mimi ni mmojawapo wa wanachuo UDOM ila ninijilaumu na kuilaumu nafsi yangu kwa kuwa UDOM kwani nilipata nafasi katika vyuo vitatu UDSM,SUA na UDOM nilishawishika kujiunga na UDOM baada ya kuelezwa na ndugu zangu na rafiki zangu kuhusu sifa za chuo hiki kumbe ni maneno ya kisiasa tu maneno matamu kumbe ubora hakuna kabisa, hii inatia uchungu kwa wapenda maendeleo, hali halisi ndani ya UDOM ukifika utalia
1.hakuna uhuru wa kujieleza, udikteta na u ccm umeezidi, ukitoa wazo zuri wanafikiri wewe ni mwana chadema na unatafutiwa zengwe kufukuzwa, wanachuo waliofukuzwa chuo mwaka juzi wengi ni wana chadema na wasiokuwa na kadi za ccm,kwani kipindi nimewasili chuoni katibu wa ccm kitivo cha elimu alinifuata anipe kadi ya ccm kwa madai kuwa wana ccm majina yao yanapelekwa kwa mkuu wa chuo na hawawezi kufelishwa au kufukuzwa ikitokea mgomo
2.watu wanaosoma kozi za biashara hawakuwa na semina badala yake wamefundishwa kupitia lecture na walimu ambao wanasoma masters udom hii ni aibu kwani walikuwa wakilipua mfano mtu anafundisha hesabu kwa projecta hii inasikitisha
3.kutumiwa kisiasa na wanasiasa kama shabiby, huyu alileta mashati ya ccm pamoja na magari kubebea wanachuo wakaandamane<mimi maandamano huwa ni hiari>kumpokea kikwete pamoja na kumchangia pesa ya kuchukua fomu huku vijijini kwao watu wakifa kwa njaa na shida ya maji hii itapelekea kutengeneza wasomi wapumbavu
4.kutokuwa na haki sawa kisiasa mfano wana ccm huweka matangazo yao na kugawa kadi bila kubugudhiwa lakini kwa chadema ni kosa
5.kukosewa kwa matokeo mara mkwa mara mfano leo mtu ana D anaenda kulalamika anapandiswa daraja au kushushwa kama akibishana na wakubwa
6.mkuu wa chuo bwana kikula kutukana wafanyakazi kuwa wote wako kwa ajili ya dhiki kwani wamepeleka CV ila yeye kachaguliwa na raisi,pia kuwaita wanafunzi wana haramu baada ya kudai haki yao ya kupewa field
7.chuo hakina mtaala wake kwani kina kopi UDSM na vyuo vya nje
8.kuchaguliwa wanafunzi wa HKL kusoma kozi kama B.COM na BBA ambapo kimsingi hawakustahili kuzisoma
Kumbe ni tatizo lako la u coservative. teh teh teh, Sio tatizo la UDOM. Kuna senteso umesema yani inazifanya hoja zako zote kua zero.