Vyombo vya habari vya umma na siku tatu za maombolezo

Juma. W

Senior Member
Mar 28, 2011
131
21
Nilitegemea tbc wangekuwa msitari ya mbele kuunga mkono tangazo la mkuu wa kaya. Cha kushangaza hakuna cha maombolezo wala nn. Sijui ni kutomwelewa mkuu wa kaya au nyodo kwa tunaowalipa posho?
 
.............Mzimu wa Tido Mhando unaendelea kuwala TBC1 ni mpaka waitubie dhambi hii.
 
labda wewe ulitaka waomboleze vipi?
Kwani kazi yao kama chombo cha habari ni nini?coz watu tunafatila kujua nini kinaendelea kule wala hakuna wanachoonyesha..pia sio watu wote wanafahamu maana ya siku 3 za maombolezo,kazi zitaendelea kesho kama kawaida au hapana..taarifa kama hizi walitakiwa wawe wanazitoa mara kwa mara,watanzania wafahamu
 
Mimi niltegemea basi iwe hakuna kazi serikalini .Lakini si bendera yapepea nusu mlingoti ? Maana waekufa watanzania wengi sana wa pande zote 2 kwa kweli .
Hivi MV Bukoba ilipozama mwaka ule hali ilikuwaje visiwani ?
 
Nyie vp si Zanzibar wana TV yao ya Taifa? hapa ndo inakuja umuhimu wa suala la muungano tunao uhitaji, watu wanasema tusizungumzie muungano! kwa hali hi muungano hauna budi kuzungumziwa?
 
Nyie vp si Zanzibar wana TV yao ya Taifa? hapa ndo inakuja umuhimu wa suala la muungano tunao uhitaji, watu wanasema tusizungumzie muungano! kwa hali hi muungano hauna budi kuzungumziwa?

Nakubaliana nawe kabisa kwenye hili it is about time watu tutoke pangoni na kusema kwa sauti kuuubwa barabarani
 
Je ule mjadala wa muungano leo Star TV utaendelea maana wazungumzaji wawaili wanatoka zenj?
 
Mimi niltegemea basi iwe hakuna kazi serikalini .Lakini si bendera yapepea nusu mlingoti ? Maana waekufa watanzania wengi sana wa pande zote 2 kwa kweli .
Hivi MV Bukoba ilipozama mwaka ule hali ilikuwaje visiwani ?

And your message here is?...
 
Nilitegemea tbc wangekuwa msitari ya mbele kuunga mkono tangazo la mkuu wa kaya. Cha kushangaza hakuna cha maombolezo wala nn. Sijui ni kutomwelewa mkuu wa kaya au nyodo kwa tunaowalipa posho?
nasikia muungano ulisha vunjika, kwa hiyo iliyozama ni meli ya wachina na imezamia hukohuko uchina.
 
.............Mzimu wa Tido Mhando unaendelea kuwala TBC1 ni mpaka waitubie dhambi hii.
nami naamini hivo, tido kafanya mengi na alijua kipi kitangazwe lini. Naona baada ya kupata comments zetu angalau wamestuka na kuweka angalau updates kiasi.

Naamini kuwa kila mtu anaweza fanya kitu fulani kwaajili ya jamii, lakini ni watu wachache sana wanaweza fanya vitu vinavyogusa maisha na mioyo ya walio wengi
 
jamani sisi Watanzania tuna mila na desturi zetu za maombolezo,hatuombolezi kizungu kwa kuvaa suti nyeusi tu! Bali kuonesha majonzi kwa kuacha kwa muda starehe,kazi n.k kupata muda wa tafakuri,watu 200 wakuu!
 
tulivyoomboleza kifo cha mwl dunia nzima ilijua tanzania wapo kwenye wingu zito,tujali na hawa wenzetu mamia kwa mamia waliopoteza maisha.
 
poleni sana wafiwa wote na ndugu na jamaa
nilikua naskiza redio leo mchana shuhuda za waliopona chupuchupu
jamani hii nchi yani toka saa 7 uck watu wanakuja okolewa saa 2 asubuhi?
wengi walishindwa himili baridi na mawimbi wakaachia walivyoshika kuwasaidia
so hiyo cku 3 imetolewa na muungano au zenji?
 
Back
Top Bottom