Vyuo vikuu kama shule za kata

Hivi Waungwana niulize tu, UDSM ilianza na wahadhiri wangapi 'wenye qualifications"na je, the other scenario, Kama isingeanzishwa UDOM, hao wanafunzi almost 18,000 wangekuwa wapi sasa hivi given the current capacaity ya public universities, na ada 'za kuruka' za vyuo vikuu binafsi?Kweli kuna mtu angetegemea, as from 2007, chuo kiwe kimeshajitosheleza kwa wahadhiri wenye qualifications, madarasa pamoja na mabweni, maktaba, vitabu vya kutosha nk?Isnt it nice to start somewhere? Ninavojua mimi, kwenye chuo kikuu kuna mchanganyiko wa wahadhiri...kuanzia tutorial assistants hadi maprofessa. Kinachoonekana sasa hivi ni kwamba maprofesa wengi wanaelekea kustaafu na hili linasababishwa na sera ya serikali (au ya WB) miaka ya 90 kufreeze ajira. Sasa wakiajiriwa wahadhiri ambao watajiendeleza wakiwa tayari kazini, at the same time kukiwa na back up ya wahadhiri kutoka nje, kuna tatizo gani?Au tunadhani kuwa vyuo vikuu "vinashuka' tu kama mana jangwani, havi-evolve over time? Unapolinganisha kwa mfano UDOM na UDSM ambayo ilianza 1964, nadhani inakuwa sio fair ....vyuo vingine duniani mfano Cambridge ni vya tangu karne!
Nakuunga mkono met. Tatizo letu sisi watanzania huwa tunatarajia makubwa kwa mara moja na hii inatokana na kutoruhusu upeo wa uelewa kuwa na mawanda mapana ya fikra. Siku zote huwa tunafananisha mbuyu na mchicha bila kuhusisha umri wao, ustahimilivu na uwezo binafsi.Hata mtoto akizaliwa huwa anaanza kuendele kukua na kukomaa sehemu muhimu kwanza na baadae sehemu zingine kuendelea kuongezeka na kuimarika sasa tukitaka mtoto azaliwe na kukua na kutembea siku hiyo hiyo si tutampindisha mgongo na miguu itakuwa na matege...hebu tujaribu kuruhusu mabadiliko yachukue nafasi yake kwa utaratibu na uwezo husika wa kiuchumi, tukilazimisha sijui kama tutafika malengo halisi ya Elimu kama ambavyo wenzetu wamefikia. Halafu siku zote msomi unapotoa hoja huwa inasindikizwa na mapendekezo madhubuti ya kufanikisha utatuzi wa changamoto unayoiwasilisha na sio kutoa lawama tu...!Bravo Kaizer!
 
Acheni watu wasome, hayo ndo maendeleo yenyewe. Nyie mnataka mwe na chuo kimoja kama cha enzi zile??Acheni hizo, na uhakika mtu aliyefika chuo kikuu hata kama kipo chini ya mwembe ana uelewa mkubwa wa kupambanua mambo kuliko yule wa LY.
uwezo mkubwa kupembunua mambo kama kumchangia Jk million 1 ya uchaguz? Hebu fkiria eti chuo kikuu anamalza miaka mitatu hajui nn maana ya field, wakat hata vyuo vya hotel management, tourism and tour guiding vya magomeni, kariakoo na buguruni wanafanya field
 
Ni mwanzo, mara nyingi mwanzo wa kitu chochote huwa mgumu, serikali kuanzisha vyuo vikuu haija kosea. Hiyo ni hatua ya kwanza kuwa na taasisi, halafu baadaye kuwa na walimu wenye sifa. Isingekuwa hekima (kwa mawazo yangu lkn) kusubiri kuwa na walimu wenye sifa, halafu ndiyo kuanzaisha taasisi. Hapa tulipo si pabaya, hayo ulioongelea hapo juu ni marekebisho tu, na si ya msingi, walimu watapatikana tu, na ndiyo maana serikali imeanza kuajiri ma-dr na ma-prof toka sehemu yoyote ya dunia.
Ondoa shaka, Roma haikujengwa kwa siku moja, vivyo hivyo, vyuo vyetu havitaimarika kwa siku moja, ni mchakato. cha msingi ni kuwa na mipango na mikakati ambayo inazingatiwa na kufuatwa.

Hivi ni lazima kila kitu kitetewe, hakuna kujaribu katika elimu you either do it correctly or miss it forever, hawa wataalamu wanakwenda kutumikia umma upi? watashindana na nani? kwa hilo tumekosea kwani tumeanzisha kimkandamkanda harafu tunaziendesha kimkandamkanda shughuli za elimu, we are destroying this nation, we are blowing our own people, we are building unequal society by condemning poor families while our children are being given the best opportunity that gurantees them quality education. They have deliberately prepared their children to be our children's leaders

Singependa kuishi nishuudie watanzania wakichinjana kuondoa madaraja tunayoyatengeneza leo kwa mfumo wa elimu

aluta contnua
 
uwezo mkubwa kupembunua mambo kama kumchangia Jk million 1 ya uchaguz? Hebu fkiria eti chuo kikuu anamalza miaka mitatu hajui nn maana ya field, wakat hata vyuo vya hotel management, tourism and tour guiding vya magomeni, kariakoo na buguruni wanafanya field
Unaongea saaaana bila kujua hali halisi. Hivi nani kakwambia kuwa wanafunzi wote wa udom ni wana ccm?? Fatilia mambo kwa ukaribu sio kukosoa tu. Wanataaluma wapewe heshma yao.
 
Nivizuri kuanzishwa kwa UDOM kutokana na population yetu na hitaji la wataalamu kuendana na wakati. NinavyoelewaTanzania kuna tume inayosimamia viwango vya programs na mitaala (acreditation) yake kabla ya kuruhusiwa kufundishwa. Tume hii inaitwa Tanzania Commission for Universities (TCU), na hivi karibuni ilikuwa inahakiki waalimu wote vyuo vikuu hata vile vya binafsi. Nikweli pia tunauhaba wa waalimu hata kwenye vyuo vikongwe, hii pia ilichangiwa na kusimamishwa kwa ajira miaka ya 90 na kwasasa ni maslahi duni hivyo watu wenye sifa wengi hawavutiwi kwenda kufundisha. Inasikitisha mshahara wa Professor ni wa chini zaidi ya mara tatu wa mkurugenzi mahali mwenye BSc. na ni sawa na wa wafanyakazi kwenye sehemu nyingi wenye BSc hata kwenye vitengo vya serikali. Ikumbukwe pia kuna kazi kubwa ili uweze kupanda daraja, kwanza uongeze kiwango cha elimu, usimamie wanafunzi projects ama supervision kwenye Mastares/PhD, na pia uweze kupublish kwenye international journals, kuandika vitabu nk. ambazo ndizo zinakupa points za kupanda daraja. Zaidi inabidi ufundishe, usahihishe (fikiria unawanafunzi kama 600 kwa uchache), hivyo inahitaji ujitoe kwelikweli ili uweze kufundisha, kusimamia wanafunzi projects na kufanya tafiti zitakazokuwezesha kupanda. Sasa kulingana na maslahi madogo, wengi wamekuwa wakienda kwingine ambapo hakuna adha kama hizi. Swala la Mtu mwenye MSc (Assistant lecturer) kufundisha BSc inakubalika, na huwa bado anajengwa na seniors wake, ila la TA kufundisha na kuhitimisha course mwenyewe huwa halipo kwenye miongozo ya vyuo vikuu. Huwa napata uchungu sana ninapopata takwimu za wahadhiri wetu wengi wanaofanya kazi nzuriza kimataifa nje ya nchi. Wengi wapo huko kwa ajili wanawajali na wanapewa Maslahi mazuri. Hebu fikiria walivyomfukuza Prof. Baregu pale UD wakati akihitajika sana kufundisha wanafunzi pamoja na wakufunzi wachanga, unafikiri inatoa picha gani kwa wakufunzi vijana? Kweli nakubaliana Siasa inauwa vyuo vyetu, si UDOM tu, hata UD na SUA ingawa sina hakika na MU. Tatizo lingine kubwa, licha ya maslahi duni ya wahadhiri wetu, bado serikali inatoa mchango mdogo sana (chini ya 1%) kwenye maswala ya TAFITI. Hivyo tafiti nyingi zinazoendeshwa vyuoni ni donor driven objectives, hili hufanya wataalamu wetu hawa tusiwatumie vizuri kwa matatizo yetu ya ndani na kufanya jamii isione mchango wao katika maisha ya kilasiku. Pia la mwisho nililoliona ni kuwa bado hakuna freedom kwa wahadhiri, unapokuwa realistic maranyingi unaonekana mchochezi, tena wahadhiri walio kwenye fani za Political Sciences ama Development Sciences. Wakifanya kazi zao vizuri ndiyo wanajijengea uadui mkubwa na serikali. Nafikiri imefika wakati, serikali izidi kuwekeza kwenye vyuo vyetu ili kuzalisha wataalamu wetu wanaokidhi na kupata majibu ya matatizo yetu ya msingi yanayohitaji utafiti. Napenda kumalizia kwa kusema, rasilimali watu ndiyo rasilimali ya kwanza katika nchi yoyote inayoendelea. Huwa tunajivunia kuwa na rasilimali za asili wakati zimeshindwa kutunufaisha sababu ya kutozitumia ipasavyo. Nilimuuliza Mjapan mmoja mwaka 2006, kwamba ni rasilimali gani wanayoitegemea kwa kiwango kikubwa katika kujenga nchi yao, alinijibu kirahisi sana kuwa ni WATU. Nchi ile ndogo kuliko TZ ina watu 127 milioni, inaviwanda vingi vinavyotegemea malighafi kutoka nje, na pia wataalamu wao wengi wanafanya kazi nje ya japani bila mizengwe. Sisi tuna malighafi ze kutosha ndani ya nchi yetu ila kutokana na kutokuwa na wataalamu wa kutosha pamoja na mifumo mibovu tumeshindwa ku-mobilize hizi resources tulizojaliwa na mwenyezi Mungu ili zitusaidie. SAsa imefika wakati, wasomi, wanasiasa na viongozi wote kwa ujumla tuwe na mtizamo chanya usio wa kibinafsi katika kuendeleza nchi yetu nzuri TANZANIA. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Elimu gani hakuna field? Udom kati ya course 43 za social science 13 tu ndo zinaenda field,just imagine Economics,poject planning management na community development,statistics,hawana field ila Ba Kiswahili wanayo,au kwa sababu Mlacha ni prof wa Kiswahili
Kwa nini watanzania hawataki kuongelea mambo ya msingi kwa undani. Mfano elimu ya chuo kikuu leo inafanana na ya shule za kata. wakubwa wanatamba majukwani wameanzisha vyuo vikuu vingi kama UDOM. lakini hawaoni matatizo yaliyopo kwenye vyuo hivyo.Hakuna vifaa,Hakuna Maprofesa,majengo hayatoshi. Watu wenye Masters ndio walimu ambao nao wamesoma kwa kuunga unga tu. vyuo vikuu vya namna hii vitatufikisha wapi. Mtoto kafaulu kwa kubahatisha darasa la saba halafu kaenda shule ya kata kafaulu kwa kukairiri kaenda chuo kikuu UDOM. Hapa kweli tutasema tumezalisha msomi wa kuiomboa nchi hii katika ulimwengu huu wa utandawzi, soko la pamoja nk. Tanzania inaelekea pabaya. lakini viongozi wetu wanafurahia sifa rahisi rahisi. Wanchi nao wamelewa fikra za kipumavu za zidumu fikra za mwenyekiti. Taifa hili linahitaji mwelekeo mpya . we are in wrong boat and wrong direction.
 
Kaizer,
Ningependa kukujibu kuwa UDSM ilianza ikiwa na waalimu wengi tu wa kutosha kutoka Uingereza, Jamaica, na kwingineko waliokuwa well qualified. Wakati huo serikali ilijitahidi sana kuajiri the best minds there was in the academic world. Sizo hizi porojo za sasa za kujenga UDOM bila kufanya maandalizi stahiki na juzi namsikia mkulu wa CCM akijidai kuwa mwaka huu waalimu elfu 15 wanafuzu masomo. UDSM ya 60-70 ilikuwa an intellectual oasis.

JASUSI imenena kweli. Ubovu wa vyuo vya Tanzania ni mpaka UDSM. Hao wanosema UDSM ilianzaje nitawaambia kweli hapa. Wakati ule kulikwa na miamba kama Professor Wamba Dia Wamba. Na Professor Walter ambae lijitabu lake titled, "Hiow Europe Underdeveloped Africa" lilitikisa dunia mpaka aliwekewa bomu kwenye gari lake na kuuawa alipofungua kuingia. Kamwe usiwafananishe hawa watu na akina Dr Bana. Hawa watu ni vilaza walioingia UDSM kwa milango ya ndugu zao na hiki ndio kiliuwa UDSM. Watu walikuwa wanaingizwa kindugu chuoni na serikali ikaacha kuajiri waadhiri toka nje. Hebu niambie mtyu kama Bashir alieko kwenye department ya public administration ambae anazeeka na masters yake miaka nenda rudi kama mwalimu msaidizi pale UDSM. Zamani ilikuwa ikipita miaka fulani bila mtu kuwa promoted alikuwa anafukuzwa. Ndio maana Dr Lamwai alifukuzwa (japo kulikuwa na politics pia) maana alikuwa Dr kwa miaka mingi kupita. Bila mabadiliko Tanzania vilaza watazidi. La muhimu ni kurudia kuajiri waadhiri wakimataifa na kuhakikisha kuwa sheria za chuo kama kuwapa wahadhiri wajibu wa ku-publish papers nk lazima zifuatwe.
 
Kwa nini watanzania hawataki kuongelea mambo ya msingi kwa undani. Mfano elimu ya chuo kikuu leo inafanana na ya shule za kata. wakubwa wanatamba majukwani wameanzisha vyuo vikuu vingi kama UDOM. lakini hawaoni matatizo yaliyopo kwenye vyuo hivyo.
Hakuna vifaa,Hakuna Maprofesa,majengo hayatoshi. Watu wenye Masters ndio walimu ambao nao wamesoma kwa kuunga unga tu. vyuo vikuu vya namna hii vitatufikisha wapi.

Mtoto kafaulu kwa kubahatisha darasa la saba halafu kaenda shule ya kata kafaulu kwa kukairiri kaenda chuo kikuu UDOM. Hapa kweli tutasema tumezalisha msomi wa kuiomboa nchi hii katika ulimwengu huu wa utandawzi, soko la pamoja nk. Tanzania inaelekea pabaya. lakini viongozi wetu wanafurahia sifa rahisi rahisi. Wanchi nao wamelewa fikra za kipumavu za zidumu fikra za mwenyekiti. Taifa hili linahitaji mwelekeo mpya . we are in wrong boat and wrong direction.

Kikubwa zaidi viongozi walioko kwenye chuo hicho ulichobold kwao taaluma si kipaumbele na ndio maana hata wanafunzi wao hawataki waende field practicals wakizidai wanaitiwa polisi na kufukuzwa kwa kudai elimu inayowastahili.

Kama hiyo haitoshi ulishapata ama pata nafasi uzungumze na wahadhiri wao unaowataja hapa wakueleze yanayojiri kwao wenyewe na stahiki zao ukilinganisha na wenzao wa elimu kama yao wa vyou vingine ama hata walioajiriwa nao
 
WanaJF tunaonekana kama watu wa visasi na mipasho,coz kila mada inayoanzishw inalenga direct kuishambulia UDOM,hamleti mada za kuchambua matatizo na kuyataftia soln,hii haitusaidii chochote kama great thinkers
 
naomba hii thread iunganishwe na thread nyingine kama hii kule jukwaa la elimu,topic za UDOM zinachosha
 
Kweli kabisa wadau UDOM ni bomu la kufa mtu. Mimi ni Afisa Utumishi Shirika fulani hapa nchini lakini najua kabisa kuwe ukiajiri mwanafunzi kutoka UDOM utakuwa na kazi ya ziada ya kumwelekeza kupita kiasi kulinganisha na vyuo vingine sijui tatizo nini jamani wanatia huruma sana. Yaani hata kumwelekeza ajibu barua ya kiofisi tu lugha atakavyoichakachua utakaa chini usikitike. Mimi naona UDOM kuna tatizo la msingi zaidi tunavyofikiria kwani haiwezekani mtoto graduate awe kila vile kazini. Nakubali mtu huanza kazi kwa shida kwa sababu ya uzoefu lakini unategemea baada ya muda at least abadilike basi lakini kwa hawa UDOM ndugu yangu hakuna kitu. Mimi nikishaona kutoka UDOM basi naanza kujisikia huzuni walivyo vilaza.
nakufahamu mh. We c afisa utumish wala nn,ila ntakutafuta ili 2onge vzur,maana ts too much
 
Tuna tatizo kuwa Utawala wetu unaangalia vigezo vya sera za mabwana wakubwa [World Bank na IMF]. Ukubwa wa tatizo la watawala wetu ni KUTOKUWA NA DHAMILA YA DHATI NDANI YA MIOYO YAO.Nikimaanisha KUJISIKIA KUWA MUNGU AMEKUITA UWE KIONGOZI ILI KUONYESHA UWEZO WAKE KUWA UMEYABADILISHA MAISHA YA MTU MWINGINE NA KUYAFANYA BORA ZAIDI TOKA HATUA MOJA KWENDA NYINGINE.

Viongozi wa SIASA za sasa wamebweteka na TAARIFA za Wakubwa.Hivi Tanzania ya Mwaka Sitini na sabini sio ya leo.Kuna idadi kubwa ya kundi la watoto waliozaliwa miaka ya themani na Tisini hawa hatima ya maisha yao ya mbele [Future] inatizamwa kwa jicho gani?Leo watoto hao wako chuo Je shule walizopita nazo je zilikuwa na ubora?.Wakati watoto hawa wanazaliwa kulikuwa na takwimu kwenye Mahospitali yetu, siitegemei Serikali ishindwe kujua kuwa HAIKUWA NA PLAN toka watoto HAWA WANAZALIWA.Kuwa watoto waliozaliwa miaka hiyo kumi kumi ya kutofautina Serikali isingekuwa na maono ya kuandaa mazingira kuwa kizazi hicho kinachokuja kitaitaji Shule za Msingi,Sekondari na Vyuo Vikuu vingapi ukizingatia takwimu za miaka hiyo ya 1980 na 1990.Yaan kwa ujumla Serikali ilikuwa na Miaka zaidi ya ISHIRINI kuweka mazingira toshelezi kukabiliana na ukuwaji wa sekta zote muhimu kuanzia Elimu,Afya nk.

Iweje mtu akukataze kuziba UFA wa NYUMBA YAKO nawe UKUBALIANE NAE.Jamani kwani tusione kuwa WORLD BANK NA Kaka yake IMF ni watu wasio tutakia MEMA, tujifunze kupitia misimamo ya Mwalimu jamani kuhusu makampuni hayo mawili ya Dunia.

Tanzania tunaitaji KIZAZI CREATIVE,kitakacho thubutu KUWEKA KANDO SERA WORLD BANK NA IMF, ZISIZO NA TIJA NA KUBISHANA NAO KWA HOJA.WAKIGOMA KUAFIKIANA NA MAAMUZI YETU KWA MUJIBU WA MAZINGIRA YETU NA HALI YET HALISI TO HELL NA PESA ZAO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.TUTAKOPA KWA WACHINA NA RUSSIA.
 
Back
Top Bottom