Vyombo Vya Habari vianzishe "Debate" Tanzania

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,600
8,741
Imefika wakati wa Vyombo vya habari kuanzisha mijadala "debate" kati ya watu wanao unga mikono agenda za serikali na wale wanao pinga. Mfano swala la Tatizo la umeme ningependa kuona Wapinzani na Serikali wanajadili mbinu za kutatua tatizo kwenye nyombo vya habari hasa radio na TV mbalimbali. Mimi sijui nyie mnafikiria vipi lakini mimi ningependa kuona "debate" za uso kwa uso.
 
Kamundu,
Idea yako nzuri sana nadhani ingekuwa bora zaidi kama ungeifanyia kazi wewe kumfuata Mengi au wamiliki wa vyombo hivi vya habari ukaanzisha kipindi hicho..
 
Mkandara mimi niko mbali sana na Tanzania lakini mimi naona imefikia wakati wa majadiliano ya uso kwa uso kupata ukweli wa mambo na kuheshimiana. Utaratibu wa mahojiano hauleti majibu bali unaongeza majadilano ambayo hayana mwisho. Tanzania tunahitaji "Meet The Press" kama ya USA. Kama kweli kuna wana CCM na wapinzani wanaojiamini na wanaweza kuelezea agenda basi jitokezeni na ku "debate". Vilevile Mwanakijiji angeweza kuweka "debate" kwenye mtandao na siyo lazima za CCM na Chadema hata wanamtandao wenye agenda tofauti!.
 
Mkuu wangu bado inawezekana kabisa, wazo kama hili lifikishe kwa kina Invisible ambao wanaweza kuongea na vyombo vya habari kisha mkwasaidia jinsi ya kuunda mjadala huu upate kufanana na hiyo ya Marekani au hata Hard Talk ya UK..

Kuna jamaa wengine wapo ktk vituo vya nje iwe BBC swahili au VOA wanaweza kusaidia sana mchango ktk kukamilisha kipindi hiki.

Mtu kama Mengi anaweza kukubali haswa mkianza na yeye kuhoji maisha yake, mikasa yake, Ufisadi, mbinu chafu dhidi yake na mengineyo ili mradi apate muda na nafasi ya kujisafisha.
 
Hasa kwa kuzingatia kwamba serikali ina run top down na rais mwenewe mzembe na mwoga, anafikiri bado ni waziri wa nishati na madini na kuna mtu yuko juu yake atampa amri. KKuwakoromea IPTL tu mpaka achukue cue kutoka kwa Zitto, labda kama kuna watu daring katika hizi debates wanaweza kutoa ideas zinazoweza kuchukuliwa na Ikulu. Maana inaonekana Kikwete kawa surrounded na yes men walio interested na kuwa courtesants zaidi ya ku serve the people.
 
Mfano swala la Tatizo la umeme ningependa kuona Wapinzani na Serikali....
Ni wazo zuri kuanzisha mijadala, lakini kwa nini tusiwaachie wataalamu ndio watutafutie ufumbuzi. Kuwaacha wapinzani na serikali kuzungumza itakuwa ni kuendeleza mijadala ambayo haina tija kwa sababu mara nyingi hawa wanaongea siasa tu
 
Back
Top Bottom