kweleakwelea
JF-Expert Member
- Nov 29, 2010
- 3,066
- 1,535
Vyuo vikuu Chadema waja na `washa taa mchana`
Na Gideon Mwakanosya
22nd March 2011
B-pepe
Chapa
Maoni
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Vijana wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamezindua kampeni waliyoipa jina la washa taa mchana, itakayoendeshwa nchi nzima, yenye lengo la kuleta ukombozi wa kifikra kwa wananchi.
Akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jana mjini hapa, Mratibu wa kampeni hiyo mkoa wa Ruvuma, Likapo Bakari, alieleza kuwa taa hiyo itawashwa rasmi Machi 26 mwaka huu, ikiwa na lengo la kumulika na kuangaza katika kila mkoa nchini ili kuleta ukombozi kwa Watanzania
Alisema kuwa, ukombozi huo utakuwa katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa na kwamba itaanzia mkoa wa Ruvuma kwa kufanya mikutano mbalimbali ya hadhara katika kata zote za Manispaa ya Songea, kwa kutoa elimu ya uraia kwa wananchi wa eneo husika ili waweze kuzijua haki zao, kuzitetea na kuzidai.
Aliongeza kusema kuwa, kupitia mikutano hiyo pia watahamasisha jamii namna ya kutumia vizuri rasilimali za taifa katika kujiendeleza na kujiongezea kipato na kuwaelimisha maana ya katiba ya nchi na umuhimu wa kudai katiba mpya.
Akizindua kampeni hiyo, Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Ruvuma, Joseph Fuime, alisema maendeleo yoyote hayawezi kufikiwa bila ya kuwepo kwa siasa safi, hivyo wameanzisha kampeni hiyo itakayoendeleza, kukuza na kukitangaza chama kila kona ya nchi na kufungua matawi mapya.
CHANZO: NIPASHE