Vyombo vya habari vya umma na siku tatu za maombolezo

Hakuna muungano ktk vyomdo vya habari, kila chombo chatangaza lwake. Angalau channel ten walijitajidi. Hata wananchi wenyewe hatujaguswa kivileeee maana mfano jana, miss tz kama kawa, burudanio nyingi dar kama kawa. Muungano wa mchanga ule aliochanganya nyerere si muungano kamwe!
 
Tunavyombo vya habari, ilimradi naona tbc hapa wanaonyesha igizo la kibongo huku wanapitisha maandishi kwamba tutawaletea taarifa za kuzama meli kadri zitakavyo jiri. Vyombo vingine kama itv,chanel 10 na star tv wanaendelea na program zao kama kawaida hukuna jipya.
 
Mkuu wa kaya hakiamini alichokise, wanajua hamaanishi anachosema ndio maana wanapuuzia.
 
nimeguswa mno
but kuomboleza kwa staili ya kifo cha nyerere sikubaliani...
hata kifo cha nyerere sikupenda kuomboleza vile

KWAKO KUOMBOLEZA NI NINI???

Ukienda kumwona rafiki yako labda amefiwa na baba au jamaa yake kawaida unampa pole, pili unapata nafasi fupi hata ya saa moja hivi kwa maongezi kidogo ambayo yatahusisha taarifa fupi ya marehemu tangu kuugua au kama ni ajali, je ilkuaje, vitu kama hivyo. Kisha pamoja na waombolezaji wengine mtajaribu kuangalia taratibu zingine zinavyokwenda, maandalizi ya mazishi, je kuna mahitaji yapi, je kuna kusafirisha nini na mtaendelea kujadiliana mpaka mwisho wa swala zima kuwa limefanikishwa na kisha kuagana au kuwekeana taratibu zingingine za kufuata kufuatana na tatizo lenyewe.

Hiyo ni level ya kifamilia, vipi unaonaje mnapokuwa na msiba kama hu wa kitaifa na vyombo vyenu vya habari viko kwenye ndombolo?? Re-call tukio la juzi hapo Marekani, halafu tafakari tuanachokifanya sisi, naamini akili yako inachakachua vizuri si lazima uelekezwe kila kitu. Au ulifikiri mtoa 3d aliposema kuomboleza alilenga kulia na kutoa machozi?

Na wala hajasema style ya Nyerere hiyo umesema wewe, japo kwa mtu mwenye kuifahamu historia ya Nyerere na Tanzania kwa ujumla hawezi kushangazwa au kuchukizwa na style ya kilio/maombolezo ya kifo chake - That was unstoppable explosion of its kind, na wala haikuwa na ushawishi wowote kutoka kwa mtu au maelekezo ya kusema watu waomboleze hivi au vile. Na kwa taarifa tu usitegemee kuona tena maombolezo ya STYLE YA NYERERE TENA HAPA TANZANIA labda ikitokea kila familia ikaondokewa na mtu vinginevyo NEVER AGAIN!!!
 
Ila kuna haja ya kuangalia upya hizi ajali kubwa zinazo ua watanzania wenzetu zinatokea vp. Mimi nimeshitukia kitu.
26/5/1996. Mv Bukoba ilizama na kuua mamia ya watanzani. Hii ilikuwa baada ya uchaguzi wa 1995. Hali kadhalika mwaka 2001 treni iliua tena mamia ya watazania wenzetu Dodoma pia hii ilikuja mwaka baada ya uchaguzi wa 2000. Haya tena 10/9/2011 meli imezama Zanzibar na kuua tena mamia ya Watanzania hii nayo imekuja mwaka mmoja baada ya uchaguzi wa 2011. Mi nadhani kuna haja ya kuangalia upya hizi ajali isije ikawa watanzania wanatumika kufanikisha maslahi ya watu flani.
FIKIRIA CHUKUA HATUA.
 
Nilitegemea tbc wangekuwa msitari ya mbele kuunga mkono tangazo la mkuu wa kaya. Cha kushangaza hakuna cha maombolezo wala nn. Sijui ni kutomwelewa mkuu wa kaya au nyodo kwa tunaowalipa posho?

Mkuu hii serikali ni legelege sana na si makini wala sikivu, TBC na waziri wa habari, linatokea jambo zito kama hili watu zaidi ya mia tatu, wanashindwa kuomboleza? nakumbuka mzee Mengi alifariki mwanae EATV na ITV ziliomboleza more zan Ten days, cheki sept 11 leo wenzetu wanavyoomboleza... kama tukio la mwaka jana, ila sishangai maana hata PINDA ambae ni PM hajafika Zanzibarkuomboleza mpaka dakika hii. TBC wangekuwa msitari wa mbele wanazidiwa hata na Issamichuzi blog yake kweli inaomboleza inakusanya salaam za rambirambi na vitu kama hivyo. TBC walipaswa pia serikari legelege
 
Leo september 11,kila television ukifungua unakuta newyork city wanaomboleza,jee maafa waliyopata wao na hapa kwetu zanzibar yana tofauti gani ? Kara yupo au lalala fofo fofo ? Tv zote zinarusha vinyago ni aibu,wenzetu wanatucheka,ukisoma habari katika bbc wana hii ni Big disaster ,jee bado tu hatukubali kuwa huu ni msiba mkubwa ? kudadadeki zao Viongozi wa television,munatia hasira kwelii,ndio maana tunauchukia muungano.
 
Nashukuru kwa comments zenu. Nadhani wametusikia na wameanza kutupa updates. Nawashauri tbc wawe proactive.
 
Mkuu hii serikali ni legelege sana na si makini wala sikivu, TBC na waziri wa habari, linatokea jambo zito kama hili watu zaidi ya mia tatu, wanashindwa kuomboleza? nakumbuka mzee Mengi alifariki mwanae EATV na ITV ziliomboleza more zan Ten days, cheki sept 11 leo wenzetu wanavyoomboleza... kama tukio la mwaka jana, ila sishangai maana hata PINDA ambae ni PM hajafika Zanzibarkuomboleza mpaka dakika hii. TBC wangekuwa msitari wa mbele wanazidiwa hata na Issamichuzi blog yake kweli inaomboleza inakusanya salaam za rambirambi na vitu kama hivyo. TBC walipaswa pia serikari legelege
Kuna haja gani ya kuwafundisha namna ya kuomboleza!.Laana ya Allah ndiyo huwa fundisho kwa asiyejuwa ubinadamu au mwenye kudharau jirani zake kwa faida ya watu wa mbali.Nakusudia....Tanzania na USA.
Siku TBC na wenzao yatakapowapata ndani ya studio zao na majumbani mwao ndipo watajua.
 
Ila kuna haja ya kuangalia upya hizi ajali kubwa zinazo ua watanzania wenzetu zinatokea vp. Mimi nimeshitukia kitu.

26/5/1996. Mv Bukoba ilizama na kuua mamia ya watanzani. Hii ilikuwa baada ya uchaguzi wa 1995. Hali kadhalika mwaka 2001 treni iliua tena mamia ya watazania wenzetu Dodoma pia hii ilikuja mwaka baada ya uchaguzi wa 2000. Haya tena 10/9/2011 meli imezama Zanzibar na kuua tena mamia ya Watanzania hii nayo imekuja mwaka mmoja baada ya uchaguzi wa 2011. Mi nadhani kuna haja ya kuangalia upya hizi ajali isije ikawa watanzania wanatumika kufanikisha maslahi ya watu flani.
FIKIRIA CHUKUA HATUA.

ndo haya mawazo mafupi niliyoonya tangu awali. Hivi haufikirii ubora wa chombo kilichotumika unawaza uchawi?
Mbona 2006 haujataja?
 
nami naamini hivo, tido kafanya mengi na alijua kipi kitangazwe lini. Naona baada ya kupata comments zetu angalau wamestuka na kuweka angalau updates kiasi.

Naamini kuwa kila mtu anaweza fanya kitu fulani kwaajili ya jamii, lakini ni watu wachache sana wanaweza fanya vitu vinavyogusa maisha na mioyo ya walio wengi
mi nafikir hyu mkurugenz wa ss amekosa vipaumbele kwny kazi yke..
 
Nimeguswa sana na msiba huu mkubwa ambao umelikumba Taifa la Tanzania.

Kwa Wenzentu waliotangulia mbele ya haki, Mungu wetu uliye mwema tunaomba uzilaze roho za wenzetu mahali pema peponi. Ameni.

Sisi sote tulioathirika kwa namna moja ama nyingine,Mungu wetu atupe nguvu na atuwezeshe kurudi katika hali ya kawaida kwa haraka ili tuweze kukabiliana na majukumu yaliyo mbele yetu.
 
Leo september 11,kila television ukifungua unakuta newyork city wanaomboleza,jee maafa waliyopata wao na hapa kwetu zanzibar yana tofauti gani ? Kara yupo au lalala fofo fofo ? Tv zote zinarusha vinyago ni aibu,wenzetu wanatucheka,ukisoma habari katika bbc wana hii ni Big disaster ,jee bado tu hatukubali kuwa huu ni msiba mkubwa ? kudadadeki zao Viongozi wa television,munatia hasira kwelii,ndio maana tunauchukia muungano.

hapa tbc inabidi watu wawajibishwe. Hatuwezi kwenda kijingajinga hivi.
 
Kwani kazi yao kama chombo cha habari ni nini?coz watu tunafatila kujua nini kinaendelea kule wala hakuna wanachoonyesha..pia sio watu wote wanafahamu maana ya siku 3 za maombolezo,kazi zitaendelea kesho kama kawaida au hapana..taarifa kama hizi walitakiwa wawe wanazitoa mara kwa mara,watanzania wafahamu
kuna watu wanatujali zaidi,CNN wanaonesha mara kwa mara,achana na hawa wehu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom