Vyombo vya Habari vimedanganya wagonjwa vifundishwe somo:

akili

Member
May 5, 2008
68
0
LEO ni kile kinachoitwa sikukuu ya wajinga. Sikukuu ambayo haina mashiko yoyote katika mila na utamaduni wetu.
Baadhi ya vyombo vya habari na waandishi wa habari wamedanganywa na kisha kuudanganya umma kwamba Babu wa Loliondo kakodiwa ndege kuja Dar au Zanzibar na hivi sasa kuna mamia ya wagonjwa na ndugu zao wanaohangaika kumfikia Babu kule asipokuwepo.

Kwa taarifa hii ninawaomba wote mziombe redio zote nchini kutangaza kuwa kilichotangazwa ni uongo ili wananchi wasiendelee kuhangaika.
Hata kama tunaikubali desturi hii ya Siku ya Wajinga kuna mambo ambayo kwa waungwana hayastahili kufanyia mzaha. Hii ndio mila ya Kiafrika. Kwa hiyo ugonjwa na ajali hatuufanyii mzaha ingawa kwa kifo baadhi ya makabila yetu hufanyia mzaha lakini sio maradhi na ajali!
Ninaomba serikali na wanasiasa pia walikemee hili na lisijitokeze tena. Na ikiwezekana vyombo vya habari vilivyoshiriki katika kuwadanganya wananchi vilipe fidia kwa usumbufu wananchi walioupata!
 
Nonsense...mimi nimeshangaa even wasomi wanahipa chapuo siku hii........................
 
Back
Top Bottom