Vyoo vy UDSM vinatia aibu

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
2,653
264
Eti kweli udsm imeshindwa kulitatua tatizo la vyoo? ukiingia baadhi ya vyoo utakuta hali ya ajabu. utakuta maji mpaka nyayoni yametnda huku yakiwa na uchafu mkubwa. kwa mfano kile choo cha idara ya maths , kinatia aibu
 
Pale inatakiwa overhauling kali, nimesoma pale miaka minne lakini hali ni kutisha kadri siku zinavyosonga mbele. Inatia aibu sana kama hakuna la maana sehemu yeyote!!
Maji bado tunabahatisha kuyapata,
umeme bado tunabahatisha,
elimu bado kabisa pamoja na kufahamu umuhimu wake,
barabara/miundo mbinu kwa ujumla bado,
utendaji wa kila sehemu ndo hivyo tena.

Pamoja na kufahamu yote hayo kuwa yana umuhimu bado viongozi wetu hawataki kuona umuhimu wa makusudi/kujitoa mhanga ili kuokoa jahazi kwamanufaa ya taifa mbeleni.
 
Chuo kilikua planned kwa watu wachache but siasa zimeingia vyuoni sasa mmejazana hapo mchawi hajulikani...poleni but naona kuna vichaka vingi pale ( just kidding) Christmas Njema
 
Pamoja na kufahamu yote hayo kuwa yana umuhimu bado viongozi wetu hawataki kuona umuhimu wa makusudi/kujitoa mhanga ili kuokoa jahazi kwamanufaa ya taifa mbeleni.
Jinamizi la maji na uchafu wa vyoo hapo UDSM limekuwapo tokea enzi za adamu na hawa. Nilisoma hapo 1980-84, hilo lilikuwa tatizo ambalo hata Sokoine au mchonga na akina Kuhanga wenyewe hawakuweza kulipatia dawa!
 
Semeni wengine maana sisi tukisema....

Kule kwenye jukwaa la elimu mh. Rutashubanyuma kabandika mada kuhusu uhaba wa vitanda UDSM kwa zaidi ya asilimia sitini ya wanafunzi wake.....
 
Katika mambo yanayonishangaza Mlimani ndo hayo.Yaani hata vyoo tutegemee wafadhali jamani.Kweli haiwezekani kuwa na chanzo cha ndani cha fedha kujaribu ku-fix baadhi ya matatizo madogo madogo kama haya?Wakuu wamebaki kuendesha ma VX tu na wanashindwa kutatua mambo madogo ya namna hii.

Kwa mfano unaingia kwenye Computer Lab...Computers hazifanyi kazi wanafunzi wanaomba kuzi-fix ili zifanye kazi(hao ni CS students)...administrators wanasema subirini tuone inakuwaje...mwisho wa siku kampuni binafsi inakuja kufanya hayo marekebisho na kuchukua mshiko...hivi huu si ufujaji wa pesa?Je,tusingeweza kutoa mwongozo kwa wanafunzi na technicians wa chuo wakafanya baadhi ya haya mambo ili kupunguza gharama jamani?
 
Tatizo la vyoo UDSM limezidi kwa kweli kama ni TUNZO wanastahili NOBEL PRIZE kwa vyoo kuziba na kujaa, yaani ukibanwa tumbo la kuhara UDSM (Main Campus) ujue utajiharia peupeeee!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom