Vyombo vya habari Tanzania

Kintiku

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
617
319
Hivi ni ajali au................... kuna vituo vya televisheni zaidi ya saba vinavyorusha taarifa za habari kati ya saa moja jioni na saa mbili usiku. Usihangaike kujaribu kuaangalia taarifa za habari katika kila kituo... ukiangalia moja tu unakuwa umeangalia taarifa za vituo vyote. Taarifa zinafanana, vyanzo vya habari vinafanana, picha na urefu wa habari

Kuna magazeti zaidi ya nane yanayotoka kila siku, huihitaji kununua yote, ukinunua moja tu ushasoma yote maana habari ni ilele, chanzo kilele, style ya uandishi ile ile, yaliyomo yale yale. Je ndo kusema waao mwalimu waandishi wa Bongo mwalimu wao mmoja.

Nawasilisha
 
Kushadidia hoja yangu nimehamishia hapa post yangu kutoka kwenye thread nyingine


Lugha inaweza kuwa kikwazo katika ngazi za kimataifa. Lakini hebu tuangalie pia katika mazingira ya kienyeji (Local News). Wakenya wametuacha mbali sana. Linganisha taarifa ya habari kutoka vituo vinavyotangaza kiswahili kati ya Kenya na TZ, taarifa za habari za Kenya utapenda kuangalia hadi mwisho. Matukio ni yale yale sawa na ya kwetu MFANO; ujambazi, mauaji, wanasiasa, dini etc lakini jinsi wao wanavyoripoti kwa ufasaha, kina na kusawiji habari hakika utafurahia.

Tatizo letu sisi ni ukilaza. Utasikia ''watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia na kuua''.......hao hawasadikiwi tayari hao ni majambazi na wauaji. Kwanini magazeti, radio na Runinga wanaripoti kama watu hao ni wahisiwa. Mfano; matukio ya ajali, mauaji au ujambazi chanzo chao cha habari ni Kamanda wa polisi, hawajishughulishi hata kutafuta upande wa pili wa stori.

Hakuna cha lugha wala nini, tatizo ni ukilaza, uoga, ushamba, kupenda dezo na kutokuwa siriasi na fani. Mfano, hivi juzi Nape na Mwiguru? wamemponda Maalim Seif, ungetegemea mwandishi wa ITV au Channel Ten anu TBC aliye ZNZ tayari kisha mhoji Maalim Seif, huko walioko Dar wamemuhoji Katibu Mkuu wa CCM, na Waziri Mkuu kuhusiana na kauli hizo.

Mfano; Magazeti, radio na Tv zote zimeripoti kuhusu barua ya David Jairo, lakini hakuna hata mmoja aliyemhoji bwana huyo kujua upande wa pili. Wala hakuna aliyeandika kuhusu Mh.Pinda kusema alitaka kumfukuza kazi Bwana Jairo, lakini ''watu'' wakamwambia mzee unaingilia anga za President. Kwangu mimi habari ingekuwa PM hakujua mipaka yake ya kazi...................................angalau kwa wakati wa tukio hilo.
 
Back
Top Bottom