Bakari Maligwa
Member
- Aug 18, 2010
- 65
- 22
...Inawezekana kwa kiasi fulani vyuo vyetu vikuu vikafanana na shule za kata. Hata hivyo, kufanana kwake kunakwenda mbali zaidi kutokana na ukweli kwamba:
- Vyuo hivyo vimegeuzwa kuwa vituo vya upigaji wa siasa badala ya kuandaa wataalamu wenye maarifa, ujuzi na maadili ya kitaaluma katika kuleta maendeleo;
- Vyuo vikuu vinatumika kwa maslahi ya maprofesa waliyesoma zamani kwa kupata fursa adimu za kusoma elimu toshelezi na si ya kuungaunga kama wanayopata walimu wa siku hizi;
- Maprofesa wamekuwa wakikimbizana na siasa badala ya kufundisha, kutafiti na kutoa huduma za ushauri elekezi kwa umma na wananfunzi ili kuwajengea uwezo wa kitaaluma; na
- Vyuo vikuu vingi vimefanywa kuwa vituo vya kueneza propaganda badala ya kukuza maarifa na uwezo wa wanafunzi kukosoa na kujenga hoja zenye akili.