Vyombo vya dola vipo kwa ajili ya nani??

msnajo

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
3,066
1,136
Wakuu salaam.

Naomba tujadili kama GT. Tuweke tofauti zetu za kiitikadi pamoja na vyama pembeni.
Vyombo vya dola hasa mahakama na polisi, wapo kwa ajili au faida ya nani?? Je, ni sisi wananchi au ni wenye uwezo, au watawala? Nimelazimika kuleta huu mjadala kutokana na ukandamizaji na uonevu unaofanywa na vyombo husika kwa wananchi ama waliomaskini au wasiokuwa watawala. Mara nyingi kwa watu wa kawaida (ordinary people) wanapofanya makosa, polisi wanawakamata "fasta" na watuhumiwa nao wanakamatwa "fasta" itakapodhibitika hawana hatia wanaachiwa huru. Mfumo huu umejikita kwa watu wachini! Kwa wakubwa hasa watawala na wenye uwezo wa fedha, polisi wamekuwa wakijishauri kumkamata mtuhumiwa au kuacha kabisa hata kuzungumzia habari zake ili kumlinda. Huyu "Ahmed Msangi", (I dont wish to know him) ametajwa sana kwenye swala la uhalifu wa kumteka na kumjeruhi Dr Uli. Masikitiko yangu, kama ni mtuhumiwa kwa nini polisi wasimhoji walau kuupata ukweli? Huyu Kova, huu mchezo wa kudanganya watanzania, kwa nini asimdanganye mkewe na watoto wake ili kufanikisha mambo fulani kwa faida ya familia yake? Iramba kumetokea fujo na mtu mmoja karipotiwa kufa, kuna watuhumiwa saba kati ya kumi na mbili inasemekana wametoka Dar na wamelipwa ili kuweza kuleta madhara. Cha kushangaza hawajahojiwa pamoja na kwamba kinadharia wanaonekana kuhusika kwa namna moja au nyingine katika fujo zile. Badala yake unapikwa uwongo na kuwahoji watu wa chama fulani ili kuwabambikia kesi! Kwa nafasi yangu kama Mtanzania, haya ndo mambo nina uhakika kwamba yatatowesha amani yetu. Watanzania tumechoka kuonewa na vyombo vya dola, je vinamtumikia nani? Mahakama nazo zinapindisha kesi ili kuwa-favour watu fulani, wanamtumikia nani? Serikali kama chombo kinachotawala watu hakioni umuhimu wowote wa kujali wananchi/watu wake, hata kama wanateseka "no problem" watajua wenyewe!! Wenye uwezo wa kudai haki wanauawa au kujeruhiwa vibaya, wananchi nasi tunatazama. Lakini ni hadi lini? Bob Marley aliwahi kusema "how long shall they kill our prophet while we stand side and look". Tujiulize, serikali na vyombo vyake vya dola vipo kwa ajili ya nani??
Hebu tupeane hoja.
 
chukua hatua mkuu kwa kuanza kuchukua fomu za uongozi ili wakulinde. vyombo vya dola husubiri amri tu ndugu.
 
Kaka nimekuwa na mawazo yanayokaribia kuwa sawa na yako kwenye hili na nimeona wazi tunayo fursa ya kuchukua hatua ya maboresho ya muda mrefu kupitia katiba mpya kama hatutatoa maoni juu ya muundo wa dola kwenye hii katiba mpya haya maswali yatabaki bila majibu kwa vizazi vingi vijavyo lakini tukipeleka maoni tunayoona ni sahii kwenye hili jambo tutaikomboa nchi yetu na haya malalamiko hayatosikika tena kila mtu atatendewa haki kwa uongozi wa katiba mpya.
 
wakuu salaam.

Naomba tujadili kama gt. Tuweke tofauti zetu za kiitikadi pamoja na vyama pembeni.
Vyombo vya dola hasa mahakama na polisi, wapo kwa ajili au faida ya nani?? Je, ni sisi wananchi au ni wenye uwezo, au watawala? Nimelazimika kuleta huu mjadala kutokana na ukandamizaji na uonevu unaofanywa na vyombo husika kwa wananchi ama waliomaskini au wasiokuwa watawala. Mara nyingi kwa watu wa kawaida (ordinary people) wanapofanya makosa, polisi wanawakamata "fasta" na watuhumiwa nao wanakamatwa "fasta" itakapodhibitika hawana hatia wanaachiwa huru. Mfumo huu umejikita kwa watu wachini! Kwa wakubwa hasa watawala na wenye uwezo wa fedha, polisi wamekuwa wakijishauri kumkamata mtuhumiwa au kuacha kabisa hata kuzungumzia habari zake ili kumlinda. Huyu "ahmed msangi", (i dont wish to know him) ametajwa sana kwenye swala la uhalifu wa kumteka na kumjeruhi dr uli. Masikitiko yangu, kama ni mtuhumiwa kwa nini polisi wasimhoji walau kuupata ukweli? Huyu kova, huu mchezo wa kudanganya watanzania, kwa nini asimdanganye mkewe na watoto wake ili kufanikisha mambo fulani kwa faida ya familia yake? Iramba kumetokea fujo na mtu mmoja karipotiwa kufa, kuna watuhumiwa saba kati ya kumi na mbili inasemekana wametoka dar na wamelipwa ili kuweza kuleta madhara. Cha kushangaza hawajahojiwa pamoja na kwamba kinadharia wanaonekana kuhusika kwa namna moja au nyingine katika fujo zile. Badala yake unapikwa uwongo na kuwahoji watu wa chama fulani ili kuwabambikia kesi! Kwa nafasi yangu kama mtanzania, haya ndo mambo nina uhakika kwamba yatatowesha amani yetu. Watanzania tumechoka kuonewa na vyombo vya dola, je vinamtumikia nani? Mahakama nazo zinapindisha kesi ili kuwa-favour watu fulani, wanamtumikia nani? Serikali kama chombo kinachotawala watu hakioni umuhimu wowote wa kujali wananchi/watu wake, hata kama wanateseka "no problem" watajua wenyewe!! Wenye uwezo wa kudai haki wanauawa au kujeruhiwa vibaya, wananchi nasi tunatazama. Lakini ni hadi lini? Bob marley aliwahi kusema "how long shall they kill our prophet while we stand side and look". Tujiulize, serikali na vyombo vyake vya dola vipo kwa ajili ya nani??
Hebu tupeane hoja.

kwenye mfumo wowote wa utawala jukumu la vyombo vya dola ni kuwalinda watawala kwa gharama yoyote ile.
 
watanzania tumekuwa kama makondoo 2, hata tungeambiwa tulipie hewa hii ya mungu tungelipa 2 hata kama ni mafukara! tumefanya taasisi zote za umma kuwa mali ya ccm na mafisadi, lakini ujinga una muda unakwisha, tutafukua hadi makaburi kwa wote waliofilisi na kutumia vibaya madaraka yake
 
wacha pressure time will tell.
Remember: YOU CAN FOOL ALL PEOPLE ONE TIME, BUT YOU CAN'T FOOL PEOPLE ALL TIME.

Also know that THEY WATCHES, BUT WE HAVE TIME by Taliban.
 
Back
Top Bottom