W J Malecela kwa hili la wizi na kutokuwajibika kwa mawaziri ungekuwa upande gani?

Labda ungependa kujiridhisha vilevile kuhusu Senators wa USA.

Soma hapa webpaGES zifuatazo na nyingine ambazo zinaonyeshwa mwishoni: List of United States senators expelled or censured - Wikipedia, the free encyclopedia ; List of federal political sex scandals in the United States - Wikipedia, the free encyclopedia ;

Utaona ni kwa kiasi gani unayotuambia siyo kweli. Wanasiasa wengi wa USA walijiuzuru, au walilazimishwa kujiuzuru, na kisha kushtakiwa au kutoshtakiwa.

Splendid indeed Mr. KVM, Mkuu wala usipoteze muda kumuelimisha jamaa huyu, mimi nimejaribu ku-analyse majibu yake humu nikagundua kitu ambacho ntakieleza hapo baadae. Hivi huyu jamaa si amewahi kuishi Merikani? Kama ana nia na wito wakua mwana siasa, anashindwaje kujua by heart wanasiasa wa USA walio wahi kujiuzuru kutokana na kashfa mbali mbali, ambazo nyingine walikuwa awahusiki nazo moja kwa moja, lakini kwa kufahamu umuhimu wa kuwajibika wanajiuzuru hata kabla ya kuandikiwa barua ya kuwalazimisha wahachie ngazi!

Sina shaka mwenzetu huyu amewahi kusoma/kusikia kashfa za links tajwa hapo juu, na anajua fika kwamba anacho tueleza humu siyo kweli au labda ajuhi kazi za CAG ni nini! Yaani nimeshindwa kumuelewa anacho jaribu kutetea ni nini, je haya anayafanya kimakusudi au aelewi vizuri hali tete inayo likabili TAIFA letu.

Wana JF wamejaribu sana kumuelimisha lakini sioni kama kazi hii imezaa matunda.Ukisoma between the lines majibu yake utaona ana malengo fulani ya kutaka ku-please kundi fulani hili aonekane ni mwezao au akubalike - I am sorry kulisema hilo, vile vile ukumbuke hapa tunajadili hatma ya taifa letu siyo michezo ya kuigiza; msikilize JK alichozungumza leo kuhusu matumizi mabaya ya fedha za UMMA nk, JK ni mwelewa wa mambo ndiyo maana amekazania kuimarisha ofisi ya CAG - kama JK ange-entertain ushauri/mawazo kama ya kwako basi mawaziri waliotajwa na CAG wange endela kupeta TU - je hilo ndilo TAIFA tunalo litaka sisi? jibu unalo.
 
Back
Top Bottom