu mkurugenzi wa Kituo cha Afrika ya Kaskazini katika Chuo Kikuu cha Cambridge, anathibitisha Waafrika kuwa walengwa.

"Nawaambia, hawa watu, kwa sababu ya mpango wao, watachinjwa ndani ya Libya. Kuna mengi watu wengi wenye hasira dhidi ya askari hawa wa kukodiwa wale, ......." Jabbar alisema.

zaidi ya watu 1.5m kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara ni wahamiaji wanaofanya kazi ya Libya kama vibarua wa kulipwa kwa kima cha chini katika sekta ya mafuta ya viwanda, ujenzi, kilimo na huduma ya jamii.

Mashirika ya haki za binadamu yanasema baadhi ya waandamanaji wanaopambana na Gaddafi wanawahusisha isivyo sahihi wafanyakazi wa wenye asili ya Afrika katika vurugu hizo.

"Wahamiaji wa wenye asili ya Afrika sasa wanahusishwa na vurugu na mauaji ya umati, na sisi tunahofu zaidi juu ya vurugu ambazo zinaweza kufuata hasa baada ya Gaddafi ni kuondoloew madarakani," alisema Haas.

Kutokana na kupuuzwa na serikali zao, wafanyakazi wa wenye asili ya Afrika ni moja ya makundi ambayo yako katika mazingira magumu zaidi ndani ya Libya kwa hivi sasa. Wachambuzi wanasema kama hatua ya kuzuia hali hii hatachukuliwa, ipo hofu kubwa ya umwagaji damu.

"Nadhani kuna umuhimu wa kufanya haraka juu ya jambo hili, vinginevyo, mauaji ya kimbari dhidi ya mtu yeyote mwenye ngozi nyeusi na ambaye hawezi kuongea Kiarabu fasaha yanawezekana," alisema Jabbar.
 
Tatizo ni kwamba nchi nyingi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara hazina takwimu sahihi kuhusu raia wake walio nje ya nchi zao. Balozi nyingi za nchi hizi zipo bila msaada wowote. Tumesikia nchi nyingi sana za ulaya na asia zikiwaondoa raia wao nchi Libya ila sijasikia hata siku moja nchi nyingine toka kusini mwa Africaikifanya hivyo. Nina wasiwasi na balozi zetu katika mataifa ya nje. Kama watanzania inabidi kujifunza kitu hapa. Je serikari inatujari?
 
Back
Top Bottom