Vyomba vya Usalama vya Z'bar vyatakiwa kufanya uchunguzi wa kina - kutoweka kwa Sheih Farid

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=3]
DSC_0089.JPG
[/h]Waziri wa nchi afisi ya makamo wa pili wa Rais Zanzibar Mh. Mohammed Aboud


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imevitaka vyombo vya ulinzi na usalama nchini kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini kiini cha kutoweka Sheikh Farid Hadi Ahmed na chanzo cha vurugu zilizotokea nchini wiki iliyopita..

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na waziri wa nchi afisi ya makamo wa pili wa Rais Zanzibar Mh. Mohammed Aboud amesema

Kutoweka katika mazingira ya kutatanisha kwa Sheikh Farid kulipelekea kuzuka kwa machafuko katika maeneo kadhaa ya mji wa Zanzibar ambapo mali za watu ziliporwa na kuharibu miundo mbinu ya barabara na kuchoma moto maskani za ccm.

Hivyo ilitaka vyombo vya ulinzi na usalama kufanya tathmini ili kujua kiwango cha hasara kilichotokana na vurugu hizo na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuhusika na kadhia nzima ya Sheikh Farid,vurugu na mauaji ya askari Koplo Said Abrahmani huko Bububu wilaya ya magharibi Unguja.

Aidha vyombo hivyo vimetakiwa kuendelea na kudhibiti hali ya usalama wa nchi kwa wakati wote kwa vile vitendo hivyo vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara na kuhakikisha kwamba havirejei tena.

Taarifa hiyo iliendelea kusisitiza wananchi kuacha vitendo vyenye kuhatarisha amani na utulivu uliopo nchini kwa vile chuki na fujo siku zote kazi yake ni kubomoa na sio kujenga.

Mh. Aboud aliendelea kusema kuwa wale wote wenye dhamira ya kugombanisha wananachi na serikali yao ni vyema waache kufanya hivyo bali jambo la msingi ni kudumisha mashirikiano ili kujenga nchi yetu kwa maslahi ya taifa na vizazi vijavyo.

Amesema kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawashukuru wananchi wote kwa ustahamilivu wao na pia kuvishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri walioifanya kutuliza fujo na vurugu ambapo hivi sasa hali imerejea kuwa ya utulivu.

Aliongeza kuwa hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kudhibiti hali hiyo na kuwaomba wananchi waendelee na shughuli zao za kawaida bila ya wasiwasi.

Kuhusu uchumi wanchi, alisema kuwa adui mkubwa wa uchumi ni kwa nchi kuingia katika vurugu na machafuko kunakopelekea kuvunjika kwa amani na utulivu ambapo zanzibar uchumi wake mkubwa ni kutokana na sekata mama ya utalii ambao huathirika sana kukikwa hakuna amani na utulivu na kurejesha nyuma maendeleo na kuzidisha hali ya umasikini jambo ambalo huongeza upungufu wa ajira kwa vijana wetu

Waziri huyo amewasihi wananchi wa Zanzibar hasa vijana kulinda amani ya nchi ambayo ndio rasilmali kuu ya taifa.

Alisema kuwa panapotokea tatizo au changamoto ya aina yoyote kwa mujibu wa misingi ya utawala bora na wakidemokrasia ni busara kufanyika kwa mazungumzo mioungoni mwa wadau wahusika.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa wazanzibari wote ni ndugu, ni watu wamoja hakuna budi kupendana, kuaminiana, na kusaidiana kwa hivyo viachwe vitendo vyenye kuhatarisha amani na utulivu uliopo chuki na fujo haziannafasi katia ulimwengu huu, kwani vitu hivyo kazi yake ni kubomoa na si kujenga

Sheikh Farid na wenzake wanatarajiwa kufikishwa tenakatika mahkama ya mwanakwerekwe hapo kesho .
 
Back
Top Bottom